- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Huku Ramadhan Ikikaribia Gaza Inaendelea Kufa Njaa
(Imetafsiriwa)
Habari:
Kulingana na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, wakaazi wote wa Gaza milioni 2.3 kwa sasa wameainishwa kama wanakabiliwa na mgogoro, dharura, au viwango vya janga vya uhaba wa chakula. Picha zimesambazwa kwenye mitandao ya kijamii zikionyesha watu, haswa kaskazini mwa Gaza, wakila nyasi, magugu na malisho ya wanyama.
Picha za setilaiti zilionyesha uharibifu wa bandari nyingi za uvuvi, masoko, nyumba za kuhifadhia mazingira, na ardhi ya kilimo. Hatari ya njaa ilikuwa ikiongezeka kila siku huko Gaza kutokana na kuendelea kwa uhasama, na kuendelea kuzingirwa kwa Gaza. Takriban familia zote za Wapalestina huko Gaza zilikuwa zikiruka mlo kila siku, Action Against Hunger iliiambia TNA, na kuongeza kuwa baadhi ya familia hupita mchana na usiku bila kula. Uharibifu wa miundombinu ya uzalishaji na usambazaji wa chakula na uzuiaji wa uagizaji wa kibiashara umepunguza upatikanaji wa chakula. (New Arab, 20 Feb. 2024)
Maoni:
Kwa wito wa kusitishwa kwa mapigano na afueni kwa watu wa Gaza, mwezi wa Ramadhan uko ndani ya siku chache. Njaa na ukosefu wa chakula vyote vimetengenezwa na kuidhinishwa kimya kimya na mataifa ya G7 huku Marekani ikiongoza kwa uovu huu na kura zao za turufu za kusitisha mapigano ya kudumu.
Kwa kutokuwa na ufikiaji salama wa mazao mapya au protini, watu wa Gaza wanalazimika kuruka milo na mara nyingi kwenda siku kadhaa bila lishe sahihi na kuugua magonjwa na maradhi anuwai. Katika kambi ya wakimbizi ya Jabalia kaskazini mwa Mji wa Gaza, wenyeji "hukusanya mitishamba, mbegu za kila aina, na kuzitumia ili kuishi. Lakini, hasa, watu hawali. Mara nyingi, huenda siku kadhaa bila chakula," alisema Caitlin. Procter, mtafiti katika Taasisi ya Wahitimu ya Geneva ambaye ametumia miaka kadhaa katika eneo hilo na amekuwa akikusanya ushuhuda wa kila siku kutoka kwa watu wa Gaza tangu Oktoba 7, 2023. (Le Monde)
Watu wa Gaza ambao wengine wamekimbilia kula chakula cha mifugo kuwa mkate ambao una athari mbaya kwa mwili wa binadamu kutokana na maumivu makali ya tumbo na kuhara. Ukatili huo haukuishia hapo, umbile la Kiyahudi limepiga marufuku bidhaa hizo za chakula cha mifugo kuingia Ukanda wa Gaza. Vyakula vikuu vinazidi kuwa vigumu kupatikana na vinatumiwa vibaya vinapoangukia kwenye mikono mibaya ya wenye pupa na wafisadi. Ni Mwenyezi Mungu (swt) pekee ndiye anayewalisha kutokana na majani ya asili ya kijani kibichi ambayo yamechipuka baada ya kunyesha kwa mvua kubwa baridi katika wiki chache zilizopita.
Ramadhan ni mwezi wa saumu na ibada kwa Waislamu kama ilivyoamrishwa na Mwenyezi Mungu (swt). Hata hivyo amri ambayo imepuuzwa kwa makusudi ni kuleta nusrah (msaada wa kimada) kwa ndugu na dada wa Kiislamu wenzako kutokana na mauaji ya halaiki na njaa. Wale walio katika vyeo vya utawala, mamlaka na nguvu lazima watekeleze upande wao kujinasua na dhambi ya watawala wao vibaraka ambao sio tu wanatazama bila kuchukua hatua bali wanashirikiana na umbile halifu la Kiyahudi katika kuwalisha idadi ya watu wao vyakula, mazao mazuri na mahitaji mengine kupitia Imarati, Jordan na daraja la ardhi la Uturuki.
Wakati unakaribia kwa mwezi uliobarikiwa wa Ramadhan na tunaomba sana kwa ajili ya afueni ya haraka kwa Umma wetu huko Gaza. Tunatumai Ramadhan hii itakuwa wakati wa ukombozi unaohitajika sana kwa Ukanda wa Gaza na Palestina yote kutokana na ukaliaji kimabavu wa kihalifu na mauaji ya halaiki.
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Manal Bader