Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Kampeni ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

"Muokoe Mateka Jannat Bespalova!"

Kutokana na maafa yanayo tekelezwa na serikali ya kihalifu ya Urusi dhidi ya Waislamu wa Urusi, leo, mamia ya Waislamu wanafungwa katika magereza ya Urusi kwa sababu ya kushiriki kwao katika kazi ya Hizb ut Tahrir. Walituhumiwa “ugaidi” kirongo kwa kutegemea uamuzi wa kufedhehesha wa Mahakama ya Upeo wa kuiorodhesha Hizb ut Tahrir kama shirika la kigaidi. Kwa mujibu wa uamuzi huu wa kiajabu, Chama hiki cha Kisiasa cha Kiislamu, kikawa chama cha “kigaidi”.  

Kutokana na mkazo wa sheria za Urusi dhidi ya wanachama wa chama hiki, mashtaka yakazuliwa sio kwa msingi wa sheria za “siasa kali” katika katiba bali kwa msingi wa sheria za “ugaidi”; ambapo vifungo vinaweza kufikia mpaka miaka ishirini gerezani.  

Utekelezaji “sheria” hizi ulipelekea kufungua mwanya wa mateso katika maeneo yote ya Urusi, ikiwemo St. Petersburg, ambako idadi kubwa ya wabebaji ulinganizi wamekamatwa katika muda wa miaka michache iliyopita. Mnamo tarehe 24 Novemba huduma za usalama zilimkamata mke wa mmoja wa wafungwa aliye hukumiwa miaka 12 gerezani, naye ni, Issa Rahimov mwanachama wa Hizb ut Tahrir. Mkewe Issa ni mwenye asili ya Kirusi; alisilimu na kubadilisha jina lake kutoka Allan na kuwa Jannat Bespalova. Alikamatwa kwa kufanya kazi kwake na Hizb ut Tahrir na kutupwa gerezani ambamo wahalifu huzuiliwa. Hatimaye iliamuliwa, mnamo Januari 2018, kuongezwa muda wa kifungo cha dada huyu kwa miezi miwili mengine, hii ikimaanisha atasalia ndani ya magereza ya Urusi hadi 16/03/2018, tarehe inayofuata ya kusikizwa kesi kotini. Allah (swt) asema:

قَدْ بَدَتِ الْبَغْضَاءُ مِنْ أَفْوَاهِهِمْ وَمَا تُخْفِي صُدُورُهُمْ أَكْبَرُ قَدْ بَيَّنَّا لَكُمُ الآيَاتِ إِنْ كُنْتُمْ تَعْقِلُونَ

“Imekwisha fichuka chuki yao katika midomo yao. Na yanayo ficha vifua vyao ni makubwa zaidi. Tumekwisha kubainishieni ishara ikiwa nyinyi mtayatia akilini” [Al-i-Imran: 118]

Kutokana na matukio yote haya, Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir imeanzisha kampeni ya kiulimwengu inayoitwa “Muokoe Mateka Jannat Bespalova!” Jibu muwafaka kwa matendo ya Urusi dhidi ya wanawake wanyonge wa Kiislamu, ni kufanya kazi na Hizb ut Tahrir kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume. Hii ndio njia sahihi ya kupata radhi za Allah (swt). Kuregesha utawala wa Kiislamu kutawapa afueni Waislamu kutokana na sheria za kikafiri na uovu wa serikali za kidhalimu. Allah (swt) asema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo lenye kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Al-Anfal: 24].

Ewe Allah, tunakuomba usaidizi wako na umbariki dada yetu Jannat kwa himaya yako, na mumewe na Waislamu wote wanaozuiliwa katika magereza ya makatili pasi na kosa lolote; na Waislamu wanaodhalilishwa kwa sababu ya kubeba kwao ulinganizi wa Kiislamu. Ewe Allah, tunakuomba uilete karibu siku ile ambayo Waislamu wataregesha tena utawala wa Uislamu ardhini, kwa nusra yako, na kuwaadhibu wale wote waliowashambulia vijana na mabinti wa Umma wetu mtukufu, Ewe Allah ikubali dua yetu, Ameen. 

Jumamosi 15 Jumada Al-Akhir 1439 H - 03 Machi 2018 M

 

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 09 Februari 2020 14:50

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu