Jumamosi, 11 Rajab 1446 | 2025/01/11
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Katika Ubepari Miradi Yote ni Maficho ya Rushwa na Unyonyaji kwa Watu wa Kawaida

(Imetafsiriwa)

Habari:

Hivi karibuni Shirika la Reli Tanzania (TRC) lilipendekeza nauli kwa njia za treni ya reli ya kisasa (Standard Gauge Railway) kutoka Dar es Salaam mpaka Morogoro zinazotarajiwa kuanza Februari, 2023.

Maoni:

Kwa mujibu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu nchini Tanzania (LATRA), nauli iliyopendekezwa na TRC kwa daraja la tatu itakuwa Tsh 24,794 kwa mtu mzima na Tsh 12,397 kwa watoto wenye umri kati ya miaka 4 hadi 12, ilhali kwa daraja la chini ni Tsh 29,752 kwa mtu mzima na Tsh 14,876 kwa watoto.

Kwa uhalisia, nauli hizi zinazopendekezwa ni kubwa mno ikilinganishwa na uwezo wa kiuchumi wa walio wengi ambao wanaishi chini ya mstari wa umaskini. Lakini zaidi ya hayo, wengi waliamini kwamba kuanzishwa kwa safari za treni ya kisasa (SGR) kungefanya huduma ya usafiri wa treni kuwa haraka na nafuu.

Inafahamika wazi kuwa watu wengi hawana uwezo wa kumudu bei hizo za juu ndiyo maana mwezi Mei 2022, Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu (LATRA), ilitoa mwongozo mpya wa nauli za usafiri wa mabasi kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro, ambapo nauli yaTsh 8,000 ilikuwa kwa mabasi ya kawaida, huku Tsh 11,000 kwa mabasi ya kifahari. Kwa hakika, nauli za sasa za SGR hazikuzingatia mahitaji ya watu, hali halisi ya umaskini na kutoweza kwao kulipa bei za juu, wala hazikuonesha hali ya kujali masuala ya kuhudumia watu.

Kwa upande mwingine, inapaswa kuzingatiwa kuwa suala la ununuzi wa mabehewa hayo ya treni ya umeme kwa ajili ya SGR ambayo yaliwasili Dar es Salaam Novemba 2022 lilizua tuhuma za ufisadi na ubadhirifu wa fedha za Umma. Iliripotiwa kuwa kila behewa liligharimu takribani Tsh 2.2 bilioni, lakini inaaminika kuwa bei halisi kwa kila behewa kuwa karibu Tsh milioni 800-900. Kenya ililipa sawa na Tsh milioni 980 kwa behewa kama hilo la SGR. Kwa hivyo, suala la kuwaminya na kuwatia dhiki watu wa kawaida kwa nauli ya juu haliepukiki, ili kulipa gharama na kuzalisha faida kubwa.

Huu ndio uhalisia wa mfumo wa kibepari, watu waliokabidhiwa, kuaminiwa na wenye mamlaka hawajali watu, katika kila mradi ni lazima kuwepo na rushwa na ubadhirifu, na mwisho mzigo wa kurejesha gharama ni wa watu wa kawaida wasiojiweza.

Ubepari haujali hali ya umaskini na kutomudu gharama kwa watu hata katika huduma muhimu, kwa sababu kitu pekee kinachothaminiwa ni faida peke yake.

Katika Uislamu, kila aina ya miradi ya maendeleo na miundombinu ni kwa ajili ya kutengeneza ajira, kuchochea utoaji wa bure wa huduma muhimu kwa watu au angalau kwa gharama nafuu wanazoweza kuzimudu bila kuathirika.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Said Bitomwa

Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Tanzania

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu