Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Bendera Yetu ni Bendera ya Mtume Muhammad (saw)!

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mnamo Disemba 4, IA 24.KG iliripoti: "Waziri wa Serikali ya Kyrgyzstan Suyunbek Kasmambetov amezungumza juu ya kubadilisha bendera ya nchi hiyo." Hebu na tutumaini kwamba wabunge wa Jogorku Kenesh watachukua hatua kwa kuzingatia matakwa ya watu. Sasa kuna majadiliano makali katika jamii juu ya kubadilisha bendera ya Kyrgyzstan," alisema. Afisa huyo anaamini kwamba Spika wa Jogorku Kenesh Nurlanbek Shakiev na Naibu Ulan Primov walianzisha mswada huo kwa nia njema na matakwa mazuri."

Rais Sadyr Zhaparov, Mwenyekiti wa GKNB Kamchybek Tashiev na mimi tulipenda wazo lililopendekezwa. Tungependa kuwa na bendera iliyosasishwa katika wakati ambapo nchi inasasishwa upya. Lakini sasa kuna majadiliano makali juu ya mada hii. Kwa kuyachunguza majadiliano ya umma, mtu anatambua kuwa bendera yetu ina nafasi yake ndani ya moyo wa watu, ni moja kwa watu. Hebu na tutumaini kwamba wabunge waliochaguliwa na watu watatenda kwa matakwa ya watu wa Kyrgyz akilini," Waziri huyo wa Serikali aliandika. Mnamo Novemba 29, Bunge la Kyrgyzstan lilipitisha katika usomaji wa kwanza mswada wa kubadilisha bendera ya serikali".

Maoni:

Mradi wa kubadilisha muonekano wa bendera ya kitaifa unajadiliwa kwa nguvu nchini Kyrgyzstan. Kwa masikitiko yetu makubwa, wale walioko madarakani wangali wanajadili sio kwa msingi wa Kiislamu na sio juu ya swali la ima kurudisha Uislamu au la. Kyrgyz, kwa kuwa ni Waislamu, wanapaswa kurudisha mjadala wao kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, kama Mwenyezi Mungu anavyoonyesha katika Quran Tukufu:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ أَطِيعُواْ اللّهَ وَأَطِيعُواْ الرَّسُولَ وَأُوْلِي الأَمْرِ مِنكُمْ فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللّهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللّهِ وَالْيَوْمِ الآخِرِ ذَلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلاً]

“Enyi mlio amini! Mt'iini Mwenyezi Mungu, na mt'iini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi. Na mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume, ikiwa mnamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Hayo ndiyo bora zaidi na ndiyo yenye mwisho mwema.” [4:59].

Kila dola ina nembo zake za kipekee, na bendera ya dola ni mojawapo ya vifungu hivyo. Dola ya Kiislamu iliundwa na Mtume wetu mpendwa Muhammad (saw) katika Madina Al-Munawwara pia ilitofautishwa na bendera yake kutoka nchi zengine zote za ulimwengu.

Nususi za Sharia zinaonyesha aina 2. Liwa'ah (bendera) – kitambaa cheupe kilichoandikwa maandishi meusi ya “LA ILLAHA ILLALLAH MUHAMMAD-UR-RASULULLAH”. Ra'yah ni bendera ya rangi nyeusi ambayo imeandikwa kwa maandishi meupe "LA ILLAHA ILLALLAH MUHAMMAD-UR-RASULULLAH" Hivi ndivyo Hadith tukufu inavyosema juu yake.

Katika Hadith Noble, Ibn Majah alipitishwa kutoka Jabir kwamba: «أَنَّ النَّبِيَّ ﷺ دَخَلَ مَكَّةَ وَلِوَاؤُهُ أَبْيَضُ» “Hakika Mtume (saw) aliingia Makkah siku ya ufunguzi na bendera yake ilikuwa nyeupe”. Imesimuliwa na Nasa'i kutoka kwa Anas kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alipomteua Usama ibn Zayd amiri wa jeshi kupigana na Warumi, alimkabidhi bendera nyeupe.

»لَأُعْطِيَنَّ الرَّايَةَ غَدًا رَجُلًا يُفْتَحُ عَلَى يَدَيْهِ يُحِبُّ اللَّهَ وَرَسُولَهُ وَيُحِبُّهُ اللَّهُ وَرَسُولُهُ«

“Kesho nitampa bendera mtu atakayefunguliwa juu ya mikono yake, anayempenda Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na Mwenyezi Mungu na Mtume Wake wanampenda.” na akamkabidhi bendera Ali. (Bukhari na Muslim).

Waislamu, leo bendera ya kitaifa ya Kyrgyzstan iliyopachikwa na wakoloni makafiri ingali ni mojawapo ya ala za kutugawanya kwa msingi wa kitaifa. Kuyagawanya maeneo ya Kiislamu na kupeperusha bendera tofauti tofauti juu yake ni mpango wa udhalilishaji na unyenyekeshaji wa wakoloni makafiri. Bendera hii ya kitaifa inadumisha mipaka na inatuzuia kuungana kwa msingi sahihi wa Kiislamu ambapo Waislamu wote ni ndugu na wanapaswa kuishi chini ya mtawala mmoja ndani ya dola moja ya Kiislamu.

Sisi ni Waislamu na bendera zetu zimeainishwa na Sharia. Hivyo basi hebu na tuharakishe kwa lile litakalotupa uhai, kutueka huru kutokana na udhalilishaji na unyenyekeshaji wa wakoloni makafiri. Tunamuomba Mwenyezi Mungu atusaidie!

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Eldar Khamzin
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu