- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Sio Mielekeo ya ‘Heterodox’, bali ni Mfumo wa Kiuchumi wa Uislamu ndio Utakaoiokoa Uturuki
(Imetafsiriwa)
Habari:
Nureddin Nebati, Waziri wa Hazina na Fedha, ambaye alitoa hotuba ya ufunguzi katika “Mkutano wa Mabadiliko ya Kiuchumi na Mihimili Mipya” ulioandaliwa na Wizara ya Hazina na Fedha, aliwasilisha taarifa kuhusu uchumi. Waziri Nebati alifasiri uchumi kwa kutumia maneno ya kuazimwa yaliyo nje ya muktadha na alitumia taarifa hizi: “Mtazamo wa heterodox (usio wiana na viwango vya kawaida), unaowakilisha epistemological (kuondoka kutoka kwa nadharia ya kielimu) kutoka kwa fikra ya kiuchumi ya neoclassical (yenye kuzingatia mahitaji na usambazaji kama kichocheo cha uzalishaji), yanapata umuhimu zaidi kwa tabia na neuroeconomics (jinsi tabia ya kiuchumi inaweza kujenga ufahamu wa akili) ambayo yanazidi kujitokeza leo.” (29.09.2022 Mashirika)
Maoni:
Mgogoro wa kifedha wa Uturuki, ulioathiri kila mtu pamoja na kushuka kwa thamani ya lira ya Kituruki baada ya janga la maambukizi, unaendelea kuwakunja watu maradufu kwa kuongezeka siku hadi siku, kwa sababu hatua halisi bado haijachukuliwa. Maafisa wa serikali ambao wanahisi kuwa na wajibu wa kutoa taarifa kwa wananchi katika mazingira ya uchaguzi ujao kwa upande mwingine, wanajaribu kukengeusha chanzo halisi cha tatizo machoni kwa kuokoa siku juu ya mipango kama vile "Muundo wa Kiuchumi wa Kituruki". Hata hivyo, kila sentensi ya Waziri wa Hazina na Fedha inabidi itafsiriwe kwa lugha ya mazungumzo na watendaji wa serikali wazama kila wanapozungumza, wanakua mbali na wananchi wanapozungumza.
Nureddin Nebati, Waziri wa Hazina na Fedha, ambaye alidhihaki ugumu wa kifedha wa watu kwa kutoa jibu “Je, munaweza kunitazama machoni mwangu? Uchumi ni mng’aro ulio machoni” kwa swali kuhusu takwimu katika mfumo mpya wakati wa kipindi cha TV alichohudhuria mwaka jana, wakati huu ilizua mjadala kwa umma kwa sababu ya maneno ya kuazimwa aliyotumia wakati wa 'Mkutano wa Mabadiliko ya Kiuchumi'.
Waziri Nebati, ambaye alitumia kati ya maneno heterodox na orthodox katika hotuba yake yote, kwa hakika ilionyesha kwamba kile kinachoitwa 'Muundo wa Kiuchumu wa Kituruki' si chochote ila ni sura ya Kituruki ya urasilimali, kwa sababu kila elimu ina maudhui ya kimfumo na fahamu zilizotumiwa na Nebati haziko huru kutokana na mfumo wa kirasilimali. Aidha, inatosha kuangalia mfumo uliotekelezwa na sera za kiuchumi zilizotekelezwa tangu kuanzishwa kwa jamhuri hii ili kuelewa utegemezi wa Uturuki kwa mfumo wa kibepari.
Hii ndio hali ilivyo; mfumo wa kiuchumi ambao kwao fedha za nchi hutegemea dolari ya Marekani, ambapo benki za riba huwa kama injini ndani ya uchumi, ambapo kazi na mapato ya watu yananyonywa kwa njia ya kodi na ghiliba, na la muhimu zaidi, sheria zinazotumika huamuliwa kwa mujibu wa sheria za kiulimwengu za kibepari. Hili halibadilishi ukweli kwamba ni mfumo wa kirasilimali, haijalishi ni jina gani umepewa au ni nguo gani unaojaribu kuvishwa.
Kinachotofautisha kiasi Uturuki na uchumi wa mataifa mengine, ambacho Waziri Nebati anataka kuelezea kwa fahamu ya 'heterodox', ni kupunguzwa kwa makusudi kwa thamani ya lira ya Uturuki na watawala na Benki Kuu. Kwa kawaida, wajibu wa Benki Kuu duniani ni kuongeza thamani ya sarafu ya nchi kupitia riba, lakini nchini Uturuki sera kinyume na hii inafuatwa.
Kulingana na nadharia ya serikali, mahuruji yataongezeka kwa kutekelezwa kwa muundo mpya wa kiuchumi wa Uturuki, na ziada ya akaunti ya sasa itatolewa kwa kuongezeka kwa ziada ya biashara ya nje na uzalishaji wa ndani, na hivyo mfumko wa bei utapungua. Hata hivyo, tangu Septemba 2021, pindi Benki Kuu ilipopunguza kiwango cha riba, mfumko wa bei umeongezeka, na nakisi ya sasa na nakisi ya biashara ya nje inaendelea kukua na kiwango cha ubadilishaji kinaendelea kuongezeka. Ingawa Rais Erdogan anajaribu kuhalalisha sera hii juu ya nadharia ya "riba ndio sababu, mfumko wa bei ndio natija" kwa eti kupingana riba, kwa kweli, mshindi kwa mara nyengine tena ni ushawishi wa kiwango cha riba na mshindwa ni watu wa Uturuki, kwa sababu tunapoangalia viashiria vya uchumi, picha ni kinyume kabisa na kile Rais Erdogan alivyo sema. Kadhalika, katika miezi 6 ya kwanza ya 2022 wakati muundo mpya, ambao unasemekana kupambana na riba, ulitekelezwa, kiwango cha faida cha benki kimezidi 400%. Bila kutaja data nyingine nyingi hasi zinazomomonyoa kipato cha wananchi.
Hivyo basi, neno pekee linalopaswa kusemwa kuhusu uchumi ni ukweli kwamba urasilimali ndio chanzo na migogoro ni natija yake. Na suluhisho sio mielekeo heterodox ambayo ni utekelezaji mwengine ubepari, bali ni utabikishaji wa mfumo wa kiuchumi wa Uislamu ambao watu wa Uturuki wanauamini, kwa sababu, katika mfumo wa kiuchumi wa Uislamu, uwepo wa benki za riba hairuhusiwi kwa vyovyote vile, kwani aina zote za riba zimeharamishwa, na tatizo la riba limetatuliwa kwa kikamilifu. Katika mfumo wa kiuchumi wa Uislamu, mfumo wa fedha si mfumo wa fedha wa noti za benki unaosababisha mfumko wa bei, bali ni kiwango cha dhahabu kilicho na thamani halisi.
Vilevile, katika mfumo wa kiuchumi wa Uislamu, aina za mali zina mipaka, ufujaji wa mali ya umma unaofanywa na makampuni hauruhusiwi na ugavi adilifu wa mali miongoni mwa watu unachukuliwa kuwa ndio msingi. Kwa ufupi, mfumo wa kiuchumi wa Uislamu ndio mdhamini pekee wa haki na maendeleo, kama ilivyokuwa hali katika historia ya Uislamu miaka 1400. Sisi kama Waislamu, jukumu letu ni kufanya kazi pamoja ili kusimamisha dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, ambayo ndiyo mtabikishaji wa mfumo wa kiuchumi wa Uislamu pamoja na mifumo mingine ya Dini hiyo tukufu.
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Muhammed Emin Yildirim