- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Mfumo wa Demokrasia Umefeli Kulinda Haki za Raia kote Ulimwenguni bila kujali Dini, Kabila au Rangi zao
(Imetafsiriwa)
Habari:
Mnamo tarehe 18 Agosti 2023, Waziri Mkuu wa Muda, Anwaarul Haq Kakar, alitoa kemeo kali dhidi ya watu waliohusika katika kukandamiza na kuchoma makanisa huko Jaranwala mapema wiki hii. Hii ni huku maafisa wakuu wakiwa na mashaka juu ya ukweli wa madai ya kufuru ambayo yalisababisha vurugu hizo.
Maoni:
Mnamo Agosti 16, 2023, familia kadhaa za Kikristo zililazimika kukimbia umati wa Waislamu wenye vurugu ambao walikuwa wanataka kumwaga damu ya vijana wawili wa Kikristo. Wenyeji wengine walidai kuwa kurasa kadhaa zilizochafuliwa za Quran Tukufu zilipatikana karibu na nyumba moja katika makutano ya barabara ya Cinema huko Jaranwala, Punjab. Makanisa manne na nyumba kadhaa za Wakristo zilichomwa moto na umati wa watu wenye hasira. Kila sehemu ya jamii ililaani kufuru zote mbili, na majibu ya vurugu juu yake.
Lakini, maswali makuu ambayo yanaibuka ni: kwa nini matukio kama haya yanaibuka? Kwa nini watu wanachukua sheria mikononi mwao?
Jibu la swali hili ni kwamba watu hawana imani katika mfumo wa demokrasia. Kwa hivyo, mtu kuchukua sheria mikono mwake sio jambo la kuzuka kwa matukio ya kufuru peke yake. Badala yake, katika kila uhalifu unaofanywa katika jamii, watu hawasubiri mfumo wa Demokrasia kuchukua hatua yake kumuadhidu mhalifu. Wanajua hiyo itachukua miaka mingi. Mateso yao yanaweza yasimalizike na adhabu. Badala yake, mfumo wa Demokrasia huokoa kuachiliwa kwa mhalifu.
Mara nyingi watu wameona kwamba mahakama za chini na mahakama za juu katika mfumo wa Demokrasia zimemhukumu mtuhumiwa wa kufuru. Lakini, mara tu serikali za Magharibi zinapoingilia suala hilo, mtu huyo huyo huondolewa hatia na Mahakama ya Upeo. Mara tu anapokuwa huru, yeye hupaa juu ya upeo wa Kimagharibi.
Kufeli kwa mfumo wa Demokrasia ni dhahiri kwamba unashindwa kutoa haki kwa idadi ya walio wengi pamoja na wachache. Inafeli kwa Waislamu na wasiokuwa Waislamu. Tunashuhudia visa vya wasichana wa Kiislamu na wasiokuwa wa Kiislamu wakilazimika kufanya kazi katika nyumba za matajiri kwa sababu ya umaskini mkubwa. Wanateswa vikali na waajiri wao. Mamlaka zinashindwa kuchukua hatua na kutoa haki, isipokuwa matukio haya kwa njia fulani huwa ni vichwa vya habari au vivumishi kwenye Twitter.
Ukandamizaji kama huo hufanyika kila palipo na mfumo wa Demokrasia. Katika nchi kubwa zaidi ya Kidemokrasia ulimwenguni, India, Waislamu, Wakristo, Makalasinga, Mabaniani wa tabaka la chini wanalengwa, kuteswa, kuhamishwa kutoka majumbani mwao, na kuuawa. Katika kitovu cha Demokrasia, Magharibi, Quran Tukufu inachomwa na heshima ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) inatukanwa kwa idhini kamili ya serikali. Waislamu wanalazimika kukubali kufuru kwa sababu ni uhuru wa kujieleza. Waislamu wanalazimishwa huko Magharibi kukubali uhusiano wa kimapenzi nje ya ndoa, ushoga na ujinsia.
Imethibitishwa, bila ya shaka yoyote, kwamba mfumo wa Demokrasia umeshindwa kulinda raia, imani zao na matukufu yao, bila kujali dini, kabila na rangi.
Iwe Waislamu au wasiokuwa Waislamu, watu wanaweza tu kuishi maisha ya utulivu na heshima chini ya Dola ya Khilafah. Ndani yake uhai na mali zao, imani zao, maeneo ya ibada, na maandiko ya kidini yanalindwa kikamilifu. Hakuna mhalifu anayeweza kukimbia akiwa huru, baada ya kufanya uhalifu wa kinyama. Historia ya Khilafah ni thibitisho la madai haya. Katika karne ya 15 wakati Waislamu na Mayahudi walipopewa chaguo, na watawala wapya wa Kikristo wa Uhispania, ima kukubali Ukristo au kuondoka Uhispania, Mayahudi wengi wa Uhispania walipendelea kuhamia hadi Khilafah Uthmani, badala ya Ulaya ya Kikristo. Sultan Bayezid II alipeleka Jeshi la Khilafah ili kuwaleta Mayahudi salama katika ardhi za Dola ya Khilafah, haswa katika miji ya Thesaloniki na İzmir, huku akitangaza, "Mnaendelea kumwita Ferdinand, mtu mwenye busara, ambaye amefukarisha nchi yake mwenyewe na kutajirisha nchi yangu!"
Katika Khilafah, raia wasiokuwa Waislamu wanalindwa kikamilifu. Wanalipa ushuru mdogo sana ikilinganishwa na Muislamu. Hawaulizwi kupigana kwa ajili ya kuihami dola. Maswala yao ya kidini, kama ndoa, talaka, riziki, yanatatuliwa kulingana na dini yao. Wanashiriki katika kila nyanja ya maisha, isipokuwa kwamba hawaruhusiwi kugombea nyadhifa za utawala. Safwan Ibn Sulaim aliripoti, Mtume (saw) alisema, «أَلَا مَنْ ظَلَمَ مُعَاهِدًا أَوْ انْتَقَصَهُ أَوْ كَلَّفَهُ فَوْقَ طَاقَتِهِ أَوْ أَخَذَ مِنْهُ شَيْئًا بِغَيْرِ طِيبِ نَفْسٍ فَأَنَا حَجِيجُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ» “Jueni, yeyote anayemdhulumu Mu’ahid, au akakiuka haki zake, au akamkalifisha juu ya uwezo wake, au akachukua kutoka kwake kitu bila ya ridhaa yake, basi nitakuwa mtetezi wake Siku ya Kiyama.” [Sunan Abu Dawud]
Waislamu wa Pakistan ni lazima watambue kwamba wana jukumu la kutabikisha Uislamu, kulinda matukufu yao, na kuwalinda raia wasiokuwa Waislamu na matukufu yao. Hili linaweza tu kupatikana baada ya kusimamisha Khilafah kwa Njia ya Utume.
[يَهۡدِىۡ بِهِ اللّٰهُ مَنِ اتَّبَعَ رِضۡوٰنَهٗ سُبُلَ السَّلٰمِ وَيُخۡرِجُهُمۡ مِّنَ الظُّلُمٰتِ اِلَى النُّوۡرِ بِاِذۡنِهٖ وَيَهۡدِيۡهِمۡ اِلٰى صِرٰطٍ مُّسۡتَقِيۡمٍ]
“Mwenyezi Mungu huwaongoa wenye kufuata radhi yake katika njia za salama, na huwatoa katika giza kuwapeleka kwenye nuru kwa amri yake, na huwaongoa kwenye njia iliyo nyooka.” [Surah Al-Maidah; 5: 16]
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Mhandisi Shahzad Sheikh – Wilayah Pakistan