Jumamosi, 04 Rajab 1446 | 2025/01/04
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Uingereza Yatangaza Kufilisika, Kwa Kukubali Kutawaliwa na “Watumwa” wa Miaka ya Jana
(Imetafsiriwa)

Habari:

Rishi Sunak ametoa ombi la umoja katika kukabiliana na "changamoto kubwa ya kiuchumi," baada ya kushinda kinyang'anyiro cha kuwa waziri mkuu mpya. Alishinda kinyang'anyiro cha uongozi wa Tory baada ya mpinzani wake Penny Mordaunt kushindwa kupata uungwaji mkono wa kutosha kutoka kwa wabunge. Katika hotuba yake ya kwanza, Bw Sunak alisema kuleta chama chake na kwamba Uingereza kwa pamoja itakuwa "kipaumbele chake kikuu". Bw Sunak atakuwa waziri mkuu wa kwanza wa Uingereza wa asili ya Asia na mwenye umri mdogo zaidi kwa zaidi ya miaka 200. Bw Sunak - mwenye umri wa miaka 42 mshika dini ya  Kibaniani - anatarajiwa kuchukua wadhifa huo mnamo Jumanne baada ya kuteuliwa rasmi na Mfalme. Anachukua nafasi ya Liz Truss, kufuatia kujiuzulu kwake kwa siku 45 tu katika uwaziri mkuu wake uliokumbwa na misukosuko wiki iliyopita. (BBC)

Maoni:

Yeyote anayefikiri kwamba 'Uingereza,' mama wa ukoloni na ubaguzi wa rangi, imekuwa nchi inayoheshimu ubwana wa nchi "zinazoendelea" na imeachana na ubaguzi wake wa rangi wa kuchukiza, baada ya kuanzisha himaya yake juu ya utumwa wa watu, haswa watu wa Bara Hindi, imekosea vibaya sana!

Badala yake, kinachoulazimu ufalme wa Uingereza kumkubali Muhindi kuingia katika jumba lao la klabu, ni kufilisika kwao kabisa kisiasa na kiuchumi. Kufilisika huku kulitokea baada ya Uingereza kupoteza ushawishi wake wa kikoloni katika maeneo mengi ya dunia, kuanzia Bara Hindi Dogo, kupita Mashariki ya Kati na kuishia Afrika. Kwa hiyo sababu ya kukubali kuingia kwa “watumwa” ndani ya jumba hilo inadhihirisha kiwango cha hasara kubwa iliyopatikana na jumba hilo. Hata hivyo, hasara hiyo kubwa haifidiwa kupitia kukubaliwa kwa “watumwa.”

Hebu tuchukulie rundo kubwa la hasara ambayo Ulaya, ikiwemo Uingereza, imepata kutokana na vita vya Ukraine. Uingereza haiwezi kushindana tu na Amerika, au hata kutembea katika kivuli chake. Uingereza imekuwa nchi ya pambizoni. Uzito wake sio zaidi ya nchi yoyote ya Ulaya, ya kiwango cha pili au cha tatu. Haiwezi kushawishi hali ya kimataifa, au hata ile ya kanda ya Ulaya.

Kuchaguliwa kwa Sunak, na kukubaliwa kwake na ufalme wa Uingereza kama waziri mkuu, kunaendana na mabepari wabaguzi wa rangi nchini Marekani, kumruhusu Obama "mweusi" kuingia Ikulu ya White House. Inathibitisha kwamba watawala halisi, wa nchi zote mbili za kirasilimali za kikoloni, sio wale wanaokaa kwenye viti rasmi, ima ndani ya Ikulu ya White House au House of Commons. Badala yake, ni wamiliki halisi wa makampuni, na wamiliki wa mali na manufaa yaliyoporwa kutoka kwa wakoloni na nchi zilizokandamizwa duniani. Wanasiasa, weupe, weusi na Wahindi si chochote ila waajiriwa wa kusimamia nyadhifa rasmi nchini. Huu ndio uhalisia wa mfumo wa serikali katika nchi za Magharibi.

Marekani inajaribu kutopingika katika hali ya kimataifa, kwa kufanya kazi ya kuvunja mbavu za dubu la Kirusi nchini Ukraine, Ulaya inayoganda katika baridi kali na kumzimua panda wa Kichina. Inategemea kikamilifu vibaraka wake miongoni mwa watawala katika ulimwengu wa Kiislamu, kwa ajili ya kuunyenyekesha Umma wa Kiislamu. Dola za Kimsalaba za Ulimwengu wa Kale hazina uwezo tena, au hata kuwa tayari, kukabiliana na Umma wa Kiislamu, kama Ummah utapiga hatua kusimamisha dola ya Khilafah, sasa.

Siku hizi ni fursa ya dhahabu kwa wanyofu wote katika Ummah huu, na walio kileleni mwao ni Waislamu wanyofu miongoni mwa majeshi ya Waislamu. Ni lazima watoe Nusrah yao katika kunusuru Dini yao, wakiegemea upande wa Ummah wao. Ni lazima watoe Nusrah yao kwa Hizb ut Tahrir ili kusimamisha Dola ya Khilafah. Je, watapoteza fursa hii kwa Ummah na wao wenyewe? Je, watapoteza izza ya dunia na neema ya Akhera?! Au wataichukua fursa hii ya kuilinda Dini ya Mwenyezi Mungu (swt) na kheri ya umma, ili wapate izza ya dunia, radhi za Mwenyezi Mungu (swt), na neema ya Pepo?! Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

(وَفِي ذَٰلِكَ فَلْيَتَنَافَسِ الْمُتَنَافِسُونَ)

 “Na katika hayo washindanie wenye kushindana.” [Surah Al-Mutafifeen 83:26].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Bilal Al-Muhajir – Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu