Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Kuweka Matumaini Yenu Kwa Muuaji!

(Imetafsiriwa)

Habari:

Erdogan, ambaye alionekana katika fremu moja na Rais wa Syria Bashar al-Assad katika picha ya familia ya Mkutano wa Kilele wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu na Umoja wa Kiarabu uliofanyika Riyadh, alijibu maswali ya waandishi wa habari kwenye ndege iliyokuwa ikiregea kutoka ziarani. Erdogan alisema wanataka kuweka mahusiano kati ya Uturuki na Syria kwenye mstari, “Bado nina matumaini kwa Assad, Mungu akipenda, uundaji upya wa sheria kati yetu na Assad utafariji zaidi eneo hilo.” (Mashirika 14.11.2024)

Maoni:

Hakuna urafiki katika sera ya kigeni; kuna maslahi. Kwa bahati mbaya, mawazo yasiyo ya kibinadamu na ya kimaadili ya mfumo wa kibepari, kama vile kutenda kwa kufuata kanuni halisi za kisiasa, yamekuwa maslahi ya wanasiasa katika jiografia yetu. Kila mtu anajua kwamba Rais Erdogan kwa muda mrefu amekuwa akitoa wito katika ngazi mbalimbali kuregea enzi za zamani pamoja na Assad. Mawazo yasiyo ya kibinadamu na ya kimaadili ya mfumo wa kibepari, kama vile kutenda kwa mujibu wa kanuni halisi za kisiasa, kwa bahati mbaya yamekuwa ndio maslahi ya wanasiasa katika jiografia yetu.

Kwa hakika, tabia hizi zisizo na mashiko si ngeni kwa Erdogan vilevile Al-Sisi, ambaye hapo awali alimwita kiongozi wa mapinduzi, muuaji, baada ya muda akamuita, Bwana Sisi! Aliboresha mahusiano kwa kusema katika mahojiano yake moja ya mifano ya karibu zaidi ya kutofautiana huku. Vivyo hivyo, muuaji wa Waislamu zaidi ya milioni moja, mhalifu wa majeraha ya mamilioni ya Waislamu na ombi la mara kwa mara la kukutana na muuaji mfululizo Assad, ambaye amesababisha karibu Waislamu milioni 10 kuwa wakimbizi, ni udhalilifu wa chini kabisa. Kwani itakumbukwa, Erdogan, huku awali akisema kuwa ngumi za kukunjana zifunguliwe kuhusu mkutano na Assad, sasa haogopi kutoa picha katika sura ile ile ya Assad na kusema kwamba ana matumaini naye. Ikiwa watawala wetu hawaogopi kufanya uzembe kiasi hiki, kuweka matumaini yao kwa wauaji ambao wamechinja mamilioni ya Waislamu, basi ni wajibu juu yetu kuwajibu kwa lugha ya haki na kunyanyua ukweli ambao hawataki kuusikia katika nyuso zao.

[وَلاَ تَحْسَبَنَّ اللّهَ غَافِلاً عَمَّا يَعْمَلُ الظَّالِمُونَ إِنَّمَا يُؤَخِّرُهُمْ لِيَوْمٍ تَشْخَصُ فِيهِ الأَبْصَارُ]

“Wala usidhani Mwenyezi Mungu ameghafilika na wanayo yafanya madhaalimu. Hakika Yeye anawaakhirisha tu mpaka siku yatapo kodoka macho yao.” (Ibrahim: 42)

[وَلاَ تَرْكَنُواْ إِلَى الَّذِينَ ظَلَمُواْ فَتَمَسَّكُمُ النَّارُ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ اللّهِ مِنْ أَوْلِيَاء ثُمَّ لاَ تُنصَرُونَ]

“Wala msiwategemee wanao dhulumu, usije ukakuguseni Moto. Wala nyinyi hamna walinzi badala ya Mwenyezi Mungu, wala tena hamtasaidiwa.” (Hud: 113)

Kuweka matumaini kwa muuaji wa Waislamu milioni moja wanaofanya kejeli ya ugaidi kwa jina la kile kinachoitwa mwisho wa ugaidi, wazo la kuregesha sheria kati yao ni ukatili kwa maana ya sharia na kuanguka katika hisia za kisiasa. Kisiasa, Uturuki na watawala wa Syria waliounganishwa na Marekani kutoka kwenye kitovu, achilia mbali kutatua suala la kikanda, hawana hata uwezo wa kufanya mkutano ambao Marekani haitengenezi mazingira. Hii inajulikana na kila mtu. Ingawa ukweli huu unahusu pande zote mbili, kwa bahati mbaya, pia kuna uraibu huu wa udhalilishaji katika jiografia nzima ya Kiislamu. Tunataka kuuliza kama haitoshi munaona aibu kutofanya biashara na wauaji wa umma huu! Je, haitoshi munaburuzwa nyuma yao kwa mujibu wa maslahi ya kisiasa ya Marekani na makafiri wengine! Je, haitoshi kwamba mumezima matumaini na uaminifu wa ummah huu! Je, haitoshi, kutowajibika kwenu kuufanya ummah huu uonekane wa chini na usio na uwezo kwa jina la siasa halisi!

Watawala, ambao ndio janga kubwa kabisa la Ummah huu, wamejifanya maafisa kwa kuuongoza Ummah kwenye udhalilifu hapa duniani na katika dhiki kesho akhera. Ombi letu kutoka kwa Mwenyezi Mungu ni kwamba tuwaondoe watawala hawa wanaotutia taabu na tufikie furaha ya dunia na akhera kwa kumjaalia Khalifa Rashid ambaye atatabikisha ahkam anazoziridhia. Amin.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Ahmet SAPA

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu