Jumatano, 23 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Je Chanjo za Virusi vya Korona ndio Suluhisho la Janga hili?

Habari:

Pakistani ndio nchi ya hivi karibuni zaidi kutangaza chanjo dhidi ya virusi vya Korona.  Dkt. Nausheen Hamid Katibu wa Bunge anayeshughulikia Afya ya Taifa alisema kwamba Pakistan itaanza kuwafanyia chanjo raia wake katika robo ya pili ya mwaka 2021. [1] Kama ambavyo nchi nyingi zimekuwa zikitangaza juhudi za kuwafanyia chanjo raia wake ili kuwakinga dhidi ya virusi vya Korona, swali la msingi ni kuhusu ufanisi wa chanjo inayotolewa.

Maelezo:

Tangu kutokea kwa janga la virusi vya Korona nchini China mwaka mmoja uliopita, kumekuwa na ushindani wa kidunia katika kuzalisha chanjo imara dhidi ya ugonjwa huo. Kutokana na chanzo maalumu New York Times kuna chanjo 58 zinazofanyiwa majaribio kwa mwanadamu katika maabara na kwa kiwango kidogo chanjo 86 zimeshafanyiwa majaribio kwa wanyama. [2] baadhi katika hizo zimeruhusiwa kufanyiwa majaribio kwa binadamu, chanjo ya China inayoitwa Sinopharm na Sinovac na chanjo iliyozalishwa na Pfizer, Moderna, na AstraZeneca ndizo ambazo zimekuwa maarufu. Pfizer inadai kwamba chanjo yake ina ufanisi wa asilimia 95 katika kupambana na Korona. [3] ukiachana na changamoto zilitokea na njia tofauti tofauti zilizo tumika katika kutengeneza chanjo, upatikanaji mgumu wa taarifa umepelekea ugumu katika kupima ufanisi wa chanjo dhidi ya virusi vya Korona.

Rekodi taarifa za chanzo dhidi ya ugonjwa wa mafua ya kawaida (ugonjwa unaoathiri mfumo wa upumuaji) zimeonyesha dosari katika ufanisi wa chanjo ya virusi vya Korona. Umahiri wake umekuwa ukitofautiana mwaka hadi mwaka, ukianzia chini ya asilimia 10 mwaka 2004-05 hadi kukua na kufikia asilimia 60 mwaka 2010-11. Kwa mustawa, imekuwa na ufanisi kwa asilimia 40—maana yake ni kwamba maradhi yamedhibitiwa kwa asilimia 40. [4] kiwango kidogo cha ufanisi kimesababishwa na madhara tofauti tofauti yaliyosababishwa na mafua, na hivyo kupelekea ugumu katika kupata chanjo moja itakayoweza kutibu aina zote za madhara. Covid-19 ni sehemu ya familia ya virusi vya Korona na hivyo hupelekea changamoto zile zile kwa watengenezaji wa chanjo. Inafahamika wazi kwamba virusi vya Korona vimegawanyika katika hali tofauti tofauti, ukijumuisha na upatikanaji mgumu wa taarifa ni wazi kwamba kuna shaka katika ufanisi wa chanjo iliyopo.

Zaidi ya hayo, kuifanya chanjo kuwa chanjo kuna hatari yake, na hiyo ni kwa wagonjwa, ambao hupata matatizo baada ya matumizi ya chanjo—wengine hutishiwa maisha yao. Madhara ya pembeni ya baada ya matumizi ya chanjo ya mafua yanajumuisha maumivu makali ya viungo, kuwa mwekundu, kujiskia vibaya, homa, maumivu ya misuli, kichefuchefu na hata kupelekea kifo. Pamoja na kuwepo kwa chanjo lakini watu 650,000 wanakufa kila mwaka [5].

Kwa miaka kadhaa chanjo zimekuwa zikifanyiwa majaribio ili kuzifanya ziwe salama zaidi kabla watu hawajaanza kuzitumia. Ukurupukaji katika kuruhusu matumizi ya chanjo ya virusi vya Korona ni wazi kwamba chanjo hiyo haiwezi kuwa na ufanisi, na huenda dunia itaendelea na mbinu ya masafa ya kijamii kwa miaka mingi ijayo. Ni bora, chanjo inayotakiwa kutibu virusi vya Korona iwe ni msingi imara katika kupambana na ugonjwa huu. Kama ilivyo kwa mafua haitarajiwi kwamba virusi vya Korona vitaangamizwa, na dunia itaendelea kuishi na maradhi haya.

Tofauti na ubepari – ambao makundi yenye uchu yamekuwa yakihodhi utoaji  huduma za matibabu  (madawa, chanjo, dawa za kawaida) – Uislamu kwa kiwango cha juu umelenga zaidi katika kulinda maisha ya mwanadamu, katika Uislamu, wahyi ndio unaotangulizwa na sayansi ni kiwezeshaji katika uvumbuzi wa tiba mpya dhidi ya magonjwa . Mwenyezi Mungu (swt) anasema:

[وَإِذَا مَرِضْتُ فَهُوَ يَشْفِينِ]

“Na ninapo ugua ni Yeye ndiye anaye niponesha.” [Ash-Shu'araa: 80]

Imeandikwa kwa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Abdul Majeed Bhatti

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu