Jumamosi, 11 Rajab 1446 | 2025/01/11
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Kurudisha Khilafah: Suluhisho kwa Matatizo ya Somalia

Habari:

  • Vurugu za kuhairishwa kwa uchaguzi wa kidemokrasia.
  • Watu milioni 5.2 wanakadiriwa kuhitaji msaada wa kibinadamu ikijumuisha watoto milioni 3 kutokana na athari ya mafuriko, uvamizi wa nzige na janga linaloendelea la Covid-19.
  • Wanafunzi wengi kufeli mitihani.
  • Kitengo cha kijeshi cha America barani Afrika (AFRICOM) kimekiri kuwaua raia wa Somalia katika oparesheni zake za kijeshi nchini humo.
  • Serikali ya Uingereza imelikabidhi Jeshi la Kitaifa la Somalia zana za kijeshi.

(Chanzo: Radio Daslan)

Maoni:

Somalia ni taifa ambalo linaruka janga kuingia janga jingine yote yakichochewa na wakoloni Wamagharibi wakiongozwa na Amerika na washirika wake upande mmoja na Ulaya, hususan Uingereza na washirika wake upande mwingine. Pande zote mbili zinazozana ili kudhibiti uongozi wa Somalia na hatimaye kupora rasilimali zake. Kilele cha mizozo ni pale ambapo Siad Barre, mtawala aliyekuwa anaegemea mrengo wa Amerika alipopinduliwa mnamo 1991. Katika kipindi cha utawala wa Barre makampuni ya mafuta ya Kiamerika kama vile Chevron, Conoco, Philips na Amoco yalifurahia mgao mkubwa wa sehemu za mafuta nchini Somalia. Kuanguka kwa kibaraka wao mtiifu ilipelekea utawala wa Bush kuwatuma wanajeshi wa Amerika (kuivamia) Somalia ili kulinda maslahi yake yaliyokuwa yametishiwa kwa pazia ya kuweka ulinzi kwa msaada uliotumwa Somalia. Somalia hadi hivi sasa inaendeshwa kwa mujibu wa mchoro wa Amerika kupitia Farmajo, Rais wa sasa nchini Somalia.

Somalia itaendelea kuzama ndani ya moto wa usekula kwa kadri itakavyo endelea kuukumbatia mfumo wa kisekula wa kirasilimali na nidhamu yake ya sumu ya kiutawala ya kidemokrasia inayopigiwa debe na wakoloni Wamagharibi waliojibandikiza kuwa ni wawekezaji na washirika wa Somalia. Wamagharibi wanang’ang’ana kuhakikisha kwamba Somalia inabakia nchi yenye Waislamu wengi lakini wasiokuwa na kitambulisho sahihi cha Uislamu kwa maana Muislamu kwa jina lakini msekula kifikra, kiufahamu, kitabia na kivitendo. Hivyo basi, Somalia inabakia kuwa dola tiifu inayotumika kama uwanja wa vita vya kiwakala baina ya dola za Kimagharibi zinazoshindana baina yao pasina kuzingatia hali mbaya na ya kutamausha ya watu wenyeji ambao wanataabika kutokana na mikasa mingi.

Njia pekee ya kusuluhisha shida za Somalia ni kwa kukata mahusiano na wakoloni Wamagharibi na washirika wao. Hususan Amerika ambayo mikono yake miovu imejaa damu za Waislamu nchini Somalia lazima ikatwe kwa ukamilifu kwa kuwa ndiyo inayowapa uhai na silaha wasaliti wanaopiga njama walioko uongozini nchini Somalia. Ifuatiwe na kukumbatia ulinganizi wa kurudisha tena maisha ya Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume. Chini ya Khilafah, Somalia itafurahia amani, ustawi na utulivu wa kikweli na watu wake watapata cheo, hadhi na heshima kwa damu na mali zao.

Nidhamu ya Khilafah itawawezesha watu nchini Somalia kuwa na utambulisho wa Kiislamu kutokana na kutekelezwa kwa nidhamu ya elimu ya Kiislamu ambayo itawafunza thaqafa ya Kiislamu na kuyeyusha fikra zao kutoka kuwa ni za kisekula hadi kuwa ni za Kiislamu. Kwa kuongezea, njama za kiuchumi kama vile njaa, umasikini n.k zinazoongozwa na mashirika ya kirasilimali zitafutiliwa mbali kwa kutekelezwa nidhamu ya uchumi ya Kiislamu ambayo inajizatiti kuwahifadhi watu maisha yao kwa kuwadhaminia raia ndani ya Khilafah njia za kutosha ili kukidhi mahitaji yao msingi kwa maana chakula, makaazi na mavazi na kuwakidhia mahitaji ya kijamii kama usalama, elimu na afya. 

Imeandikwa kwa ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Ali Nassoro Ali

Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu