Jumamosi, 11 Rajab 1446 | 2025/01/11
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Baraza la Wazee wa Kiislamu linapaswa Kutumia Hekima na Kulingania Khilafah ili Kuwaokoa Watoto wa Ulimwengu

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mnamo tarehe 20 Novemba 2022, Baraza la Wazee wa Kiislamu (MCE) likiwakilishwa na Jaji Mohamed Abdelsalam lilitoa hotuba ya hadhara likitaka ulinzi wa watoto wa Kiislamu na watoto wa dunia nzima chini ya bendera ya dini nyingi zilizokubaliwa mwaka wa 2019. Katika mwaka huo mkutano mmoja uilifanywa jijini Abu Dhabi na Hati juu ya Udugu wa Kibinadamu ilitiwa saini na Mwadhama Ustadh Ahmed Al-Tayeb, Imamu Mkuu wa Al-Azhar na Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Kiislamu, na Mtakatifu Papa Francis huko Abu Dhabi ambao walitoa wito wa ulinzi wa watoto duniani.

Maoni yake yamekuja wakati MCE iliposhiriki katika Kongamano la Siku ya Maombi na Kuchukua Hatua kwa Watoto Duniani la 2022, lililoandaliwa kwa pamoja na Arigato International na Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregorian cha mjini Roma chini ya kaulimbiu ‘Siku ya Maombi na Kuchukua Hatua kwa Watoto Duniani 2022’.

Abdelsalam aliongeza kuwa kuna mamilioni ya watoto wanaoteseka kwa sababu ya vita vinavyoendelea, mizozo, na migogoro. “Hali hizi zimeongeza idadi ya wakimbizi, familia zilizohamishwa, na watoto wanaohama wakiacha makwao na jamii zao, ingawa hawajafanya kosa lolote.”

Maoni:

Majukwaa ya imani nyingi ni majaribio ya kiliberali ya kisekula ya kuyeyusha masuluhisho ya kweli ya Kiislamu na kuwalaza Waislamu kutokana na mfumo mpana wa kisiasa ambao unashughulikia mahitaji yote ya Waislamu, vijana kwa wazee. Majukwaa haya yanafadhiliwa vyema na serikali za Magharibi ambazo husajili madomo kaya kusema kwa niaba ya Waislamu ili kuukusanya Ummah kuzunguka pambizoni mwa kitu chochote isipokuwa Khilafah.

Ni lazima tutambue kwamba "vita" hivi na uharibifu unaozungumzwa katika mikutano hii ni matokeo ya moja kwa moja ya fikra za Kimagharibi ambayo yanapaswa kuwa na ufumbuzi. Ulafi wa kibepari, utawala wa makampuni na ufisadi wa kisiasa ndio chanzo kikuu cha ukandamizaji wa watoto duniani kote. Droni zinazo waangushia mabomu watoto wakati wanasoma katika sehemu mbalimbali za ulimwengu wa Kiislamu kamwe hazitakoma bila ya nguvu za majeshi ya Waislamu yenye kuhami Dini ya Kiislamu kivitendo.

Watoto wanaokabiliwa na njaa nchini Yemen, Syria, Afrika na Afghanistan kamwe hawatakuwa na usalama wa chakula au usalama wa kimwili bila ya mfumo uliopangiliwa unaounganisha rasilimali za Umma. Kwa dolari bilioni 200 zilizotumika katika viwanja vya Kombe la Dunia nchini Qatar kitendo cha jinai cha viongozi wetu kiko wazi, matumizi mabaya ya madaraka yatamalizwa tu na Khalifa muongofu na mambo ya Ummah katika usimamizi wa Sharia.

(إِنِ الْحُكْمُ إِلَّا لِلَّهِ أَمَرَ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا إِيَّاهُ ذَٰلِكَ الدِّينُ الْقَيِّمُ)

“Hapana hukumu ila ya Mwenyezi Mungu tu. Yeye ameamrisha msimuabudu yeyote isipo kuwa Yeye tu. Hiyo ndiyo Dini Iliyo Nyooka.” [12:40]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Imrana Mohammad
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu