Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Uongozi wa Kisiasa na Kijeshi wa Pakistan Unalinda Ufisadi na Wafisadi nchini Qatar
(Imetafsiriwa)

Habari:

Baraza la mawaziri la kifederali la Pakistan mnamo tarehe 22 Agosti 2022 liliidhinisha kutiwa saini kwa makubaliano kati ya dola ya Qatar na Jeshi la Pakistan kwa ajili ya kutoa usalama kwa kipute kijacho cha Kombe la Dunia la FIFA 2022, hafla kubwa itakayofanyika nchini Qatar, ambapo zimesalia siku 90 pekee.

Idhini hiyo ya baraza la mawaziri ilikuja baada ya Makao Makuu ya Pamoja (JSHQ) ya Jeshi la Pakistan kupendekeza kutiwa saini kwa makubaliano hayo na wizara ya mambo ya nje pamoja na Kurugenzi Kuu ya Huduma Anuwai za Ujasusi (ISI) haikuonyesha pingamizi yoyote dhidi yake. Uidhinishaji kutoka kwa baraza la mawaziri umekuja kabla tu ya ziara ya Waziri Mkuu Shehbaz Sharif nchini Qatar, iliyopangwa kufanyika Agosti 23 na 24, kwa mwaliko wa Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani, Amir wa Qatar. (Chanzo)

Maoni:

Uongozi wa kisiasa na uongozi wa Jeshi la Pakistan haukuridhika na kuwatumia wanajeshi jasiri, wenye mafunzo ya hali ya juu na wenye ujuzi wa Pakistan katika matendo yao maovu. Waliwageuza kuwa jeshi la mamluki, kwa kushiriki katika Vita vya Msalaba vya Magharibi katika ulimwengu wa Kiislamu na usiokuwa wa Kiislamu, ndani ya vile vinavyoitwa vikosi vya "kulinda amani", ambavyo kwa hakika vilihifadhi maslahi ya dola kubwa za kikoloni duniani. Viongozi hawa wawili hawakuridhika hata na kuzuia vikosi vya jeshi, kwa msingi wa sera ya kuzuia jihad, kutokana na kupigana na Wahindi wanaoikalia kimabavu Kashmir.

Kwa msingi wa sera hiyo hiyo, wanazuia usaidizi wa kijeshi kwa Waislamu wa Rohingya nchini Burma (Myanmar) na Waislamu wa Uyghur wa Turkestan Mashariki, wa Jeshi la Pakistan. Uongozi huu miwili unawadhibiti vikosi vyetu, kutokana na kuzuia ukiukaji utukufu wa Al-Masjid Al-Aqsa wa majeshi vamizi ya Kiyahudi. Hawana dira, hamu au uwezo wa ushindi wowote kwa ajili ya dhamira yoyote ya Kiislamu, popote pale duniani. Viongozi hawa hawakuridhika na usaliti na kufeli kwa mara kwa mara. Waliongeza juu yake kwa kulaani Jeshi la Pakistan kwa jukumu duni la kulinda huduma za mechi za kandanda za Kombe la Dunia la FIFA, kuwalinda washindani na mashabiki wenye kujistarehesha, kuhakikisha usalama wao.

Inaweza kuonekana kwa mpokeaji wa habari kwamba kile ambacho Jeshi la Pakistan litafanya ni kitendo cha kishujaa na cha kiungwana, kama ilivyowasilishwa na viongozi hawa wawili wafisadi. Kiuhalisia, ni kuulinda ufisadi unaofanyika nchini humo, miongoni mwa wahudhuriaji. Inapuuza kile ambacho watu wa nchi mwenyeji wanakilipia, kutokana na ufisadi huo. Mubashara na moja kwa moja kupitia mtandao na satelaiti bado inasisimua, na sio ghali sana. Hata hivyo, watawala wa Qatar wameweka masharti, chini ya uenyeji, kwa aina mbalimbali za ufisadi, kuanzia kuchanganya wanaume na wanawake na majanga yanayoletwa na hilo, hadi kucheza kamari kwa mechi, pamoja na matumizi ya pombe na dawa za kulevya na maovu mengineyo.

Haishangazi kwamba Warusi wana neno deti festivalya, 'watoto wa sherehe,' baada ya ongezeko la kuzaliwa kwa watoto chotara kutokana na hafla za kimataifa za michezo, ikiwemo Olimpiki ya 1980 ya Moscow. Huu ni mfano tu wa asili ya matendo yanayotendeka. Hakika, ni ufisadi miongoni mwa matineja, vijana na kundi la makamo kuhudhuria sherehe hizo. Hili linadhihirika wazi kutokana na maandalizi ambayo nchi mwenyeji, ikiwemo Qatar, hufanya. Watawala wa Qatar wametumia zaidi ya dolari bilioni 230 za mali ya Ummah katika maandalizi, ikiwemo kujenga hoteli na kumiliki meli ambayo ni jiji linaloelea, ambayo inaweza kubeba zaidi ya uwezo wa mahoteli kadhaa. Je, wasimamizi wa hoteli hizi na meli inayoelea watakesha usiku kwa ibada?!

Uongozi wa kisiasa na kijeshi umeyadunisha na kuyachafua majeshi ya Pakistan na haiba yao, hadi kufikia kiwango hiki duni. Kwa ajili ya mapato ya fedha za kigeni, viongozi hawa wanaona ni vyema kuajiri majeshi yetu ili kulinda ufisadi na kamari, na pia kuwalinda wafisadi, ikiwemo Mpiganaji katili wa Kimsalaba wa Kimagharibi na muabudu sanamu wa Kihindi aliyejaa chuki, adui mkubwa wa Waislamu na watu wa Pakistan, na Myahudi mwenye chuki, anayeichafua nyumba ya Mitume wa Mwenyezi Mungu (as).

Wenye ikhlasi ndani ya Jeshi la Pakistan lazima wakomeshe uongozi huu, wasafishe mafisadi walioko kwenye safu zao katika uongozi wao, kupitia kumpa Nussrah yao yule atakayesimamisha Khilafah kwa Njia ya Utume, Hizb ut Tahrir. ili Waislamu wanaodhulumiwa waokolewe, ardhi zilizokaliwa kimabavu zikombolewe na ufisadi utokomezwe.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Bilal Al-Muhajir – Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu