Jumamosi, 26 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Serikali ya Kazakhstan Yawashtaki Mashababu wa Hizb ut Tahrir

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mnamo tarehe 4 Novemba, shirika la habari la Zakon.kz liliripoti: “Katika mji wa Kentau, eneo la Turkestan, seli ya siri ya shirika la kidini lenye misimamo mikali la Hizb ut Tahrir ilifutwa. Kulingana na taarifa hiyo, shughuli za utafutaji-utendaji zilifanywa na kitengo cha kukabiliana na misimamo mikali za Wizara ya Mambo ya Ndani kwa usaidizi wa Kamati ya Usalama wa Kitaifa.

Kama matokeo ya hatua zilizochukuliwa, wanachama 10 wa seli waliwekwa kizuizini. Wakati wa upekuzi katika maeneo yao ya makaazi, kiasi kikubwa cha fasihi za kidini zenye msimamo mkali na uthibitisho mwengine wa kimada vilikamatwa.

Fikra ya shirika hili inalenga kupindua utaratibu wa kikatiba wa kisekula na kuanzisha kanuni za ‘sharia’ nchini. Wakati wa hatua za kiutendaji na za uchunguzi, ukweli wa propaganda ya fikra za washiriki wa kundi hilo, pamoja na kuzitusi hisia za kidini na uduni wa raia wa imani zengine zilithibitishwa. Wanachama wa seli walitumia rasilimali za mtandao kupokea na kusambaza mihadhara ya wahubiri wa kigeni wenye itikadi kali wa Hizb ut Tahrir”.

Maoni:

Kutokana na hali ya mwamko wa Waislamu wa Kazakhstan kutoka mafichoni mamlaka za nchi hiyo zimezidisha vita vyao dhidi ya wana waadilifu wa Umma wa Kiislamu wanaobeba wito wa Kiislamu licha ya dhiki na dhulma zote. Huko nyuma katika majira ya kiangazi ya mwaka huu, mamlaka iliripoti kuhusu mashababu 22 wa Hizb ut Tahrir walio kizuizini.

Kwa kuwa ni utawala wa kihalifu, ambao una damu nyingi za Waislamu wasio na hatia mikononi mwake, wenye mamlaka wanatumia uwongo na hadaa kuichafua Hizb ut Tahrir, wakiituhumu kwa majaribio ya kunyakua madaraka na kueneza mawazo ya ugaidi na misimamo mikali. Kwa upande wake, kwa tuhuma zote kutoka kwa serikali ya uhalifu, ningependa kusema yafuatayo:

Hizb ut Tahrir ni chama cha kisiasa cha Kiislamu ambacho mfumo wake ni Uislamu. Hizb ut Tahrir inafanya kazi ndani ya Ummah na pamoja nayo kuuongoza Ummah na kuurudisha kwenye Dola ya Haki ya Khilafah kwa njia ya Utume. Ili kufikia lengo lake, Hizb ut Tahrir haitumii vurugu, na inafuata njia ya Mtume Muhammad (saw) na hii ni mapambano ya kifikra na kisiasa.

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Kitabu chake kitukufu:

[وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُم فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَى لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُم مِّن بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْنًا يَعْبُدُونَنِي لَا يُشْرِكُونَ بِي شَيْئًا وَمَن كَفَرَ بَعْدَ ذَلِكَ فَأُوْلَئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ]

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu.” [Al- Nur:55]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Hizb ut Tahrir na
Khamzin Eldar
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu