- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir:
Kampeni ya Kitengo cha Wanawake ya Ramadhan: “Ramadhan ni njia ya mafanikio”
(Logo)
Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema katika Kitabu Chake kitukufu: شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِيَ أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى﴾ لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِّنَ الْهُدَى وَالْفُرْقَانِ﴿ “Mwezi wa Ramadhan ambao imeteremshwa humo Qur'ani kuwa ni uwongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uwongofu na upambanuzi”. Mwezi mtukufu wa Ramadhan ni wakati muafaka kwetu sisi Waislamu kuzingatia na kutafakari upya jinsi tulivyo karibu na Mola Mlezi wetu (swt), na vilevile jinsi tunavyoliona lengo na kipimo chetu cha kweli maishani, na jinsi tunavyofafanua maana ya mafanikio katika maisha na jinsi tunavyoyafikia. Ni mwezi ambao unashikilia ndani yake uwezo wa kutupa “njia ya mafanikio.”
Katika jamii tunazoishi ndani yake, tumezungukwa na mitazamo mingi, athari, na mashinikizo yanazoweza kutengeneza mtazamo wetu wa mafanikio. Lakini upi ufafanuzi wa Muumba kuhusu mafanikio? Je, tutayafikiaje kupitia matendo yetu binafsi, ndoa zetu, maisha ya familia zetu, mambo yetu ya kifedha, na vipengee vyengine vya maisha yetu? Je, ni upi mtazamo sahihi wa mwanamke aliyefanikiwa kwa mujibu wa Uislamu? Zaidi ya hayo, Muislamu anatafuta mafanikio si kwa ajili yake tu, bali hata kwa Umma wake wa Kiislamu na dini yetu ya Kiislamu. Je, sisi kama Umma wa Kiislamu tunapaswa kuutazama vipi Umma na dola iliyofanikiwa na iliyoendelea, na tunawezaje kufikia lengo hili? Je, ni kichocheo gani cha mafanikio cha kutatua matatizo mengi ya kisiasa, kiuchumi na kijamii tunayokabiliana nayo kwa sasa, na ni zipi sifa za harakati au chama chenye mafanikio ili kufikia mabadiliko ya kweli katika nchi zetu na kwa wanadamu? Tutashughulikia maswali haya na mengine katika maudhui yetu ya mwezi huu uliobarikiwa katika Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir: “Ramadhan: Njia ya Mafanikio.” Mnaweza kufuatilia warsha ya Ramadhan kwenye link iliyopo hapo chini. Tunamuomba Mwenyezi Mungu maudhui hizi ziwe ni njia ya kuangaza njia kwa Umma huu kufikia mafanikio ya kweli hapa duniani na kesho akhera, Mungu Mungu akipenda.
﴿ذَلِكَ الْكِتَابُ لاَ رَيْبَ فِيهِ هُدًى لِّلْمُتَّقِينَ * الَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِالْغَيْبِ وَيُقِيمُونَ الصَّلاةَ وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنفِقُونَ * والَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِمَا أُنزِلَ إِلَيْكَ وَمَا أُنزِلَ مِن قَبْلِكَ وَبِالآخِرَةِ هُمْ يُوقِنُونَ * أُوْلَـئِكَ عَلَى هُدًى مِّن رَّبِّهِمْ وَأُوْلَـئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ﴾
“Hiki ni Kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake; ni uwongofu kwa wachamungu. Ambao huyaamini ya ghaibu na hushika Sala, na hutoa katika tuliyo wapa. Na ambao wanayaamini yaliyo teremshwa kwako, na yaliyo teremshwa kabla yako; na Akhera wana yakini nayo. Hao wapo juu ya uwongofu utokao kwa Mola wao Mlezi, na hao ndio walio fanikiwa.” [Al-Baqara: 2-5]
Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir
jumamosi, 01 Ramadhan Al-Mubarak 1446 H sawia na 01 Machi 2025 M
(Banner Hapa)
- Kijitabu cha Maelezo cha Kampeni ya Ramadhan -
Ili Kupakua Kijitabu cha Maelezo kwa Umbo la (PDF)
Bonyeza Hapa
- Alama Ishara za Kampeni ya Ramadhan -
#رمضان_سبيل_الفلاح
#Gateway2Success
- Fuatilia Kampeni ya Ramadhan katika Mitandao ya Kijamii -
QANITATHT1: (Facebook)
https://www.facebook.com/QanitatHT1
@ALQANITAT: (Mtandao wa X)
@WOMEN_SHARIA: (Instagram)
https://www.instagram.com/women_sharia?igsh=NTc4MTIwNjQ2YQ==