Jumapili, 22 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Kufeli kwa Kila Mwaka kwa Mkutano wa ASEAN kwa Waislamu Kusini Mashariki mwa Asia

(Imetafsiriwa)

Habari:

Rais wa Indonesia Joko Widodo amethibitisha kwamba kuwalinda wafanyikazi wahamiaji na wahanga wa ulanguzi wa binadamu ni mojawapo ya makubaliano msingi yaliyotokana na Mkutano wa 42 wa Wakuu wa ASEAN uliomalizika hivi karibuni huko Labuan Bajo, Indonesia, Mei 2023. Rais Jokowi alisisitiza wasiwasi mkubwa wa viongozi kwa masuala yanayoathiri moja kwa moja maslahi ya watu na kuzitaka nchi za ASEAN kuchukua hatua madhubuti dhidi ya wahusika wakuu. Aidha alisema kuwa ASEAN inazungumza kwa sauti moja katika kulaani ukiukaji wa maadili ya kibinadamu, na ujumuishwaji ni kanuni kuu ya kudumisha uaminifu wa ASEAN.

Kuhusu mgogoro wa kibinadamu nchini Myanmar, Rais Jokowi alionyesha utayari wa Indonesia kushiriki katika majadiliano na washikadau wote, ikiwa ni pamoja na utawala wa kijeshi, kwa ajili ya maslahi ya kibinadamu. Hata hivyo, alifafanua kuwa ushirikiano haupaswi kueleweka vibaya kama utambuzi, na alisisitiza umuhimu wa umoja wa ASEAN ili kuzuia nguvu za nje kutokana na kuugawanya ushirika.

Eneo la tatu la makubaliano linalenga kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi ndani ya ASEAN. Rais Jokowi alitangaza mipango ya kuendeleza mfumo wa ekolojia wa magari ya umeme, akilenga kuujumuisha katika silsila ya usambazaji wa kimataifa na kuvipa kipaumbele viwanda vya chini. Zaidi ya hayo, viongozi wa ASEAN walikubali kuimarisha miamala ya fedha za ndani na kukuza muunganisho wa malipo ya kidijitali kati ya nchi wanachama, kwa kuzingatia lengo la shirika kuu la ASEAN na kujitahidi kupata ASEAN imara na huru zaidi.

Rais Jokowi alielezea kuridhishwa kwake na Mkutano wa 42 wa ASEAN uliofaulu huko Labuan Bajo. Alisisitiza hamu ya Indonesia ya kushuhudia ASEAN thabiti inayoweza kukabiliana na changamoto, kukabiliana na mabadiliko ya mienendo, na kudumisha dori yake kuu katika eneo hilo. Matarajio ya mwisho ni kuifanya ASEAN kuwa kitovu cha ukuaji na kuanzisha eneo lenye amani, utulivu na ustawi, kuangazia fungamano thabiti na umoja kati ya nchi wanachama wa ASEAN. (Chanzo: kemlu.go.id)

Maoni:

Tangu kuanzishwa kwake mwaka wa 1967, ASEAN haijaweza kufikia lengo lake la kuunda jumuiya ya haki, salama, na amani katika kanda, licha ya kufanya mikutano ya mara kwa mara na kuzalisha makubaliano mbalimbali. ASEAN inafanya vyema katika kubuni mikutano na makubaliano lakini inapungukiwa katika kuunda hali chanya katika Asia ya Kusini-Mashariki.

Kizuizi hiki kinatokana na umbile la ASEAN kama jukwaa la ushirikiano na uratibu miongoni mwa nchi wanachama, zisizo na mamlaka ya kutekeleza sera. Zaidi ya hayo, nchi wanachama kimsingi zinaendeshwa na maslahi yao ya kitaifa. Ingawa kanuni nyingi bora zimekubaliwa, mara nyingi hukiukwa na kuthibitisha kuwa changamoto kutekelezwa. Kwa mfano, ASEAN imeshindwa kushughulikia ipasavyo dhuluma na ubabe, kama unyanyasaji unaoendelea wa Waislamu walio wachache wa Rohingya.

Hata pamoja na nchi zenye Waislamu wengi kama Indonesia, Malaysia, na Brunei Darussalam ndani ya ASEAN, mataifa haya yameshindwa kukusanya hatua muhimu kutoka kwa wenzao katika kushughulikia masuala yanayoikabili jamii ya Kiislamu nchini Myanmar. Kulaani, kutoa misaada, na kuwapokea wakimbizi yamekuwa ndio kiwango cha muitiko wao.

Vile vile, viongozi wa Kiislamu katika Mashariki ya Kati wanakabiliwa na changamoto hizo hizo, kukosa uwezo wa kujitegemea kutatua matatizo ndani ya eneo lao. Badala yake, mara nyingi hutegemea ajenda za Magharibi. Hili linaweza kuhusishwa na uaminifu wao kuegemea zaidi kwenye usekula kuliko Uislamu, na kusababisha dola dhaifu na viongozi wenye fikra baridi. Maadamu haya yataendelea, umma wa Kiislamu utajitahidi kutoa mchango chanya kwa ulimwengu, licha ya kuinuliwa na Mwenyezi Mungu kama umma bora.

[كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللّهِ وَلَوْ آمَنَ أَهْلُ الْكِتَابِ لَكَانَ خَيْرًا لَّهُم مِّنْهُمُ الْمُؤْمِنُونَ وَأَكْثَرُهُمُ الْفَاسِقُونَ]

“Nyinyi mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu. Na lau kuwa Watu wa Kitabu nao wameamini ingeli kuwa bora kwao. Wapo miongoni mwao waumini, lakini wengi wao wapotovu.” [Aali-Imran 3: 110].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Abdullah Aswar

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu