Ijumaa, 10 Rajab 1446 | 2025/01/10
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Afrika Yalazwa Njaa Kikatili na Wakoloni wa Kibepari chini ya Uangalizi wa Viongozi wake Wafisidifu

(Imetafsiriwa)

Habari:

Ripoti ya maeneo yanayokabiliwa na majanga ya mashirika mawili ya kimataifa (Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) na Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) imetoa onyo la mapema kuhusu ukosefu mkubwa wa chakula na kutoa mwito wa kuchukuliwa hatua za haraka za kibinadamu ili kuokoa maisha na kuzuia njaa katika nchi zenye uhaba mkubwa wa chakula ambapo unatarajiwa kuwa mbaya zaidi kuanzia Oktoba 2022 hadi Januari 2023. Tayari katika eneo la Pembe ya Afrika, zaidi ya watu milioni 37 katika eneo hilo wanatarajiwa kufikia kiwango cha juu zaidi cha Kiwango cha Uainishaji cha Awamu ya Usalama wa Chakula (IPC3).

Maoni:

Madhara ya ukame ni makubwa hasa maeneo ya mashariki na kusini mwa Ethiopia, mashariki na kaskazini mwa Kenya, na kusini na kati ya Somalia. Hii ina maana kwamba idadi kubwa ya watu iko katika hali mbaya, na ina uwezo mdogo wa kupata mahitaji ya kiwango cha chini ya chakula na hilo hufikiwa ima kwa kukatiza pakubwa zile bidhaa msingi au kwa kile kiitwacho mikakati ya kukabiliana na mgogoro.

Kwa miongo kadhaa, eneo la pembe ya Afrika bali bara lote limekabiliwa na majanga chini ya mnyororo wa ukoloni wa Kimagharibi. Afrika imesibiwa na Mauaji ya halaiki, kuharibiwa kwa miundo mbinu, uporaji wa rasilimali, ukame na umasikini. Tawala za kibepari pamoja na mashirika ya kimataifa ya kutoa misaada yako mbali mno kuweza kufikia kwenye suluhisho la kweli juu ya majanga na maafa haya!

Sababu halisi hasa kwa nini watu wana njaa katika sehemu hii ya bara ambayo kiujumla haina mahusiano na uhaba wa mvua au mabadiliko ya tabianchi na migogoro kama inavyodaiwa na vyombo vya habari na taasisi za chakula na utafiti duniani; badala yake, inahusiana pakubwa na sera mbovu za kiuchumi za mfumo wa Kibepari pamoja na tawala mbovu na wanasiasa ambao hawajali chochote isipokuwa matakwa yao ya kilafi. Afrika ambayo inajumuisha sehemu ya pembe yake ina utajiri mkubwa wa asili yakiwemo madini, mito, ardhi kubwa yenye rutuba, lakini, rasilimali hizi zinatumiwa na mabwenyenye wa makampuni pekee wanaojinufaisha huku raia wakiishia mikono mitupu! Bara hili tajiri limenyanyaswa kinyama, na watu wake wanakufa njaa kikatili chini ya uangalizi wa viongozi wake. Hili limefafanuliwa vyema na mwandishi Torm Burgis katika kitabu chake ‘The Looting Machine’ ambapo anaeleza jinsi wingi wa malighafi unavyopelekea baadhi ya mabwenyenye wa Kiafrika, wafadhili wa Kimagharibi, maslahi maovu ya Wachina, na hata Benki ya Dunia kupora na kunyonya nchi za Afrika. 

Afrika kamwe haitoweza kujinasua kutokana na hali hii mbaya ila kwa kuyafukuza mashirika ya Kimagharibi yanayonyakua na kufukarisha ardhi kuchimba lindi la umasikini, ujinga na maradhi. Njia ya Afrika kujitoa hakuna ila waachiliwe kulima ardhi zao zenye rutuba na kula mazao yake waachane kabisa na kuchukua suluhisho za mataifa ya kigeni ambayo ndiyo yanayofukarisha nchi na watu wake. Lakini hili nalo haliwezekani isipokuwa kwa kuangalia na kutatua tatizo la utawala na kutambua uhalisia wa ukhalifa katika ardhi.

Ni muhimu kufahamu kwamba ndwele hii inayokumba pembe ya Afrika yapaswa itie chachu Afrika kufanya kazi kwa haraka pamoja na harakati ya kiulimwengu ya Hizb ut-Tahrir kusimamisha utawala wa Khilafah kwa njia ya Utume kwani pekee ndio utakaolinda Afrika na ulimwengu kwa ujumla dhidi ya majanga haya, kusitisha kabisa uingiliaji wa kikoloni katika ardhi zetu na kuhakikishia kila raia ndani yake ya anapata usalama wa chakula.

Kwa ukumbusho, ni chini ya Khilafah ya Umar Ibn Khattab pindi Madina ilipogubikwa na baa la njaa aliwaandikia barua Magavana kuwataka wapeleke chakula cha nafaka Arabuni. Ngamia waliobeba shehena ya chakula cha nafaka na mahitaji mengine yalikuja kutoka Syria, Iraq, na Misri. Milo ilipikwa katika ngazi ya Dola na watu wote waliokimbilia hifadhi Madina walilishwa kila siku kwa gharama za serikali. Kulingana na akaunti moja, watu takriban 40,000 walilishwa kila siku. Umar (ra) alikataa kula nyama au siagi wakati wa kipindi cha njaa. Tumbo lake lilikuwa likinguruma, lakini akasema:

“Ewe tumbo unaweza kunguruma upendavyo, lakini maadamu njaa inaendelea, siwezi kukuruhusu kitu chochote kitamu.”

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Shaban Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Kenya

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu