Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Kukutana na Muuaji Aliyejaa Damu Hupakaza Damu Mikononi, Ewe Erdoğan!

(Imetafsiriwa)

Habari:

Rais Erdoğan anakwenda Sochi mnamo Agosti 5 kukutana na kiongozi wa Urusi Putin. Erdoğan na Putin watajadili ukanda wa nafaka, vita vya Ukraine na Urusi, uwezekano wa operesheni ya Uturuki Syria na Kiwanda cha Nyuklia cha Akkuyu. (03.08.2022 haberler.com)

Maoni:

Erdoğan atakutana na Putin kwa mara ya 5 mjini Sochi. Mkutano wa mwisho wa Sochi wa viongozi hao wawili ulifanyika mnamo Septemba 29, 2021. Atakutana na Putin kwa mara ya pili ndani ya siku 17. Licha ya Mkataba wa Sochi wenye nukta 10 uliotiwa saini na Erdoğan na Putin mnamo 2019, Urusi inaendelea kuwachinja Waislamu huko Idlib. Watu 7 wakiwemo watoto 4 waliuawa katika shambulizi la anga lililotekelezwa na Urusi kwenye wilaya ya Jisr ash-Shugur nchini Syria mnamo Julai 22. Erdoğan kuna uwezekano mkubwa atakutana na Putin, mchinjaji aliyegubikwa na damu ya Waislamu na ambaye hatosheki na damu kama zimwi, huko Sochi, kupata maslahi ya Marekani au kuwasilisha ujumbe wa Amerika.

Putin anafahamu kuwa Erdoğan ametumwa na bwana wake Marekani kumdhalilisha na kumshusha cheo. Ndio maana Putin alimdhalilisha Erdoğan mara kwa mara katika mikutano yao kwa sababu Erdoğan sio sawasawa yake. Kwa mfano, Erdoğan daima alikaribishwa katika ngazi ya gavana wakati wa mikutano ya Sochi. Nyakati ambazo aliwekwa nje kwa dakika 2 kabla ya kuingizwa kwenye chumba rasmi cha mikutano huko Kremlin kukutana na Putin mnamo Machi 5, 2020 iliyopeperushwa kwenye runinga ya serikali ya Urusi. Lazima itakuwa ni ulipizaji kisasi kwa hili, kwa nyakati ambazo Erdoğan alimfanya Putin asubiri kwa sekunde 50 kwenye mkutano wa kilele uliofanyika Tehran, mji mkuu wa Iran, uliopeperushwa sana kwenye vyombo vya habari vya kimataifa. Inaonekana Erdoğan huku akijua kuwa atadhalilishwa, hawezi kuvumilia udhalilishwaji kwa kwenda Sochi kulingana na maagizo kutoka Marekani. Inawezekana, Putin atalipiza kisasi kwa Erdoğan kwa kumfanya asubiri jijini Tehran.

Inachekesha sana kwamba Erdoğan alikutana na Putin, ambaye Amerika inamtaja kama "jambazi", "dikteta muuaji" na "mhalifu wa kivita". Mkutano wa Erdoğan na mtu kama huyo una uwezekano mkubwa wa kufanywa tu kwa idhini ya Marekani pekee. Marekani yaitaka Urusi kujiondoa Syria. Katika tovuti zenye vyanzo vya kijasusi vya kigeni, vyombo vya habari na habari vinatajwa na "duru za kijeshi" zisizojulikana kwamba "Urusi, iliyokwama nchini Ukraine, iko tayari kuutoa muhanga uwepo wake wa kijeshi nchini Syria." Erdoğan anajaribu kumshawishi Putin kujiondoa Syria katika mazungumzo haya. Kwa kweli, hizi ni ziara za kushawishi badala ya mikutano ya kilele. Ukweli kwamba Syria ni miongoni mwa ajenda zitakazojadiliwa huko Sochi unathibitisha hili.

Yeyote anayekutana na muuaji hakika atajipaka damu kutoka katika mikono ya muuaji. Urusi iliwachinja Waislamu huko Chechnya na Syria, na bado inaendelea kufanya hivyo. Haiwezekani kutojipaka damu ya Muislamu mikononi mwa mtu anayepeana mikono na mtu aliyejaa kama huyo. Erdoğan ima hajui hili, au inabidi akutane na muuaji aliyemwaga damu kulingana na maagizo kutoka kwa mtu asiyeweza kumpinga kwa kisingizio cha maslahi ya kitaifa (maslahi ya Marekani) ingawa anajua.

Kuna jibu moja pekee linaloweza kutolewa kwa muuaji huyu wa Kirusi. Na hilo ni vita. Ni kulipiza kisasi damu ya Waislamu aliyoimwaga nchini Syria na kwengineko. Lakini kwa bahati mbaya, haitarajiwi kwamba mtu kama Erdoğan, anayefanya kazi kwa amri ya bwana wake, atalipa kisasi kwa Waislamu. Kwa sababu bwana wake pia ni muuaji wa Waislamu. Imewachinja Waislamu wasio na hatia nchini Afghanistan, Iraq, Syria, Yemen na nchi nyingine za Kiislamu, ima moja kwa moja au kwa kutumia ndege zisizo na rubani, na inaendelea kufanya hivyo.

Ni Dola ya Khilafah pekee ndiyo inayoweza kulipiza kisasi cha damu ya Waislamu kutoka Urusi pamoja na Marekani. Kwa sababu kwa mujibu wa Khilafah, damu ya Muislamu ina thamani zaidi kuliko kuvunjwa kwa Ka'bah jiwe baada ya jiwe na kuangamia wa ulimwengu wote. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

«لَزَوَالُ الدُّنْيَا أَهْوَنُ عِنْدَ اللَّهِ مِنْ قَتْلِ رَجُلٍ مُسْلِمٍ» Kuangamia kwa dunia nzima ni sahali mbele ya Mwenyezi Mungu kuliko kumuua Muislamu mmoja.” (Nisa'i and Tirmidhi)

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Ercan Tekinbaş

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu