- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Utangulizi wa Kumbukumbu ya 25 ya Kampeni ya Srebrenica:
“Miaka 25 Baadaye: Mafunzo kutoka Srebrenica”
Mnamo 11 Julai, 1995, majeshi ya Serbia yalivamia eneo la Waislamu la Srebrenica nchini Bosnia ambapo maelfu ya Waislamu walikuwa wametafuta himaya kutokana na mashambulizi ya jeshi la Serbia kaskazini mashariki mwa Bosnia. Mji huo ulikuwa umetengwa na Umoja wa Mataifa (UN) kama "eneo salama" na kutangazwa kuwa chini ya ulinzi wa UN. Siku zilizo fuatia kutekwa kwa Srebrenica, wanaume na wavulana wa Kiislamu 8000 waliuwawa kinyama na Waserbia hao. Ilitangazwa kuwa ndio ukatili mbaya zaidi kufanyika katika nchi ya Ulaya tangu Vita vya Pili vya Dunia. Sambamba na mauwaji haya, wanawake, watoto na wazee kati ya 25,000 na 30,000 walifurushwa kutoka mjini humo kama sehemu ya kampeni ya kikatili ya Kiserbia ya mauwaji ya kimbari ya Waislamu kutoka katika ardhi zinazo pakana na Jamhuri ya Serbia. Waislamu wa Srebrenica waliahidiwa ulinzi na Umoja wa Mataifa lakini ulinzi huo kamwe haukuja. Waliahidiwa kwamba serikali za kimagharibi zingesitisha mashambulizi ya Waserbia kupitia NATO lakini usaidizi huo kamwe haukuwa.
Mauwaji haya ya halaiki yalikuwa ndio silsila ya ukatili uliofanywa na majeshi ya Serbia dhidi ya Waislamu wa Bosnia katika vita vya Bosnia huku serikali za kiulimwengu – za Waislamu na zisizokuwa za Waislamu – zikitazama.
Miaka kadhaa baada ya mauwaji ya halaiki ya Srebrenica, ulimwengu uliahidi, "Kamwe Haitatokea Tena" na kwamba mafunzo yatapatikana kutokana na doa hili jeusi katika historia ya sasa. Hata hivyo, leo tunaona chinja chinja na uhalifu wa vita vya Bosnia na mauwaji ya halaiki ya Srebrenica yakijirudia dhidi ya Waislamu katika ardhi ya India huku ulimwengu kwa mara nyengine tena unatazama. Mtume (SAW) amesema: «لاَ يُلْدَغُ الْمُؤْمِنُ مِنْ جُحْرٍ وَاحِدٍ مَرَّتَيْنِ» “Muumini hang'atwi katika tundu moja mara mbili.” Hivyo, ni yapi mafunzo halisi yanayo paswa kusomwa kutokana na janga hili la kibinadamu? Vipi kumbukumbu ya matukio haya ya kinyama yaliyo pita yatatusaidia kuunda upya mustakbali wetu kama Waislamu ili kunali usalama na haki? Vipi tutaweza kuvunja turathi hii ya mauwaji ya halaiki yaliyo usibu Ummah wetu… ili historia isiendelee kujirudia?
Kampeni hii imezinduliwa na Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir kinacho tarajia kuzungumzia kadhia hizi.
Dkt. Nazreen Nawaz
Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Jumatatu, 15 Dhu al-Qi'dah 1441 H sawia na 6 Julai 2020 M
Fuatilia Kampeni kwa Lugha Nyenginezo
Taarifa kwa Vyombo kutoka kwa Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Uzinduzi wa Kampeni ya Kumbukumbu ya Mauwaji ya Halaiki ya Srebrenica:
“Miaka 25 Baadaye: Mafunzo kutoka Srebrenica”
Jumatatu, 15 Dhu al-Qi'dah 1441 H Sawia na 6 Julai 2020 M
Alama Ishara za Kampeni
#Srebrenica25YearsOn | |||
#سربرنيتشا_جرح_لم_يندمل | |||
#Srebrenitsa25Yıl |
Video Fupi ya Kampeni
https://hizbut-tahrir.info/sw/index.php/kampeni/918.html#sigProId1934a08240
Ili Kupakua Kipeperushi kwa umbo la PDF
Makala