Ijumaa, 10 Rajab 1446 | 2025/01/10
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Mamlaka za Kyrgyzstan Zaendelea Kuwatesa Wabebaji Dawah

(Imetafsiriwa)

Habari:

Oktoba 31, 2022 Huduma ya habari ya Kamati ya Serikali ya Usalama wa Kitaifa ya Jamhuri ya Kyrgyz kwenye ukurasa wake wa tovuti iliripoti: “Shughuli za seli ya chinichini ya Shirika la Kidini lenye itikadi kali (REO) “Hizb ut-Tahrir al-Islami” zimekandamizwa. Mnamo Oktoba 27, 2022, ndani ya muundo wa kesi ya jinai iliyoanzishwa chini ya Kifungu cha 332 sehemu ya 2 (Uzalishaji, usambazaji wa nyenzo zenye msimamo mkali) ya Kanuni ya Jinai ya Jamhuri ya Kyrgyz, wanachama 11 wachangamfu wa REO “Hizb ut-Tahrir al-Islami”.

Kutokana na upekuzi huo, kiasi kikubwa cha fasihi, vipeperushi, simu za mkononi, vyombo vya habari vya kielektroniki na ripoti za shughuli za kifedha zenye itikadi kali za seli hiyo zilikamatwa. Watu hawa waliendesha masomo ya kidini kwa utaratibu ili kukuza itikadi kali, na pia walisambaza nyenzo zenye itikadi kali kupitia mitandao ya kijamii. Wafungwa hao waliwekwa katika kizuizi cha kabla ya kesi hiyo cha Kamati ya Serikali ya Usalama wa Kitaifa ya eneo la Jalal-Abad. Hatua za uchunguzi na operesheni zinaendelea ili kubaini mafungamano yao ya ziada ya kihalifu.”

Maoni:

Mamlaka za Kyrgyzstan zinaendelea kuwatesa wabebaji dawah, wakiwatuhumu kwa shughuli za uhalifu zenye itikadi kali. Vikosi vya usalama vinatumia tuhma zisizo na msingi dhidi ya Mashababu (wanachama) wa Hizb. Wacha nikukumbusheni kwamba Hizb ut Tahrir ilipigwa marufuku kwa uamuzi wa Mahakama ya Upeo ya Jamhuri ya Kazakhstan mwezi Agosti 2003 na kujumuishwa katika orodha ya mashirika yenye itikadi kali. Tangu wakati huo, mamia ya kina ndugu na dada wamekamatwa, kufinikwa uso, na wengi wameuawa mashahidi.

Kama inavyoonekana kutoka kwa nyenzo za kesi za jinai na taarifa za vyombo vya habari, kila kitu kinachokamatwa wakati wa upekuzi katika nyumba za kina kaka na dada ni Quran, hadith na fasihi ya hizb inayotokana na Quran na Sunnah. Vitabu hivi, ikiwemo Quran na Hadith, vimeainishwa kama fasihi yenye itikadi kali kwa mapendekezo ya wataalamu wa serikali. Yaani, tuhuma za kuwa na itikadi kali kwa wabebaji dawah zinazotolewa na mamlaka zimeunganishwa tu na ukweli kwamba Mashababu wa Hizb wanawalingania Waislamu wa nchi hiyo kutii maagizo ya Qur'an na Hadith na kuyafanyia kazi maagizo hayo.

Kimaumbile, dola hii, dola ya Taghut, iliyojengwa juu ya kutenganisha dini na maisha, usekula na udhalimu, itawatesa Waislamu wanyoofu wanaume na wanawake wa nchi, wanaolingania ulinganizi wa mwamko kwa mfumo kamili wa maisha ya Kiislamu. Dola hii ya kihalifu hutumia nguvu ya kikatili dhidi ya Waislamu wasio na ulinzi wa nchi hii, wakivamia majumba yao usiku, kama wezi na wanyang'anyi. Wameshindwa kutoa badali kwa fikira za Hizb au kukanusha fikra za Hizb kwa fikra iliyo wazi na safi zaidi kwa maisha, na hivyo wanapigana dhidi ya wabebaji da’wah kwa nguvu katili za kisilaha.

Lakini mashtaka haya, mateso kutoka kwa mamlaka, kukamatwa, na kuteswa si jambo geni kwa Mashababu wa Hizb na wabebaji da’wah. Mtume Muhammad (saw) mwenyewe na Maswahaba zake watukufu walikumbwa na mitihani hiyo. Mashababu wa Hizb, mithili ya Maswahaba (ra), hufaulu majaribio haya kwa heshima katika nchi nyingi za ulimwengu, na haswa katika jela za madhalimu wa Kyrgyzstan. Licha ya kukamatwa na kuteswa, wabebaji da’wah, kwa kutaraji ahadi za Mwenyezi Mungu na rehema zake, kila wakati wanaongoza kwa uchangamfu zaidi ulinganizi wao. Hizb, nchini Kyrgyzstan pamoja na sehemu nyinginezo za dunia, imefanya kazi na inafanya kazi, licha ya matatizo yote, na inaendelea na shughuli zake za kuhuisha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu kwa mujibu wa njia ya Utume. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Kitabu chake Kitukufu:

(وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُم فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَى لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُم مِّن بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْنًا يَعْبُدُونَنِي لَا يُشْرِكُونَ بِي شَيْئًا وَمَن كَفَرَ بَعْدَ ذَلِكَ فَأُوْلَئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ)

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu.” [24:55].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Eldar Khamzin
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu