Ijumaa, 10 Rajab 1446 | 2025/01/10
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Pauni ya Sterling ya Uingereza ni Mwathiriwa wa Mfumo wa Sarafu Zisizo na Thamani ya Dhati (Fiat)

(Imetafsiriwa)

Habari:

Benki Kuu ya Uingereza imesema kwamba haitasita kupandisha viwango vya riba ili kudhibiti mfumko wa bei baada ya kuanguka kwa pauni kwa rekodi ya chini dhidi ya dolari ya Marekani. Kauli yake ilikuja baada ya Hazina kusema kwamba itachapisha mpango wa kushughulikia deni katika jitihada za kuwahakikishia upya wawekezaji.

Pauni ilianguka kwa kiwango cha chini kabisa hapo awali dhidi ya dolari ya Marekani baada ya Chansela Kwasi Karteng kuahidi kupunguza ushuru zaidi wakati wa wikendi juu ya bajeti ndogo ya Ijumaa ambapo  alitangaza punguzo kubwa la ushuru katika miaka 50. Pauni imekuwa ikiteleza huku masoko ya kimataifa yakiguswa na ongezeko kali la kukopa kwa serikali ili kuhifadhi punguzo.

Wawekazaji sasa wanatabiri kwamba viwango vya riba vitakuwa maradufu ifikapo msimu ujao wa mchipuo kwa 5.8% kutoka 2.25% ya sasa ili kudhibiti mfumko wa juu wa bei ambao unatarajiwa kuchochewa na punguzo kubwa la ushuru liliotangazwa katika bajeti ndogo ya Ijumaa.

Samuel Tombs, mwanauchumi mkuu wa Uingereza katika Macroeconomics ya Pantheon alisema ikiwa viwango vya riba kama vilivyotabiriwa, familia ya wastani inayolipa upya kiwango maalum cha mkopo wa nyumba wa miaka miwili katika nusu ya kwanza ya  mwaka ujao ingeona malipo ya kila mwezi yakiruka mpaka pauni 1490  kutoka pauni 863.

Wataalamu wanasema kuwa ongezeko katika gharama ya kukopa kwa muda mrefu kwa ajili ya msukosuko wa soko lingemaanisha gharama za wakopeshaji wa kutoa mikataba mipya ya mikopo ya nyumba ni ghali mno.

Martin Weale, profesa wa uchumi katika King’s College jijini London na mjumbe wa zamani wa Kamati ya Sera ya Fedha ya Benki Kuu ya Uingereza, ambayo hupiga kura juu ya viwango vya riba, aliiambia redio ya BBC katika kipindi cha saa kumi jioni kwamba watu wana wasiwasi kuwa serikali haina mpango wa kudhibiti bajeti ya kitaifa.

“Pauni ya Sterling imeanguka kwa sababu wafanyibiashara wa soko wamehofishwa na sera za serikali, na nafikiria walihofishwa zaidi na hali ilivyokuwa mwishoni mwa wiki kwamba hii ilikuwa ni awamu ya kwanza tu ya baadhi ya makato ya ushuru” (chanzo: BBC)

Maoni:

Mifumo ya sarafu ya zisizo na thamani ya dhati (Fiat) imo katika huruma ya mfumo wa benki ambao huamua mtiririko wa fedha kulingana na makadirio yao ya mahitaji na hatari. Katika nyakati ambapo kuna haja kubwa ya uwekezaji na mikopo, tumeona mara kwa mara mabenki yakiwa katika kipindi cha upunguzaji gharama na kupelekea kudhibitiwa kwa fedha zilizoko. Uislamu kinyume na haya hutoa mazingira thabiti yasiyo na riba ambapo hakuna kichocheo cha kuzitoa fedha kutoka katika mzunguko.

Mfumo wa utawala wa pekee ambao husisitiza dhahiri juu ya mfumo wa dhahabu ni uchumi wa Kiislamu unaotabikishwa na dola ya Kiislamu. Katika Uislamu mfumo wa madini mawili ya dhahabu na fedha hutumika. Hakuna sarafu zisizo na thamani ya dhati (Fiat) zitakazotolewa na serikali, na sarafu yoyote ya karatasi lazima iegemezwe kwa asilimia 100. Riba zote zimeharamishwa; kwa hivyo uundaji wa mikopo zaidi ya raslimali zilizopo unakatizwa.

Mfumo wa dhahabu unahakikisha uthabiti wa viwango vya ubadlilishanaji baina ya nchi, na uthabiti wa viwango vya ubadilishanaji hupelekea kustawi kwa ghafla kwa biashara ya kimataifa, kwa kuwa wafanyibiashara hawataogopa mashaka ya kuyumba-yumba kwa viwango vya ubadilishanaji.

Leo tumeshuhudia kuwa uwezo wa watu kuweka akiba umapungua kwa muda licha ya ukweli kwamba tunachuma zaidi ya hapo awali. Nguvu ya ununuzi ya pesa imepungua katika hali halisi huku thamani ya mali kijumla ikibaki kuwa ile ile, lakini kiwango cha pesa kinachohitajika kununua mali ya kushikika (ardhi, mali, bidhaa) inapanda. Kwa ujumla watu leo wanaweka akiba chache ikilinganishwa na watu katika miongo miwili tu iliyopita.

Uislamu hutia mkazo juu ya mali na hutafuta kuhifadhi mali ya watu kwa kuhakikisha kwamba sera zake hazishushi thamani ya pesa. Mfumo wa Kiislamu hauruhusu uchapishaji wa pesa utakavyo kwa sababu sarafu zake zote lazima ziegemezwe 100% kwa akiba za dhahabu na fedha. Hii ina maana kwamba thamani kwa mnunuzi wa ardhi itabaki kuwiana na thamani ya dhahabu. Hii husababisha uthabiti na imani katika thamani ya sarafu ya Dola.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Yahya Nisbet

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Uingereza

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu