- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Ni Nidhamu ya Uadilifu ya Kiislamu Pekee Ndio Inayoweza Kutufanya Tuhisi kuwa na Amani na Usalama
Habari:
Lahore: Polisi wa Punjab wameshuhudia ongezeko kubwa sana la visa vya ubakaji kote mkoani humo katika kipindi cha mwezi wa Septemba. (Chanzo: The news)
Maoni:
Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Idara ya Polisi ya Punjab, kesi 2523 za ubakaji zilisajiliwa katika mkoa huo. Ripoti hiyo ilisema kuwa visa 132 vya ubakaji wa magenge vilisajiliwa katika mwaka huu. Tukio la hivi karibuni la ubakaji wa genge wa Motorway kwa mara nyengine tena limetikisa taifa. Hili sio tukio la kwanza la ukatili kama huo na ukizingatia hali ya sheria na utulivu, halitakuwa la mwisho. Kuanzia kulaumiwa kwa waathiriwa hadi kushambuliwa kwa wanaume, aina zote za maoni zilionekana. Mashirika ya kijamii yamefanya maandamano ambayo yalionyesha ubakaji kama uhalifu wa kijinsia na hisia za chuki kwa wanaume zilionyeshwa bila kufahamu kuwa uhalifu kama huo unazungumzia uvunjaji wa sheria. Wahalifu wamesikia visa vingi ambapo mkosaji hukwepa adhabu ya uhalifu huu na hili huwapelekea kutenda uhalifu huo huo. Pia wahalifu wengi wana rekodi ya aina hiyo hiyo ya uhalifu unaofanywa mara kwa mara; kutokamatwa au kuadhibiwa huwafanya wajiamini zaidi.
Kukithiri kwa uhalifu katika jamii sio tu kunaonyesha kuporomoka kwa maadili pekee bali pia kukosekana kwa adhabu. Hata kama mkosaji atakamatwa, mchakato wa haki ni mrefu na wenye kumdhalilisha mwathiriwa kiasi kwamba mwathiriwa anaweza kuchagua ubora wa kutoripoti kesi hiyo. Kwa hivyo pamoja na kesi hizi zilizoripotiwa kuna kesi kadhaa ambazo hazijaripotiwa kamwe. Ingawa Sheria ya Hadud iliyotangazwa na Rais Zia ul Haq inaahidi adhabu za Kiislamu, mahakama hazihukumu wala kutoa kifungo, badala yake zinawaacha washtakiwa kuoza gerezani hata kama hawana hatia. Kwa hivyo chini ya mfumo wa uadilifu wa sasa tuna wahalifu wanaotembea wakiwa huru na kufanya uhalifu tena na tena na watu wasio na hatia wamefungwa gerezani wakisubiri kesi yao ifanyike.
Suluhisho la hili na matatizo mengine ambayo Ummah unakabiliwa nayo ni utakabikishaji kamili wa Uislamu. Kukabiliana na uhalifu kupitia kutekeleza hudud za Kiislamu hakika kutashusha kiwango cha uhalifu kwani adhabu zitafanyika kwa ufahamu wa umma na mbele ya hadhira kulingana na hukmu za Shariah. Hili hakika litaweka mfano na watu watajua kuwa kufanya uhalifu kutakuwa na matokeo mabaya kama kupoteza maisha au kupoteza kiungo. Jukumu la polisi litakuwa kulinda watu na kuhakikisha kuwa watu wanajisikia salama kila mahali. Mfumo wa uadilifu wa Kiislamu utakuwa na makadhi wanaomcha Mungu ambao watakuwepo hapo kwa kigezo cha maarifa na uwezo wao.
Utekelezaji wa adhabu ni wajibu kwa wale walio na mamlaka na wawakilishi wao. Katika hali ambapo hakuna dola ya Kiislamu inayotawala na Hukm (sheria) ya Mwenyezi Mungu, ni wajibu kwa Waislamu wote kufanya kazi kwa ikhlasi na kwa bidii kusimamisha mamlaka yanayohukumu kwa Uislamu.
(فَاحْكُم بَيْنَهُم بِمَا أَنزَلَ اللَّهُ وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاءَهُمْ عَمَّا جَاءَكَ مِنَ الْحَقِّ)
“Basi hukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao ukaacha Haki iliyo kujia.” [Al-Maida: 48]
Imeandika kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Ikhlaq Jehan