Jumamosi, 21 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Mafuta: Uchumi na Siasa

(Imetafsiriwa)

Habari:

Gharama ya mafuta nchini Kenya iligonga rekodi ya juu mnamo Ijumaa (Septemba 15) baada ya mdhibiti wa kawi kurekebisha bei ya pampu, na kuongeza ugumu wa kiuchumi unaowakabili mamilioni ya watu.

Tangazo la Mamlaka ya Udhibiti wa Kawi na Petroli imeleta bei ya rejareja ya lita moja ya petroli hadi zaidi ya shilingi 200 za Kenya ($ 1.36).

Wakenya tayari wanakabiliwa na mgogoro wa gharama kubwa ya maisha na ongezeko la bei ya bidhaa nyingi, mzigo wa ushuru mpya na shilingi inayoanguka.

Msururu wa maandamano ya upinzani dhidi ya serikali ya Rais William Ruto na sera zake za kiuchumi yalifanywa mwaka huu, baadhi yake yakiingia kwenye vurugu baya.

Maoni:

Kuanzia kwa mivuke ya mafuta ya kisukuku na athari kwa mazingira na ile inayoitwa "ajenda" hadi kusafisha mazingira na kuitengeneza au kuivunja serikali, mafuta yako katikati ya siasa za sasa za kilimwengu. Mikono ya ushawishi wa kikoloni kwenye nchi za ulimwengu wa tatu kupitia taasisi za wakoloni kama IMF na Benki ya Dunia ili kudhibiti uchumi wa mataifa dhaifu daima msingi wake umekuwa ni mafuta na gesi rasilimali muhimu zaidi ya karne ya 21. Utawala wa dolari leo umewekwa juu ya mafuta na gesi na hivyo kupata jina la ‘Petrodollar’. Hivi sasa kwa zaidi ya miaka 150, mafuta na gesi yamecheza dori muhimu katika kuwezesha ukuaji wa uchumi usio wa kawaida katika ule unaoitwa ulimwengu wa kwanza kwa gharama ya mataifa dhaifu.

Kenya imekuwa muathiriwa wa mwenendo huu wa ulimwengu na ililazimishwa na IMF kutoendelea na utoaji ruzuku mnamo Mei 2023 juu ya mafuta na badala yake kuongeza mapato ya ushuru. Kupata kwa ushuru kwa jumla na haswa katika mafuta kumeathiri riziki za raia kugeuka kuwa mbaya zaidi. Hili limedhoofisha zaidi sarafu ya nchi dhidi ya dolari ya Marekani inayowaathiri raia wa kawaida kula zaidi mapato yao ili kumudu mahitaji msingi.

Hivi sasa bei ya mafuta imeongezeka zaidi ya maradufu ikilinganishwa na miaka 4 iliyopita yaani, gharama ya usafirishaji imeongezeka maradufu ambayo inathiri bei ya bidhaa na huduma katika uchumi wote. Mtu yeyote aliye na akili isiyo na upendeleo hawezi kuacha kuona dosari katika mfumo na sera za kibepari. Hizo zinazoitwa ruzuku hazina maana yoyote kwani kuanzia mwanzo kupunguzwa kwa ushuru kunaweza kupunguza bei kwa kiwango kinachohitajika pasi na ruzuku.

Mfumo wa Ushuru kama ulivyoundwa na mfumo wa kibepari kama chanzo kikuu cha mapato kwa serikali unabaki kuwa ala ya ukandamizaji na ya kinyama zaidi kuwahi kutumiwa kusimamia mambo ya watu. Mafuta yanasimama kuwa bidhaa pekee rahisi na inayoweza kudhibitiwa kutozwa ushuru na kuongeza pakubwa ukusanyaji wake vilevile. Kama ilivyotajwa hapo awali ubepari ni mfumo wenye dosari ambapo dola inakopa kwa msingi wa riba kwa ajili ya miundombinu na madhumuni mengineyo ya maendeleo na kulitoza ushuru taifa kwa ajili kulipia riba wakati mwanzoni ingetoza ushuru kwa ajili ya hilo hilo.

Kwa kuongezea, mojawapo ya dosari kuu kufafanua zaidi, ni mafuta huzingatiwa kama mali ya kibinafsi, inayomilikiwa na mashirika ya kibinafsi ambayo lengo lake pekee ni kupata faida sio kuwezesha maisha ya heshima. Yakitengeza faida ya kila mwaka kwa trilioni za dolari za Marekani. Kwa kumatamisha utozaji ushuru, deni la kitaifa na ubinafsishaji wa viwanda vya mafuta kumesababisha msukosuko wa sasa wa kiuchumi wenye kulimbikiza utajiri mikononi mwa wachache.

Uchumi uliojengwa juu ya Uislamu huutazama utozaji ushuru kama ubanaji kwa nguvu haki yao ya kumiliki na kutumia mali yao kama ilivyo kuja katika hadith «لَا يَدْخُلُ الْجَنَّةَ صَاحِبُ مَكْسٍ» “Haingii Peponi mtoza ushuru.” (Ahmad). Pia imeharamisha mashirika ya kibinafsi kutokana na kumiliki mali ya umma kama maji, kawi na ardhi ya malisho ya Wanyama kama ilivyo katika hadith «الْمُسْلِمُونَ شُرَكَاءُ فِي ثَلَاثٍ: الْمَاءِ وَالْكَلَإِ وَالنَّارِ» “Waislamu ni washirika katika vitu vitatu: maji, malisho na moto”. Chini ya sera hizi Uislamu umelinda riziki za raia wote, Waislamu pamoja na madhimmi, na kuliondoa hili kwani Uislamu umeharamisha sufaha (watepetevu) kuchukua majukumu ya mambo ya watu kama ilivyo elezwa na Quran:

[وَلاَ تُؤْتُواْ السُّفَهَاء أَمْوَالَكُمُ الَّتِي جَعَلَ اللّهُ لَكُمْ قِيَاماً وَارْزُقُوهُمْ فِيهَا وَاكْسُوهُمْ وَقُولُواْ لَهُمْ قَوْلاً مَّعْرُوفًا]

“Wala msiwape wasio na akili mali yenu ambayo Mwenyezi Mungu ameyajaalia yawe ni kiamu yenu. Walisheni katika hayo na muwavike, na mseme nao maneno mazuri.” [Al-Nisaa 4:05]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Ali Omar
Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Kenya

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu