Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Uoanishaji wa Waislamu nchini Denmark Unahusiana na Maadili na Imani, Sio Kazi wala Elimu

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mnamo tarehe 30 Septemba, Wizara ya Uhamiaji na Uoanishaji ya Denmark ilichapisha ripoti ya hali ya kile kinachojulikana kama kipimo cha uoanishaji. Kipimo hicho cha uoanishaji kilichapishwa mnamo 2012, na kinakusudiwa kuonyesha maendeleo katika uoanishaji wa wahamiaji wasio wa Kimagharibi ndani ya malengo kama vile kazi, elimu na lugha.

Baada ya miaka 10 na malengo haya kama kipimo cha uoanishaji, inakadiriwa kuwa uoanishaji unaimarika nchini Denmark.

Maoni:

Tukiangalia kwa makini baadhi ya shabaha za kipimo hicho, kuna takwimu na ripoti kadhaa ambazo pia zinathibitisha kuwa wahamiaji wanaimarika kwa kiasi kikubwa katika nyanja za elimu na kazi.

Kulingana na Waziri wa Uoanishaji Kaare Dybvad Bæk, hii inaonyesha kwamba kwa hivyo inafaa kuwa na sera kali ya uhamiaji.

Wiki moja baadaye, mwaka wa bunge ulifunguliwa, na Waziri Mkuu Mette Frederiksen akaitisha uchaguzi. Katika hotuba yake ya ufunguzi, alizungumzia kuhusu wasichana wahamiaji kudhibitiwa kijamii na maadili "yaliyopitwa na wakati" ya wazazi wao, ambayo anamaanisha maadili ya Kiislamu. Pia amewachafulia sura vijana wahamiaji na kudai kwamba wanazua machafuko na hofu mitaani. Hii bila shaka inakuja juu ya mjadala wa wiki kadhaa kuhusu marufuku iliyopendekezwa ya hijab katika shule za msingi, ambayo iliagizwa moja kwa moja na serikali.

Ukweli ni kwamba uoanishaji kamwe haukuwa tu kuhusiana na malengo haya kwa kuanzia.

Njia hiyo imeundwa kwa ajili ya kampeni ya uchaguzi na mapambano dhidi ya Uislamu na Waislamu kama ajenda maalum kwa vyama vyote katika mwezi ujao. Malengo ya kipimo cha uoanishaji ni kama vile ambavyo fahamu ya uoanishaji imekuweko, ulaghai na kifiniko cha sera ya uigaji ambayo imewekwa na maarufu katika pande zote kupitia kushoto na kulia. Hata kama Waislamu watasonga mbele katika masuala ya elimu na ajira, sera ya serikali ya Denmark kwa Waislamu bado inahusu kuwalazimisha Waislamu kuwa watiifu na kukubali maadili ya kisekula ya nchi hiyo. Bila kujali umeelimika kiasi gani, unaijua vizuri lugha kiasi gani, na jinsi unavyochangia kwa jamii, wewe ni tatizo usipofuata thaqafa ya kisekula. Vile vile kupiga kura na kujaribu kupata kura za Waislamu inahusiana na kitambulisho na utiifu, na hii inalazimu kuwashinikiza Waislamu kuukubali mfumo wa kisekula na utenganishaji dini na siasa.

Ushiriki wa Waislamu katika taasisi za elimu na katika soko la ajira ni kwa sifa za Waislamu wenyewe. Haipaswi kamwe kujadiliwa au kukubaliwa kama msingi kwamba Waislamu wanapaswa kutangaza shukrani au kuwa na mtazamo kwamba wana deni la mfumo ulio dhidi ya Uislamu ambao umeupiga vita Uislamu kwa miaka mingi, utiifu wa aina yoyote kama malipo.

Kuchukua misimamo ya Kiislamu na kusimama dhidi ya serikali ya Denmark kuendelea kuchafua maadili ya Kiislamu kupitia sheria na vyombo vya habari ndivyo Uislamu unavyotaka na ndio utiifu tunaopaswa kuutangaza kuwa ni kwa Mwenyezi Mungu kama Waislamu. Ndio msimamo pekee wa kuchukua, kinyume na kura zisizo na maana, kura za batili ambazo serikali ya Denmark inataka Waislamu wapige chini ya mfumo ambao kwao wakaazi wa Denmark wenyewe wanapoteza imani.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Younes Piskorczyk

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu