- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Kutekwa Nyara na Kupotezwa kwa Lazima: Ishara ya Mfumo Uliofeli
(Imetafsiriwa)
Habari:
Kenya inashuhudia wimbi kubwa la utekaji nyara na mauaji yanayolenga watu mbalimbali. Tume ya Kitaifa ya Haki za Kibinadamu ya Kenya (KNCHR) inaelezea wasiwasi wake juu ya ongezeko la kutisha la utekaji nyara, kupotezwa kwa lazima na mauaji ya kiholela kote nchini. Mwenendo huu ni wa kuchukiza. Baadhi ya makundi ya vijana waandamanaji waliandamana katikati mwa jiji la Nairobi mnamo siku ya Jumatatu, tarehe 30 Disemba, huku makundi madogo ya watu wengine wakipanga kuketi vikao vya kulaani huku mawingu ya vitoa machozi yakitanda hewani. Waliimba kauli mbiu dhidi ya serikali, huku wengine wakiwa na mabango ya kulaani kuwekwa kizuizini kinyume cha sheria huku polisi waliokuwa wamepanda farasi wakishika doria karibu na hapo.
Maoni:
Utekaji nyara na mauaji yamekuwa jambo la kimataifa ambalo dola pamoja na magenge ya uhalifu yaliyopangwa hutumia kama chombo cha kunyamazisha mazungumzo ya kisiasa na kuondoa ushindani wa magenge. Kuhusu dola, huu ni sawa na ugaidi wa kiserikali kwamba utekaji nyara huwa njia ya kuondoa upinzani wowote wa kisiasa au tishio la kimfumo. Mfumo wa sasa ya kiliberali ambao seti yake ya maadili ni haki za binadamu, uhuru na haki ya mchakato wa sheria ya mahakama, kwa dola yoyote ya kiliberali yenye ubwana na uhalali wa serikali maadili haya lazima yazingatiwe.
Utekaji nyara unaofadhiliwa na serikali ni ishara kuu katika uhalisia wa leo kwamba mfumo huria imeporomoka kifikra na umefilisika, ambao hauwezi kukabiliana na mfumo wowote pinzani kifikra. Pamoja na wingi wa sheria za jinai zinazotolewa na mifumo ya mahakama huria na maadili yote ambayo yanaunda msingi wa mfumo huu yanaporomoka mbele ya Uislamu. Baada ya tamko la rais wa zamani wa Marekani George W. Bush kuhusu vita dhidi ya ugaidi, Uislamu ulichorwa kama mfumo wa ugaidi. Tangu wakati huo ulimwengu ulishuhudia Dola kote ulimwenguni zikitekeleza utekaji nyara bila kuchukuliwa hatua. Ugaidi wote wa kiserikali ulifanywa kwa Umma wa Kiislamu huku ulimwengu ukiendelea kujitia hamnazo juu uhalifu huu wa kinyama.
Kenya baada ya kupitishwa kwa sheria kuhusu ugaidi, Waislamu walikuwa wahanga kwa zaidi ya miaka 15 ya sheria hii ya kishenzi ambayo iliibua utekaji nyara mwingi na kupotezwa kwa lazima hadi leo bila kidokezo cha hatima yao. Hamu hii kubwa ya Serikali leo imeongezeka na kuwajumuisha wasiokuwa Waislamu jambo ambalo limepelekea wananchi kwa jumla kuamka kutoka katika usingizi huo wa muda mrefu ili kutoa kilio cha umma juu ya ongezeko la utekaji nyara nchini. Pamoja na kwamba bado ingali ni jinai ni wakati sasa kwa wananchi wa kawaida kunyanyua ufahamu wao wa hali ya kimataifa, kuwaona Waislamu kama wahanga wa mfumo wa kiliberali uliofilisika.
Uislamu ndio nguzo pekee ya matumaini na ukombozi wa kweli kutoka katika minyororo ya utumwa wa urasilimali huria, ambao kwa kukatikiwa utasimamia utu wa wanadamu, heshima, uhai, damu na mali kama lengo la kisheria (maqaasid) la utekelezaji wa Shariah ya Kiislamu. Historia ya Kiislamu imejaa mifano ya uadilifu kwa Waislamu na wasiokuwa Waislamu tangu kuanzishwa kwake Madina na Mtume Muhammad (saw) hadi kuanguka kwa Khilafah ya Kiuthmani mwaka 1924 M.
[وَمَآ أَرْسَلْنَـٰكَ إِلَّا رَحْمَةًۭ لِّلْعَـٰلَمِينَ]
“Nasi hatukukutuma ila uwe ni Rehema kwa walimwengu wote.”
[21:107]
Imeandikwa kwa ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Ali Omar Al-Beity
Mjumbe wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Kenya