- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Usalama wa Chakula katika Uislamu
(Imetafsiriwa)
Habari:
Katika wiki zilizopita, kumekuwa na zogo kuhusu suala la usalama wa chakula, ambalo linasemekana kuchochewa na vita vya Urusi na Ukraine. Hili linachochewa zaidi na kusitisha uuzaji nje wa ngano na serikali ya India kutokana na mawimbi ya joto ambayo husababisha uzalishaji mdogo wa ngano. Hata hivyo, kulingana na Wizara ya Biashara ya Ndani na Masuala ya Watumiaji (KPDNHEP), usambazaji wa unga wa ngano nchini hautarajiwi kuathiriwa, kwani Malaysia inaagiza asilimia 80 ya ngano kutoka Australia na nyingine kutoka Marekani, Canada na Ukraine. Kisha, kuna kupungua kwa ghafla kwa usambazaji wa kuku na kusababisha serikali kutangaza masuluhisho kadhaa ya muda mfupi ya kukabiliana na tatizo hilo. Miongoni mwa mengine, serikali ingesimamisha mauzo yake ya nje ya kuku milioni 3.6 kwa mwezi kuanzia Juni 1, 2022 hadi bei na hifadhi ya kuku nchini itengemee. Kando na hayo, serikali pia inapanga kuweka hifadhi salama ya kuku na kuondoa vibali vilivyoidhinishwa (AP) vya kuku ili kuongeza fursa za ushiriki wa waagizaji katika kutoa vyanzo zaidi vya kuku.
Maoni:
Chakula ni mojawapo ya mahitaji msingi ya binadamu ili kuhakikisha uhai pamoja na masuala ya afya. Kila binadamu anahitaji kiasi fulani cha chakula kila siku ili kuhakikisha usalama wa maisha yake. Imepokewa kutoka kwa Ubaydullah bin Mihsan: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake.
«مَنْ أَصْبَحَ مِنْكُمْ آمِنًا فِي سِرْبِهِ مُعَافًى فِي جَسَدِهِ عِنْدَهُ قُوتُ يَوْمِهِ فَكَأَنَّمَا حِيزَتْ لَهُ الدُّنْيَا»
“Yeyote anayepambaukiwa miongoni mwenu akiwa na usalama katika boma lake, mwenye afya katika mwili wake, aliye na chakula cha siku yake, basi ni kama amepewa ulimwengu mzima.” [al-Tirmidhī 2346].
Huo ndio mfano wa Mtume (saw) kuhusu chakula anachohitaji mtu kila siku. Uislamu umepanga mambo ya chakula yaendeshwe kwa mujibu wa maumbile ya mwanadamu. Uislamu pia unapanga jinsi ya kuondokana na matatizo ya lishe ambayo yanaweza kuwepo katika jamii na nchi. Ukosefu wa chakula katika jamii au nchi unaweza kutokea kutokana na sababu kadhaa zikiwemo ukiritimba, mikurupuko ya maradhi, hali mbaya ya hewa, majanga ya kimaumbile, migogoro ya muda mrefu, vita na kadhalika. Tatizo la uhaba wa chakula linaweza kuenea duniani kote, zaidi katika ulimwengu wa kisasa, ambapo nchi zina mahusiano magumu ya kuagiza na kuuza nje. Mambo haya yatazaa mzozo wa chakula duniani ambao unaangukia chini ya mwavuli wa masuala ya usalama wa chakula. Usalama wa chakula kwa nchi kwa ujumla unamaanisha uwezo wa nchi kufikia uzalishaji wa kilimo kwa kiwango cha kutosha au cha ziada, kwa mahitaji ya watu wake, ili isitegemee tena chakula kinachoagizwa kutoka nchi zingine. Kisiasa kushindwa kwa nchi kuwapatia watu wake chakula cha kutosha kutaifanya nchi kutegemea nchi nyingine na kuruhusu nchi nyingine kuzitawala. Leo, nchi nyingi za Kiislamu zinategemea kivitendo dola za makafiri za kigeni sio tu kwa chakula chao bali karibu nyanja zote za maisha! Si vigumu sana kuhitimisha kwamba utawala wa kibepari wa dola hizi za makafiri kwa maumbile yake yenyewe, huathiriwa na migogoro mingi ya kibinadamu, ikiwa ni pamoja na shida ya chakula tunayoikabili sasa.
Ni jambo lisilopingika kwamba mgogoro wa chakula unaweza kutokea kutokana na sababu zilizotolewa hapo juu, kwa hakika hili lilitokea wakati wa utawala wa Khilafah. Hata hivyo, katika hali ya kawaida, haiwezekani kwamba ulimwengu wote utakabiliwa na hali sawa wakati mmoja. Wakati njaa ilipotokea Madina wakati wa utawala wa Umar al-Khattab (ra), kando na uongozi wake wa kupigiwa mfano na usimamizi mzuri na wenye ufanisi, pia alitatua tatizo la uhaba wa chakula kwa kumwamuru gavana wake huko Misri, Amr bin al-As, kuleta nafaka kutoka Misri hadi Hijaz. Kimsingi, dola ya Kiislamu inawajibu wa kuhakikisha kwamba ugavi wa chakula daima unatosha na unagawanywa kwa haki, ama kwa kununua vifaa au kuleta kutoka maeneo mengine au kwa njia nyingine yoyote iliyo ndani ya mipaka ya Sharia ya Kiislamu ambayo ingeweza kutatua tatizo la upungufu wa chakula. Dola pia inapaswa kutabikisha sheria za ardhi ya kilimo barabara kama ilivyoainishwa na hukmu za Sharia na kuendelea kuweka juhudi kubwa katika utafiti na maendeleo yanayohusiana na usalama wa chakula. Uislamu pia unasisitiza juu ya wajibu wa umma kujaliana. Ibn Abbas amepokea kutoka kwa Mtume (Rehma na amani zimshukie) akisema:
«لَيْسَ الْمُؤْمِنُ الَّذِي يَشْبَعُ وَجَارُهُ جَائِعٌ إِلَى جَنْبِهِ»
“Si katika Muumini yule ambaye anashiba na jirani yake ubavuni mwake ana njaa.” [al-Sunan al-Kubrá 19049].
Zaidi ya hayo, kuna hukmu za zaka na mafundisho mengine mengi ya Kiislamu yanayosisitiza kuwa Waislamu ni ndugu na hawapaswi kuruhusu Waislamu wenzao na raia wa dola kuwa katika njaa au dhiki. Kwa ufupi, endapo Uislamu utatabikishwa kikamilifu chini ya Khalifa mwenye ikhlasi, usalama wa chakula kamwe haitakuwa ni kadhia!
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Dkt. Mohammad – Malaysia