Jumanne, 22 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hakuna Udhuru kwa Majeshi ya Waislamu Leo Lazima Wataharaki au Mwenyezi Mungu (swt) Atawabadilisha
(Imetafsiriwa)

Habari:

Huku vita vya Gaza vikiingia siku yake ya 49, vikosi vya Mayahudi vilizidisha uvamizi wao kwenye maeneo mbali mbali katika Ukanda wa Gaza. Walivamia mahospitali kabla ya usitishaji vita wa muda kuanza kutekelezwa, na kuacha makumi kadhaa ya maiti na majeruhi.

Maoni:

Licha ya juhudi zote za muungano wa Mayahudi na Makruseda, vita vyao vya wazi juu ya sehemu ndogo ya Ummah wa Kiislamu, uhamasishaji wao wa vikosi vyao vyote, utumiaji wao wa teknolojia ya hali ya juu na aina mbali mbali za silaha, pamoja na zana nzito, ndege, manuari na nyambizi za nyuklia, Makafiri hawakufanikiwa kuvunja azma na uthabiti wa Waislamu wa Gaza. Hakuna shaka katika Dini yao kwani wana nyoyo za kweli za waumini. Hii ni licha ya majambazi hao wa Kiyahudi kuua wanawake na watoto wasio na ulinzi, na uharibifu wao wa majengo na nyumba, hadi kufikia kwamba hospitali, misikiti, na shule hazikusazwa, na hakuna hata mti mmoja uliobaki. Mayahudi walifanya haya yote kwa sababu hawakusubutu kukabiliana na wanaume, achilia mbali kifo, katika viwanja vilivyo wazi vya Gaza, na vifua visivyo na ulinzi, kama vile Mujahidina hufanya katika njia ya Mwenyezi Mungu (swt).

Hivyo, Mayahudi na wanalingana sambamba na maneno ya Mwenyezi Mungu (swt), Al-Aziz, Al-Alim,

[لَا يُقَاتِلُونَكُمْ جَمِيعًا إِلَّا فِي قُرًى مُحَصَّنَةٍ أَوْ مِنْ وَرَاءِ جُدُرٍ بَأْسُهُمْ بَيْنَهُمْ شَدِيدٌ تَحْسَبُهُمْ جَمِيعًا وَقُلُوبُهُمْ شَتَّى ذَلِكَ بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لَا يَعْقِلُونَ]

“Hawatapigana nanyi kwa mkusanyiko isipo kuwa katika vijiji vilivyo zatitiwa kwa ngome, au nyuma ya kuta. Wao kwa wao vita vyao ni vikali. Utawadhania kuwa wako pamoja, kumbe nyoyo zao ni mbali mbali. Hayo ni kwa kuwa wao ni watu wasio na akili.” [Surah Al-Hashr 59:14]. Ama kuhusu Waislamu wa Gaza na mujahidina wao, wanalingana sambamba na maneno ya Mwenyezi Mungu (swt),

[إِنَّ اللَّهَ اشْتَرَى مِنَ الْمُؤْمِنِينَ أَنفُسَهُمْ وَأَمْوَالَهُم بِأَنَّ لَهُمُ الْجَنَّةَ ۚ يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللَّهِ فَيَقْتُلُونَ وَيُقْتَلُونَ ۖ وَعْدًا عَلَيْهِ حَقًّا فِي التَّوْرَاةِ وَالْإِنجِيلِ وَالْقُرْآنِ ۚ وَمَنْ أَوْفَىٰ بِعَهْدِهِ مِنَ اللَّهِ ۚ فَاسْتَبْشِرُوا بِبَيْعِكُمُ الَّذِي بَايَعْتُم بِهِ ۚ وَذَلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ]

“Hakika Mwenyezi Mungu amenunua kwa Waumini nafsi zao na mali zao kwa kuwa wao watapata Pepo. Wanapigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu - wanauwa na wanauwawa. Hii ni ahadi aliyo jilazimisha kwa Haki katika Taurati na Injili na Qur'ani. Na nani atimizae ahadi kuliko Mwenyezi Mungu? Basi furahini kwa biashara yenu mliyo fanya naye. Na huko ndiko kufuzu kukubwa.” [Surah At-Tawba 9:111]

Kuna ushahidi unaovutia kuhusu vikosi vyote vya ukafiri, muungano wa Mayahudi na Makruseda, kwamba wao hawana hadhi ya kupigana na Waislamu, wala wenye uwezo wa kuwakabili. Askari wao hawajui maana ya heshima na maadili ya hali ya juu. Wanakosa itikadi ya msingi ya vita na sifa za ushujaa. Wamethibitisha kutofaulu kwao kuwashinda Waislamu, haijalishi idadi yao au vifaa ni kidogo kiasi gani. Yote hii pia ni ushahidi wenye hoja unaopaswa kushikiliwa dhidi ya majeshi ya Waislamu, yaliyofungiwa kwenye kambi zao, katika nchi mbali mbali za ulimwengu wa Kiislamu, haswa majeshi ambayo yanazingatiwa miongoni mwa majeshi yenye nguvu zaidi, makubwa na yenye ujuzi zaidi ulimwenguni, majeshi ya Pakistan, Misri na Uturuki.

Ikiwa kipote kidogo cha Waislamu leo kimepambana majeshi ya makafiri yaliyounga pamoja, vipi basi ikiwa Waislamu wote na majeshi yao wangefanya hivyo?! Hatuwezi tena kutoa udhuru kwa majeshi yetu, haijalishi wanahisi vibaya kiasi gani. Majeshi hayo sasa yako kwenye njia panda. Ima wataharaki, wakiwa wenye silaha nyepesi au nzito, katika njia ya Mwenyezi Mungu (swt), au Mwenyezi Mungu (swt) atawabadilisha na askari ambao anawapenda na wanaompenda, wanapigana katika njia ya Mwenyezi Mungu (swt), hadi watauwawe kishahidi au kuibuka washindi. Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

[وَإِنْ تَتَوَلَّوْا يَسْتَبْدِلْ قَوْمًا غَيْرَكُمْ ثُمَّ لَا يَكُونُوا أَمْثَالَكُمْ] 

“Na mkigeuka atawaleta watu wengine badala yenu, nao hawatakuwa kama nyinyi.” [Surah Muhammad 47:38]

Imedhihirika wazi kwa wanachama wote wenye ikhlasi wa vikosi vya majeshi ya Waislamu, na kwa hakika kwa Waislamu wote ulimwenguni, kwamba watawala wa Ulimwengu wa Kiislamu, wa karibu na wa mbali, waliosimama na kutazama mauaji hayo yaliyofanywa na Mayahudi, na kusimama waziwazi na upande wa adui, hawasimami sambamba na Iman ya Ummah. Imedhihirika wazi kuwa watawala hawa ni maadui wa Ummah, wanaoutawala kama vibaraka wa muungano wa Makruseda na Mayahudi, kama vizazi halisi vya Abu Rughaal.

Haitoshi kwetu kuomboleza wafu na kukemea mauaji. Pia haitoshi kwetu sisi kutoa fedha na kutuma misaada, ambayo haifikii watu wa Gaza, isipokuwa kwa idhini ya Mayahudi na wale walio waaminifu kwao! Badala yake, kila mwanachama mwenye ikhlasi wa majeshi ya Waislamu leo lazima asafishe jina lake dhidi ya ushahidi wenye hoja dhidi yake. Lazima awanusuru wanaokandamizwa nchini Palestina na mahali pengine na kuunusuru Uislamu. Majeshi lazima yakate shingo za watawala wahalifu na vibaraka, wakanyage maiti zao na waipe Nusrah Hizb ut Tahrir kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Ni Khilafah Rashidah ndiyo itakayowaongoza kunyanyua neno la Mwenyezi Mungu (swt) juu zaidi huko Gaza, Palestina yote na miji yote ya nchi za Waislamu.

Ushindi kwa Uislamu na Waislamu hautoki kwa watu. Ushindi unapeanwa na Mwenyezi Mungu (swt), haijalishi mihanga na juhudi ni kubwa kiasi gani. Ushindi ni nishani iliyopeanwa ambayo mtu yeyote mwenye busara anaweza kujivunia kuivaa katika ulimwengu huu, na akhera. Kwa hivyo, hatuwaombi isipokuwa watu wenye busara katika majeshi.

Ushindi ni suala la muda. Ushindi unangojea ruhusa kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt). Ushindi unangojea uhamasishaji wa watu safi, wenye ikhlasi ambao wanastahili kuwa washindi, kwa ajili yao na Dini yao. Ushindi unangojea utoaji wa Nusrah na wanyoofu katika majeshi kwa Da'wah ya kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume. Kwa hakika, tunajua kuwa ni tukio tukufu, baada ya kazi kubwa. Ni waheshimiwa pekee ndio wanaostahili ushindi. Hakuna mtu atakayestahiki thawabu yake, isipokuwa wale waliouza ulimwengu huu kwa maisha ya akhera. Kwa hivyo, pongezi kwa mtu yeyote atakayepata heshima hii kubwa.

Mwenyezi Mungu (swt) amesema, [وَفِي ذَلِكَ فَلْيَتَنَافَسِ الْمُتَنَافِسُونَ] “Na katika hayo washindanie wenye kushindana.” [Surah Al-Mutafifeen 83:26]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Bilal al-Muhajir – Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu