- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Uhusiano wa Kisiasa na Dhalimu?
(Imetafsiriwa)
Habari:
Msemaji wa Rais Ibrahim Kalin alitoa taarifa kuhusu ajenda kwenye matangazo ya moja kwa moja ya A Haber. Ibrahim Kalin, ambaye alisema kuwa mahusiano na utawala wa Bashar al-Assad nchini Syria yanaendelea katika kipimo cha kijasusi, alisema kuwa mahusiano ya kisiasa yanapaswa kuanza pia. (Mepa News 18.10.2022)
Maoni:
Tunashuhudia kwamba mabadiliko ya sera ya kigeni ya Uturuki yamegeuka na kuwa mchakato wa kina zaidi na usio na maana mbali na mbinu rahisi za kisiasa. Bila shaka, sababu kubwa ya kuibuka kwa suala hili ni kwamba ni sehemu ya mipango ya dola kuu ambayo ni sehemu yake. Dola ambazo zinakosa fikra msingi yao wenyewe, yaani mfumo, daima huwa sehemu ya siasa za nguvu za kimfumo. Kutenda kwa mujibu wa masharti na hatua zinazotokana na itikadi ya kisekula ya mfumo wa kibepari yote mawili hulazimisha maumbile na kudhalilisha jamii ambazo watu wake ni Waislamu. Kwa bahati mbaya, watawala katika nchi zetu, ambao wametabanni hatua na ufahamu huu kama msingi, hawajaweza kuchukua msimamo wa heshima kwa niaba yao wenyewe au kwa niaba ya watu wao.
Ukosefu wa maadili ni wimbi ambalo wale wanaokamatwa ndani yake hawawezi hata kukisia wapi, kwa njia gani, katika hali gani wataburutwa. Katika hatua tuliyofikia hivi leo, kuyumba kwa watawala katika siasa za Uturuki, haswa kutokana na vuguvugu la siasa za nje zisizo na kanuni na maadili, ni jambo la kupigiwa mfano. Hebu fikiria, kizungumzia kuendeleza mahusiano ya kisiasa na muuaji mashuhuri ambaye ana damu ya mamilioni ya Waislamu mikononi mwake, mamilioni ya Waislamu waliojeruhiwa, wakimbizi, walioteswa na kubakwa kwa sababu ya ukatili wake, ni ukosefu wa maadili na aibu.
Uturuki, ambayo haikuwa na sera yoyote zaidi ya kutekeleza mipango ya Marekani tangu kuanza kwa Mapinduzi ya Syria, haijabaki nyuma katika kufanya biashara na Marekani kafiri. Baada ya yote, uhusiano wa kisiasa na Assad leo unatuonyesha jinsi mtazamo wa marafiki na maadui umepata msingi. Bila shaka, kuyumba huku kwa sera za kigeni hakukomei Syria pekee. Kama ambavyo kila mtu ameshuhudia, uwepo wa Mayahudi, mabadiliko sawia katika mahusiano na dola kama vile Libya, Misri, Saudi Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu yanavuka mipaka ya maadili. Labda faida ndogo zinaweza kupatikana kama matokeo ya kufadhilisha udhalilifu badala ya utu. Lakini ni bora zaidi kuregea kwenye radhi za Mwenyezi Mungu azza wa jalla, zenye rutuba.
Kinachoshangaza ni kauli mbiu katika sera ya kigeni jana, wale wanaotumia njia za kutoka kama nyenzo katika siasa za ndani kama hadithi ya mafanikio. Na kutokana na hali hiyo, watawala ambao wamekuwa wakiwahadaa wananchi kwa miaka nenda rudi na kuwalazimisha wajitegemee wenyewe, wanawalazimisha wananchi wawaunge mkono tena leo kwa kusema kinyume kabisa cha maneno ya jana.
Hii inatuonyesha kwamba hakuna dola iso na kipimo, iso na maadili, iso na mfumo, inayoweza kuwa na nidhamu zenye maana na mistari mekundu, hususan katika mujtamaa ambao watu wake ni Waislamu, hakuna kipimo kisichotokana na itikadi ya Kiislamu, hukmu hiyo haiwezi kudhihirisha sera tukufu. Kugeuza maslahi kuwa sera ya dola ni kujisalimisha kwa mamlaka na kuwapa mgongo wanaodhulumiwa. Hakuna kazi ambayo haikuegemezwa juu ya hukmu ya Shariah itakayopata kheri. Hakuna jografia ambayo hukmu za Uislamu hazitabikishwi itakayopata amani. Wakati wowote ambao Khilafah haitawali, ni makafiri na madhalimu ndio wanaoendeleza makosa yao.
Tunajua kwamba maneno yetu yatagonga kuta za makasri ya watawala na kurudi yalikotoka, lakini hatutasita kusema neno la haki. Inatarajiwa kwamba mutatubu haraka iwezekanavyo, na kisha mutafanya marekebisho. Endapo uhusiano wa kisiasa utapatikana, tambueni uhusiano huu na Waislamu katika jografia ya Kiislamu. Undeni mamlaka ya kutabikisha hukmu za Uislamu. Watangazieni makafiri na madhalimu wazi kwamba wao ni maadui zenu, ili waliodhulumiwa wapate kukuaminini, na ili wakuogopeni makafiri. Mkifanya hivi, Mwenyezi Mungu atakufanyeni wenye nguvu na maadui zenu wanyenyekee. Chaguo ni lenu!
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Ahmet SAPA