Ijumaa, 10 Rajab 1446 | 2025/01/10
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Utaifa ni Chombo Kichafu Mikononi mwa Madhalimu!

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mnamo Septemba 16, huduma ya habari ya Wizara ya Mambo ya Kigeni ya Jamhuri ya Kyrgyz iliripoti: “Katika jengo la Wizara hiyo, upande wa Tajik ulipewa ilani ya kupinga hatua zisizo halali na za uharibifu za upande wa Tajik.

Upande wa Kyrgyz ulibaini kuwa mnamo Septemba 16, 2022, kukiuka makubaliano yote yaliyofikiwa hapo awali, upande wa Tajik, baada ya kuwavuta wanajeshi kwenye mpaka wa Kyrgyzstan kwa mapema, kwa kutumia vikosi vya jeshi, vifaa vizito vya kijeshi, walishambulia kwa khiyana mpaka na huduma za raia katika eneo kati ya mpaka wa Dola ya Kyrgyz na Tajik katika wilaya za Batken na Leilek za jimbo la Batken la Jamhuri ya Kyrgyz.

Upande wa Kyrgyz ulidai kufuata vilivyo makubaliano yote yaliyofikiwa, kusitisha mapigano na kuondoa vikosi vya kijeshi, na pia kutounda hali ambayo inaweza kusababisha kuchochea moto hali katika maeneo ya mpakani, na tena ukasisitiza kuwa matatizo yote yanayotokea mpakani yanapaswa kutatuliwa kwa njia za kisiasa na kidiplomasia pekee”.

Maoni:

Mzozo wa hivi punde kwenye mpaka kati ya Tajikistan na Kyrgyzstan ulisababisha vifo vya watu wengi. Wizara ya Afya ya Kyrgyzstan iliripoti kwamba kwa sababu ya uchokozi kutoka kwa upande wa Tajik, watu 59 walikufa na 140 walijeruhiwa. Takriban wenyeji 140,000 walihamishwa kutoka maeneo ya karibu. Kwa upande wake, Wizara ya Mambo ya Nje ya Tajik ilithibitisha 41 waliokufa. Pande zote mbili zinashutumu kila mmoja kwa uchochezi na kuingia ndani ya eneo lao.

Mzozo huo ulipamba moto na kushika kasi wakati ambapo marais wa jamhuri zote mbili walikuwa Samarkand, Uzbekistan kwa mkutano wa kilele wa SCO mnamo tarehe 16 Septemba. Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi wa dola 15. Usalama wa kimataifa ulibakia kichwani mwa ajenda ya SCO, lakini mzozo uliozuka karibu, kwenye mpaka kati ya Tajikistan na Kyrgyzstan, haukuibuliwa kwenye ajenda.

Wakati V. Putin alipokuwa akisubiri mkutano rasmi na Rais wa Kyrgyzstan S. Zhaparov, Uzbekistan na China zilitia saini makubaliano ya ushirikiano wa kibiashara wenye thamani ya dolari bilioni 15. Vilevile, China, Kyrgyzstan na Uzbekistan zilitia saini makubaliano juu ya ujenzi wa reli - Uzbekistan, Kyrgyzstan, China. Leo, bidhaa za Uzbek hupitia Kazakhstan, Urusi na Belarusi kufikia masoko ya Ulaya. Na barabara hii itakuwa njia fupi kwa Uzbekistan kwenda Ulaya na masoko ya Asia, ikipitia Urusi, ambayo ilianguka chini ya vikwazo.

Kila mtu anajua kwamba Urusi imekuwa ikijaribu kuitiisha Uzbekistan kwa muda mrefu, lakini Rais Shavkat Mirziyoev anajitenga na Kremlin. Kukataliwa kwa uanachama katika CSTO pia kunathibitisha hili. Inaonekana kwamba V. Putin alichukua kama tusi la kibinafsi matarajio ya mkutano na makubaliano yaliyotiwa saini na Rais wa Kyrgyzstan na Zhaparov. Kwa sababu hiyo, V. Putin alitoa idhini kwa mtumwa wake mtiifu, dhalimu E. Rahmon, kumfundisha S. Zhaparov somo na kumtisha Sh. Mirziyaev kwa mzozo wa kisilaha. Mzozo huu kwenye mpaka hauko mbali na mpaka wa Uzbekistan, ambao kwa hivyo unamtia shinikizo Sh. Mirziyoyev vilevile. Dhalimu E. Rahmon, naye akiwashambulia majirani zake, anatoa wito wa utaifa ili kunyanyua hisia za watu na kuungana pambizoni mwake. Kwa upande mwingine, mamlaka za Kyrgyzstan zinajitetea na kuongeza mafuta kwenye moto wa ari ya utaifa. Hatimaye, ndugu wawili, Waislamu, wanajikuta wakivutwa ndani ya mapambano ya umwagaji damu.

Hisia za kitaifa, ambazo hutumiwa kwa ustadi sana na madhalimu, kwa mara nyingine tena zimekuwa chombo kichafu cha kufikia malengo yao mikononi mwa E. Rahmon na V. Putin. Ndugu wawili, wa Tajik na Kirghiz, kimsingi ni Waislamu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Kitabu chake kitukufu: (إِنَّمَا ٱلْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ)  “Hakika Waumini ni ndugu” [49:10].

Enyi Waislamu! Utaifa, uzalendo na fikra zinazofanana nazo ni ngeni kwa Uislamu na Waislamu! Sisi sote ni kizazi cha Adam (as). Mola wetu Mlezi ni Mwenyezi Mungu! Mtume wetu ni Muhammad (saw)! Kitabu chetu ni Quran! Mtume Muhammad (saw) amesema:

«يا أيُّها الناسُ إنَّ ربَّكمْ واحِدٌ ألا لا فضلَ لِعربِيٍّ على عجَمِيٍّ ولا لِعجَمِيٍّ على عربيٍّ ولا لأحمرَ على أسْودَ ولا لأسودَ على أحمرَ إلَّا بالتَّقوَى إنَّ أكرَمكمْ عند اللهِ أتْقاكُمْ»

“Enyi watu! Hakika, Mola wenu ni mmoja. Hakuna ubora wa Muarabu kwa asiyekuwa Muarabu, wala wa asiyekuwa Muarabu kwa Muarabu, wala wa mwekundu kwa mweusi wala wa mweusi kwa mwekundu isipokuwa kwa uchamungu. Hakika mbora wenu, ni yule mchamungu wenu Zaidi.” [Ahmad].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Eldar Khamzin
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hzib ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu