Jumapili, 12 Rajab 1446 | 2025/01/12
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 “Mwaka Mpya” sio sherehe bali ni maombolezi ya majanga na maafa!

(Imetafsiriwa)

Habari:

Asilimia 50 ya Wakenya wameutaja mwaka wa 2022 kuwa mbaya zaidi. Kulingana na ripoti ya hivi punde ya kampuni ya utafiti ya Infotrak, gharama ya juu ya maisha, ukosefu wa ajira na upatikanaji wa huduma za afya, yameorodheshwa kuwa ni miongoni mwa masuala yanayowatia Wakenya tumbojuto. Mkurugenzi Mtendaji wa Infotrak Angela Ambitho pia anasema ikilinganishwa na mwaka jana, utafiti sawia ulipofanywa, hakuna kilichobadilika tangu Wakenya kulalamikia matatizo haya. Asilimia 82 ya Wakenya hata hivyo wana matumaini, kwamba 2023 itakuwa bora kuliko mwaka huu.

Maoni:

Mwaka Mpya ni sherehe inayoadhimishwa kote duniani tarehe Mosi Januari, nayo ni siku ya kwanza ya mwaka katika kalenda ya Miladi. Kwenye hotuba zao za kitaifa, viongozi wa Kisekula wa Kidemokrasia hutaja mwaka mpya kama mafunzo ya kusahihisha na kupangilia vizuri zaidi yaliyokoseka mwaka unaoisha! Raia huambiwa kwamba mwaka mpya huleta fursa nyengine mpya za kuanza na kupeleka mambo vizuri pia kuja na ufumbuzi wa kufikia kwenye ndoto zote za mafanikio!

Walimwengu wote leo duniani wanakabiliwa na matatizo ya kiuchumi, kisiasa na kijamii ambayo hayajawahi kutokea. Taabu na majanga haya hayatokamani na mikasa ya kimaumbile bali kwa hakika yanafanywa kuundwa na serikali za Kibepari zenye mtazamo finyo wa kibeberu katika maisha unaolinda maslahi mahususi ya mabwenyenye huku ukidharau hadhara na rai zote unazokinzana nazo. Kwa uhalisia huu matatizo haya yataendelea kuibuka kwa sababu ya mfumo huu uliotungwa na mwanadamu hali inayofanya kimaumbile kusuhubiwa na kasoro na makosa, hii ikizingatiwa kuwa inatokamana na maumbile ya udhaifu wa mwanadamu na ubinafsi alionao. Suluhisho pekee la migogoro hii iliyoenea ni kuwa na mfumo unaotoka kwa Mwenyezi Mungu SWT yaani Uislamu na kimsingi itaugeuza ulimwengu wote kuwa maisha yenye mafanikio.

Ama hukmu ya Kiislamu katika  kusherehekea mwaka mpya katika kalenda ya kinaswara, hii ni sehemu ya hadhara ya Kimagharibi inayolazimishwa kwa Waislamu. Katika ulazimashaji huo Wamagharibi wanawalenga Waislamu waweze kukubali na kutambua  sherehe za kidini za Kinaswara na kuamini juu ya fikra ya usawa wa kiimani baina ya Ukristo na Uislamu. Mtume Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu zimshukie aliwaonya Waislamu juu ya kuiga mila za mayahudi na manaswara. Katika hadith sahihi aliyoipokea Abu Saed Al-Khudriy (ra) kwamba Mtume (saw) alisema:

لَتَتَّبِعُنَّ سَنَنَ مَنْ قَبْلَكُم شِبْرًا بشبْر، وذراعًا بذراع، حتَّى لو سَلَكُوا جُحْر ضَبٍّ لَسَلَكْتُمُوهُ؛ قلنا: يا رسول الله؛ اليهودُ والنَّصارى؟ قال النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم: فَمَن؟

“Mtafuata nyendo za wale waliokuja kabla yenu shubiri kwa shubiri, dhiraa kwa dhiraa mpaka itafika wakiingia katika shimo la kenge, na nyinyi mtaingia pia Wakasema (Maswahaba): Ee Mtume wa Mwenyezi Mungu! Je, unamaanisha Mayahudi na Manaswara?  Akasema: Hivyo nani tena wasokuwa hao?” (Bukhari na Muslim).

Katika vita vyao dhidi ya Uislamu, baadhi ya tawala dhalimu za Kisekula kama vile Urusi zimefikia kiasi cha kumtia jela Muislamu yeyote asiyesherehekea sikukuu za Kinaswara! Mnamo mwaka wa 2015 ndani ya Mahakama ya mji wa Berm Oral ya Kaunti ya Sverdlovsk, uamuzi ulipitishwa katika kesi ya toleo lililochapishwa na Muislamu kwenye mtandao kwa kichwa: "wito kwa Waislamu kutosherehekea sikukuu zisizo za Kiislamu". Mahakama ilimhukumu Elvira Sultana Khamitova kwa saa 120 za kazi ya kulazimishwa kwa kueneza kipeperushi katika mitandao ya kijamii kuhusu marufuku ya Waislamu kusherehekea sikukuu ya jadi ya Urusi ya Mwaka Mpya.

Kwa hivyo watoto wa Umma huu wanapaswa kuachana na kanuni za kibinadamu na nidhamu mbaya za kiutawala badili yake wafanye kazi ya kubadilisha hali hiyo kwa ukamilifu, kwa kusimamisha tena utawala wa Mwenyezi Mungu kwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, na kusimamisha Khilafah Rashida (Ukhalifa ulioongoka) ya pili kwa njia ya Utume ambayo watu wote watashuhudia maisha ya furaha na mafanikio.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Kenya

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu