Jumatatu, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/04
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Habari na Maoni

Wavamizi Wamuua mtu katika ardhi yake, damu ikilowanisha ardhi

Vipi Kuhusiana na maisha yake juu ya watawala wa Waislamu?

 Habari:

KHAN YOUNIS - GAZA: Mohammed Al-Naem alipigwa risasi na kufa mnamo Jumaapili na jeshi la Israeli, ambalo lilimshitaki kwa kutega bomu karibu na mpaka wa uzio wa mashariki ya Khan Younis yenye kuzingirwa na Mpaka wa Gaza. Familia ya Mohammed ilikanusha hili kwa kusema kwamba uwepo wake karibu na uzio ulikuwa wa amani.

Mwandishi wa habari wa eneo hilo aliyarekodi matukio hayo kwa video, iliyosambazwa kwa kiasi kikubwa kwenye mitandao ya kijamii, ambayo ilionyesha kundi la watazamaji Wapalestina wakijaribu kuuchukua mwili wa Mohmmed huku tingatinga la kijeshi la Israeli likiulekea.  “Kwa mara ya tatu walipojaribu kumuokoa, tingatinga la Israeli liliingia Gaza likiwa na kifaru. Na kwa mara ya kwanza katika miaka yote tumeona tingatinga la Israeli likiingia takribani mita 70 ndani ya Gaza” al-Najjar alielezea.

“Mtu mmoja aliweza kuubeba mwili wa Mohammed, tingatinga kwa haraka liliwaelekea na kutumia kijiko chake kuuzuia mwili wasiuchukue, huku askari wakimpiga risasi mwokozi katika mguu wake. Upigaji wa risasi uliendelea hata kufikia watu wale kushindwa kuuendea ule mwili.” Video ya mwandishi wa habari huyo imeibua mshituko duniani kote. [Chanzo: Aljazeera.net Middle East Eye February 24, 2020]

Maoni:

Tunaona na kuwasikia wanafki, wasiokuwa na huruma dhidi ya watu wao wenyewe wa Palestina ambao wamekuwa wa kisimama kivyao na kwamba Magharibi na watu wao hawalaumu au kulikemea hili mbele za umma dhidi ya vitendo hivi vya kutisha vinavyofanywa na umbile la Kiyahudi na vikosi vyake.

Moja ya mifano ni Charlie Hebdo huko Paris ambapo Rais wa Mamlaka ya Palestina, Mahmoud Abbas alishikana mikono ya rambirambi na kulaani kitendo cha kikatili ambacho kilichochewa na wachoraji na wahariri wa jarida ambapo pia tuliwaona watawala kutoka ardhi za Waislamu wakipaza sauti zao kulaani kitendo walichofanyiwa Wafaransa.

Kudhihirisha na kuonyesha wazi mapenzi na kukubalika kwa wauaji wa Waislamu pale ambapo Abbas alipochukua msimamo thabiti kwa kuunga mkono ushirikiano wa kiusalama uliopo kati ya vyombo vyake vya ulinzi na ujasusi pamoja na wavamizi na kusisitizia mbele ya umma.

Ni ipi gharama ya uhai wa kijana wa Palestina aliyeuawa na mvamizi ndani ya ardhi yake? Ukosefu wa kutenda na kuchukua hatua inatosha kuwa ndio jibu la swali hili.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Manal Bader

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 09 Agosti 2020 06:08

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu