Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Taliban Waliwasili jijini Moscow kama Wafanyibiashara badala ya Kufikisha Risala kutoka kwa Mwenyezi Mungu!

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mnamo Agosti 15, shirika la habari la Kormesant.ru liliripoti: "Taliban" (harakati inayotambuliwa kama ya kigaidi na iliyopigwa marufuku katika Shirikisho la Urusi) inakusudia kuanzisha biashara ubadilishanaji na Urusi. Waziri wa Viwanda na Biashara wa Imarati ya Kiislamu ya Afghanistan, Nuriddin Azizi, alisema hayo wakati wa ziara yake ya kikazi jijini Moscow. Ujumbe wa Taliban uliwasili nchini Urusi katika kumbukumbu ya kujiondoa kwa vikosi vya Marekani. Mbali na Moscow, pia itazuru Kazan. Kulingana na Azizi, Kabul iko tayari kununua mapipa milioni 1 ya mafuta kwa kubadilishana na baadhi ya bidhaa za Afghanistan. Kwa kuongezea, kama inavyotarajiwa, tutazungumzia kuhusu usambazaji wa nafaka na mafuta ya alizeti ya Urusi".

Maoni:

Mwaka mmoja umepita tangu Waamerika waondoke Afghanistan, na Taliban kuchukua utawala nchini humo na kuchukua nafasi zao katika medani ya kimataifa. Chaguo lililofanywa na Taliban lilikuwa ni msimamo wa kufedheheshwa na kushindwa, kwani, mwishowe, Taliban waliendelea na sheria za wakoloni na mfumo wa kiulimwengu wa Kitwaghut (wakidhalimu), badala ya kutangaza mwamko wa dola ya Kiislamu ya Khilafah na kuleta nuru ya Uislamu kwa ulimwengu mzima.

Kwa kipindi cha mwaka mzima uliopita, wawakilishi wa Taliban wametembelea dola kadhaa. Ni dola zipi, kwa nafasi gani, na kwa masharti gani wanazizuru nchi hizi? Wakati Taliban walipowasili Oslo mnamo Januari iliyopita, Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Anniken Huittfeldt alisema mazungumzo "hayatajumuisha uhalalishaji au utambuzi wa Taliban." Yaani, Taliban hata hawatambuliwi kama watawala halali wa nchi huru. Takriban nchi zote za ulimwengu, Taliban wamepigwa marufuku kama "shirika la kigaidi" na hawataki kuzungumza nao kwa mizani sawa, zikiwadhalilisha hadi kiwango cha kufanywa wajinga na wahalifu.

Taliban pia walizuru majirani zao - Urusi, China, Uzbekistan, Turkmenistan. Kila moja ya nchi hizi pia imewapiga marufuku Taliban kama "shirika la kigaidi" na hawataiondoa lebo hii. Mazungumzo yote yanakuwa tu ni mahusiano ya kibiashara. Afghanistan ilikuwa na ingali kwa wakoloni ni kama tu kiambatisho cha malighafi, na muamala wa Taliban ni kama tu wafanyibiashara.

Tunaona jinsi Taliban wanavyojaribu kuwaridhisha wakoloni, wakishawishi mikataba ya biashara na vibaraka wao katika eneo hilo, hata kwa madhara ya watu wao wenyewe. Wanawaomba wakoloni warudishe pesa za nchi kutoka benki za Amerika. Vyombo vya habari vimejaa mashambulizi dhidi ya utawala wa Taliban nchini humo, vikitaka kuheshimiwa kwa "haki za binadamu" na kadhalika. Taliban wanajizoezesha tu na mfumo wa kiulimwengu ulioanzishwa na wakoloni.

Hili ni nini ikiwa sio udhalilifu na kushindwa?! Je, Mujahidina walimwaga damu zao kwenye viwanja vya vita kwa ajili ya hili?! Je, watu waliteseka na kutoa muhanga maisha, mali na ustawi wao kwa ajili ya hili!? Je, ni kwa ajili hili kwamba bendera ya Mtume Muhammad (saw) inanyanyuliwa?!

Mtume wetu kipenzi Muhammad (saw), kwa kuunda dola ya Kiislamu mjini Madina Al-Munawwara hakugeukia msaada, mwongozo, urafiki kwa dola za ulimwengu za wakati huo, kama vile Dola ya Kirumi, Byzantium na Fursi. Mtume Muhammad (saw) aliongozwa ndani ya dola pamoja na nje yake na makatazo na maamrisho ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Yeye (saw) hakungoja na wala hakutafuta uhalali wala msaada kutoka kwa mwengine yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu!

 Mtume Muhammad (saw) hakujenga mahusiano na majirani kwa ajili ya biashara au urafiki. Yeye (saw) alieleza kwa wazi msimamo wake katika jumbe zake kwa watawala wa nchi mbalimbali. Kwa ufupi nitatoa mfano wa barua moja ya Mtume (saw) kwa Heraclius, mtawala wa Dola ya Kirumi, ambapo Mtume (saw) anasema:

«بسم الله الرحمن الرحيم، من محمد بن عبد الله ورسوله، إلى هرقل عظيم الروم، سلام على من اتبع الهدى: أما بعد، فإني أدعوك بدعاية الإسلام، أسلم تسلم يؤتك الله أجرك مرتين، فإن توليت عليك إثم الأريسيِّين»

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu! Kutoka kwa Muhammad, ibn Abdillah, kwenda kwa Heraclius, kiongozi wa Roma. Amani iwe juu ya mwenye kufuata uongofu: ama baada ya salamu, hakika mimi nakulingania kwa ulinganizi wa Uislamu. Silimu utasalimika na Mwenyezi Mungu atakupa malipo maradufu, na ukikataa utabeba madhambi ya Waarisia.”

Yaani, msimamo uliochukuliwa na Mtume Muhammad (saw) katika medani ya kimataifa wakati huo, licha ya kwamba Waislamu walikuwa wachache na kivitendo ndani ya muundo wa mji mmoja, ulikuwa ni msimamo uliowekwa na Mwenyezi Mungu, nafasi ya dola yenye nguvu yenye kudai kuwa kiongozi wa ulimwengu, kwa kuwa Mtume (saw) alikuwa na yakini kabisa juu ya ahadi na msaada wa Mwenyezi Mungu! Nafasi hii, nafasi ya kiongozi wa ulimwengu yenye kupelekea kwenye nuru, ilishikiliwa na makhalifa waongofu na watawala waliofuata wa Waislamu, ilioleta ushindi na uongozi wa kiulimwengu kwa Umma mzima wa Kiislamu. Hivyo ndivyo Taliban wanapaswa kutuma mabalozi wao kwa watawala wa nchi nyengine!

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Kitabu Chake Kitukufu:

(وَكَذَلِكَ جَعَلْنَاكُمْ أُمَّةً وَسَطًا لِّتَكُونُواْ شُهَدَاء عَلَى النَّاسِ وَيَكُونَ الرَّسُولُ عَلَيْكُمْ شَهِيداً)

“Na vivyo hivyo tumekufanyeni muwe Umma wa wasitani, ili muwe mashahidi juu ya watu, na Mtume awe ni shahidi juu yenu.” [2: 143].

Mwenyezi Mungu Mtukufu ametuwajibisha kuutabikisha Uislamu katika maisha, akatukabidhi jukumu la kufikisha haki - Uislamu kwa wanadamu wote. Hii ndiyo njia ya utukufu na wokovu!

Na leo, njia pekee ya kuwaondolea Taliban udhalilifu na kushindwa ni kuuachana na mfumo wa Kitwaghut, na kuregea kwenye uamuzi wa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. Taliban kuweni Maanswari! Ipokee mara moja njia ya Hizb ut Tahrir iliyojengwa juu ya Qur'an na Sunnah, na mufanye kazi pamoja kuhuisha Dola ya Khilafah Rashida ya pili! Na kwa msaada wa Mwenyezi Mungu, tutaleta nuru ya Uislamu kwa ulimwengu mzima! Tunamuomba Mwenyezi Mungu atusaidie!

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Eldar Khamzin
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu