- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Mgawanyiko wa Umma wa Kiislamu na Athari zake za Sumu
(Imetafsiriwa)
Habari:
Kuongezeka kwa kasi kwa uhasama kati ya Pakistan na Afghanistan katika wiki iliyopita kumesababisha kifo cha mwanajeshi mmoja wa vikosi vya usalama vya Pakistan na makumi ya raia nchini Afghanistan. Raundi hii ya hivi punde ya mapigano ya kuvuka mpaka inatokana na kile Pakistan ilisisitiza kuwa ni jibu lake kwa mashambulizi ya mara kwa mara ya kundi lenye silaha la Tehreek-e-Taliban Pakistan (TTP), ambalo Islamabad ilisema limepata kimbilio katika mpaka wa Afghanistan. Shambulizi la hivi punde zaidi la TTP, mnamo Disemba 21, lilisababisha vifo vya wanajeshi 16 wa Pakistan. Vyanzo vya jeshi la Pakistan viliithibitishia Al Jazeera kwamba siku ya Jumanne, Pakistan ilianzisha mashambulizi ya anga katika jimbo la Paktia nchini Afghanistan, ambalo linapakana na wilaya ya kikabila ya Pakistan ya Waziristan Kusini. Ndege za Pakistan zimeripotiwa kulenga maficho ambapo wapiganaji wa TTP walikuwa wametafuta hifadhi. Hata hivyo, serikali ya Taliban ya Afghanistan, iliyo madarakani tangu Agosti 2021, iliishutumu Pakistan kwa kuua takriban raia 46, wakiwemo wanawake na watoto, katika mashambulizi ya anga. Katika kujibu, serikali ya Afghanistan iliahidi “kulipiza kisasi”. Mnamo siku ya Jumamosi, vikosi vya Taliban vya Afghanistan vilidai kulenga “maeneo kadhaa” karibu na Mstari wa Durand, mpaka unaogombaniwa kati ya mataifa hayo mawili. (Al-Jazeera)
Maoni:
Mapigano kati ya Pakistan na Afghanistan ni matunda machungu ya mbegu iliyopandwa na ukoloni wa Magharibi. Ukoloni wa Magharibi ulisimamia kuvunjwa kwa Dola ya Kiislamu ya Khilafah mwaka 1924, zaidi ya miaka mia moja iliyopita. Baada ya kugawanya ardhi za Waislamu, kila ardhi ilipewa kitambulisho tofauti cha utaifa.
Mapigano kati ya Pakistan na Afghanistan yanafanyika wakati ambapo makafiri wanawashambulia Waislamu kutoka pande zote, na kumwaga damu za Waislamu bila huruma kila mahali. Wakoloni walichukua maagizo bandia kwa msingi wa fahamu ya utaifa. Dola za Magharibi zilieneza utaifa miongoni mwa Waislamu ili kuugawanya Umma wa Kiislamu. Utaifa unaendelea kuusukuma Ummah kuelekea kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe, mauaji na uadui baina yao. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema, «لَا تَرْجِعُوا بَعْدِي كُفَّارًا يَضْرِبُ بَعْضُكُمْ رِقَابَ بَعْضٍ» “Msikufuru baada yangu kwa kukatana shingo zenu.” (Sahih Bukhari na Muslim)
Fahamu ya utaifa inategemezwa juu ya msingi wa ubora wa rangi. Husababisha ushindani wa madaraka na unyonyaji. Inachochea ubaguzi wa kijamii na ubaguzi wa rangi. Uislamu unakataza kabisa aina zote za upendeleo kwa misingi ya kabila na rangi. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema, «لَيْسَ مِنَّا مَنْ دَعَا إِلَىٰ عَصَبِيَّةٍ» “Si miongoni mwetu anayelingania uaswabiya.” (Sunan Abu Dawud).
Kama matokeo ya ugawanyaji wa kitaifa wa dola za Magharibi, Muafghani, Mpakistan, na Mbengali wanachukuliwa kuwa tofauti kutoka kwa kila mmoja. Hata hivyo, Uislamu unawaunganisha Waislamu wote ndani ya Umma mmoja. Uislamu umewatangaza Waislamu wote kuwa ni Umma mmoja. Katika Uislamu, hakuna ubaguzi kwa misingi ya rangi, rangi, au jiografia. Amesema Allah (swt): ﴾إِنَّمَا ٱلْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ﴿ “Hakika Waumini ni ndugu.” [TSurah Al-Hujurat: 10].
Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) ameuelezea Umma wa Kiislamu kuwa ni mwili mmoja, «مَثَلُ الْمُؤْمِنِينَ فِي تَوَادِّهِمْ وَتَرَاحُمِهِمْ كَمَثَلِ الْجَسَدِ، إِذَا اشْتَكَىٰ مِنْهُ عُضْوٌ تَدَاعَىٰ لَهُ سَائِرُ الْجَسَدِ بِالسَّهَرِ وَالْحُمَّىٰ» “Mfano wa Waumini katika kupendana na kuhurumiana wao kwa wao ni kama mwili mmoja. Pindi kiungo chochote cha mwili kikiumia, mwili mzima huitikia kwa kukosa usingizi na homa.” (Sahih Bukhari na Muslim). Hakika, pindi inapodhurika sehemu yoyote ya mwili, mwili mzima huathirika. Pindi mwili wa mwanadamu unapogawanyika, viungo vyake vilivyotengana haviwezi kufanya kazi pamoja. Kitambulisho na chimbuko la nguvu ya Umma wa Kiislamu ni katika kuungana kwake chini ya dola moja.
Lau Uislamu ungefungiwa ndani ya mipaka ya kitaifa au ya kabila, usingeenea zaidi ya Al-Madinah Al-Munawwarah. Risaalah (ujumbe) wa Uislamu ni wa ulimwengu mzima na wito wake haukufungika na mipaka. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):
[هُوَ ٱلَّذِى أَرْسَلَ رَسُولَهُۥ بِٱلْهُدَىٰ وَدِينِ ٱلْحَقِّ لِيُظْهِرَهُۥ عَلَى ٱلدِّينِ كُلِّهِ]
“Yeye ndiye aliye mtuma Mtume wake kwa uwongofu na Dini ya Haki ipate kushinda dini zote.” [Surah At-Tawbah: 33].
Waislamu ni wadhaifu kwa sababu ya kukosekana kwa Dola ya Kiislamu ya Khilafah ili kuhakikisha umoja wao. Bila ya Khilafah, dola yoyote ya kikafiri inaweza kumwaga damu za Waislamu na kuwakandamiza. Ni kwa sababu ya kukosekana kwa Dola ya Kiislamu ndiyo maana Marekani leo, kama fahali mkali, inaranda randa kwa uhuru katika ardhi za Kiislamu, ikinyakua rasilimali zao na kulazimisha sheria zake. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema, «إِنَّمَا ٱلْإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِن وَرَائِهِ و يُتقى بِهِ» “Hakika Imaam (Khalifa) ni ngao ambayo Waislamu hupigana nyuma yake na kutafuta ulinzi.” (Sahih Muslim).
Ni lazima tuuchukulie Uislamu kama msingi wa mwamko. Lazima tusuluhishe tofauti kati ya pande zote kwa mujibu wa Uislamu. Ni lazima tusimamishe dola ya Kiislamu ambayo itawaunganisha Waislamu kuanzia Morocco hadi Indonesia chini ya rayah (bendera) ya Muhammad (saw) na italinda maisha, mali, na heshima ya Waislamu wote.
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Musa Muazzam – Wilayah Pakistan