Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Ongezeko la Watu Sio Chanzo cha Umaskini Tanzania

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mnamo tarehe 12/03/2024, wakati wa uzinduzi wa toleo la 20 la Taarifa ya Hali ya Sasa ya Uchumi wa Tanzania jijini Dar es Salaam, Benki ya Dunia ilidai kuwa eti kasi ya ongezeko la watu inasababisha kudorora ukuaji wa uchumi nchini. Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, wakati uchumi unatarajiwa kukua kwa 5.6 % hadi 6.0% mwaka 2024, Watanzania wengi bado wapo kwenye umaskini.

Maoni:

Dhana ya Ubepari kwamba ukuaji wa idadi ya watu unasababisha maendeleo duni ya kiuchumi ni matokeo ya nadharia za kiuchumi za "uhaba wa rasilimali" na "mahitaji ya binadamu yasiyo na kikomo". Mawazo hayo yalinasibishwa na idadi ya watu mwishoni mwa miaka ya 1700’s na mwanzoni mwa miaka ya 1800’s ambapo Mabepari walidai kuwa ongezeko la watu linasababisha viwango duni vya maisha.

Nadharia za Ubepari zinadai kwamba, kwa kuwa kuna kiwango maalumu cha rasilimali, ongezeko la watu hatimaye litapunguza mgawanyo wa kiasi cha rasilimali ambazo kila mtu anaweza kutumia, matokeo yake ni kusababisha uhaba mkubwa na umaskini. Kukabiliana na hili walipendekeza kuweka ‘kizuizi cha kimaadili’ (kujizuia kuwa na watoto ‘wengi’).

Kiuhalisia, Tanzania na nchi za Afrika kwa ujumla, zina rasilimali nyingi zikiwemo rasilimali watu ambazo zinaweza kabisa kuwafanya wawe na maendeleo kama si unyonyaji wa kikoloni wa mataifa ya kibepari. Kwa mfano, Tanzania inakadiriwa kuwa na mrundo wa kiwango cha dhahabu ya takribani wakia milioni 45 (tani 1,275), inachimba almasi kwa karne nyingi, mbali na madini mengine, kuna kilomita 1,424 ukanda wa pwani, hekta milioni 44 za ardhi ya kilimo na wastani wa hekta milioni 29.4 zinazofaa kilimo cha umwagiliaji, eneo la maji safi linakadiriwa kuwa kilomita za mraba 54,337, ambayo ni karibu asilimia 6.1 ya eneo lote la nchi, eneo la bahari ya kilomita za mraba 64,000, zaidi ya futi za ujazo trilioni 54 za gesi asilia nk.

Nadharia inayotokana na Malthus (ya kupunguza idadi ya watu) haina uhalisia, kwani tunachoshuhudia leo ni matumizi yasiyoisha ya rasilimali nyingi zinazosaidia idadi ya watu inayoongezeka. Wafuasi wa nadharia hii hawakuona wala kuzingatia maendeleo ya kiteknolojia ambayo yameongeza tija na kupunguza idadi ya magonjwa ya kuambukiza, na kufanya maisha kuwa yenye ufanisi. Leo mbinu za kisasa za kilimo zimepelekea uzalishaji wa chakula kuongezeka kwa kasi zaidi kuliko vile akina Malthus walivyotarajia. Ukuaji wa aina yake wa uchumi wa nchi za Asia kama China na India leo umewezeshwa sana na idadi yao kubwa ya watu.

Kwa hakika, kinachoifanya Tanzania na nchi nyingine zinazoendelea kuwa maskini, ni mfumo wa Ubepari unaotumia ukoloni kama mbinu yake isiyobadilika ya kufikia lengo lake la kinyonyaji. Sera za kinyonyaji za kikoloni kama vile soko huria, kukimbiza wataalamu nje ya nchi na uchumi wa karatasi, zimeyafanya mataifa yanayoendelea kuwa mashamba ya mataifa ya kikoloni na kuyaacha mataifa haya katika mdororo wa kiuchumi na minyororo ya kiuchumi ya nchi za Magharibi.

Ni wazi kwamba mwanadamu anahitaji mfumo wa haki na uadilifu ambao ni Uislamu, kupitia dola yake ya Khilafah itamkomboa mwanadamu kwa ukamilifu kutokana na uovu, uchumi wa kinyonyaji hadi kwenye ustawi wa kweli wa dunia na Akhera.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Said Bitomwa

Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Tanzania

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu