Jumapili, 02 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/03
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Habari na Maoni

UFSB ya Tatarstan iliitikia Ombi la Putin kuhusiana na Bodi ya FSB

Habari:

Rais wa Urusi Vladimir Putin mnamo Februari 20, 2020 katika mkutano mkuu wa mwaka wa Bodi ya FSB alisema:

“Nidhamu ya kupambana na msimamo mkali lazima iwe nyepesi na ya kisasa. Ni muhimu kutegemea uungwaji mkono na imani ya mujtama. Nataraji kusikia kutoka kwenu kwa haraka mkiizuia miito yote ya kichochezi na vurugu. Mwito wowote wenye chuki dhidi ya utaifa na udini lazima uzuiliwe.”

Kwa mujibu wa Putin, “Ni lazima kufanyakazi na watu wa vizazi tofauti, ikijumuisha, hasa vijana”, “pamoja na miungano ya umma na vyombo vya habari ni dharura kutengeneza mazingira ya kupinga msimamo mkali kwa aina zake zote na madhihirisho yake, kiuwazi na ufahamu wa waziwazi hatari ya uharibifu wake kwa dola yetu, kwa maendeleo imara ya Muungano wa Urusi.”

Na siku hiyo hiyo jioni, Kitengo cha FSB cha Tatarstan kiliripoti kutiwa korokoroni kwa  watu watatu wanaodaiwa kushukiwa kuasisi kiini cha shirika la msimamo mkali lililopigwa marufuku “At-Takfir Val-Hijra”:

“Kupitia watumishi wa muundo wa jamhuri ya FSB, Wizara ya Mambo ya Ndani na Ulinzi wa Urusi umewashika kiongozi wa “mujahideen” na wanachama wawili, wakati wakifanya msako katika anwani nne zenye kutumika na wanachama wa kundi lenye msimamo mkali wa kidini,” kilisema kitengo cha habari cha UFSB cha Tatarstan.

Wizara ilisema kwamba walikamata majambia, kifaa cha kumpigia mtu shoti ya umeme na majarida yenye fikra ya msimamo mkali na vile vile vyombo vya habari vya kielectroniki kutoka kwa washukiwa hao.

Kitengo cha habari cha FSB kilisema mahabusu “walikusudia kufanya tukio zito la uhalifu.” ikiwa ni pamoja na kutaka kujipatia pesa kwa njia za uhalifu kwa ajili ya maandalizi ya kwenda Syria.

Kesi ya uhalifu katika sehemu 1 na 2 ya Kipengee 282.2 “Kupangilia shughuli za jamii yenye msimamo mkali” ya Kanuni ya Uhalifu ya Urusi.

Maoni:

FSB ya Urusi ndio wamekuwa wakiendeleza vita juu ya wanaoitwa “magaidi” na “wenye msimamo mkali,” ikijumuisha kuwafunga jela wanachama wa Hizb ut Tahrir, ambao hawana mahusiano ya matumizi ya silaha au vurugu. Silaha yao pekee ni matamshi. Moja ya tukio la karibu zaidi, mahakama za kijeshi za Urusi zilitoa hukumu ya kidhuluma kwa kumi, na kisha mwanachama mwengine wa Hizb ut Tahrir, mkaazi wa Tatarstan, kuwanyiwa uhuru kwa kifungo cha takribani miaka 11 mpaka 23. Na sasa, kwa mara nyingine Waislamu wamepatikana kwa mujibu wa FSB na kubandikizwa kuwa ni “magaidi” na “wenye msimamo mkali” ili tu “kuhalalisha umuhimu” wao na kupata medali, daraja za juu, vyeo vya juu, marupurupu, na kuripoti kwa Putin kwa “kazi nzuri.” Na kwa hawa “mujahideen,” silaha yao “hatari” kabisa ilikuwa ni kifaa cha kumpigia mtu shoti ya umeme, na kile kinachoitwa kuwa ni fasihi yenye “msimamo mkali.” Washukiwa hawa watatu “hatari zaidi” waliwekwa kizuizini na “vikosi vya muungano vya FSB, Wizara ya Mambo ya Ndani na Ulinzi wa Urusi”

Muendelezo wa kesi za kubuni za mashtaka ya ugaidi na watu wenye msimamo mkali, na kudumu kukazanisha sheria katika vipengee, na kuzidhilibu utambuzi wa umma kupitia vyombo vya habari sio chochote bali kunadhihirisha kwamba Urusi haipambani na vikosi au mashirika maalumu ya Kiislamu. Kinyume chake, ukweli ni kwamba Urusi ina historia mbaya dhidi ya Uislamu na Waislamu, na mamlaka za Urusi zinazingatia kwamba Uislamu umebakia katika miji iliyovamiwa tu kutokana na dosari zao na kuelewa kwao tofauti. Hata hivyo, wakoloni hawawezi hawawezi kuupiga marufuku rasmi Uislamu, kama walivyofanya mwanzo katika kipindi cha kaisari wa Urusi na utawala wa Sovieti. Na hii ndio sababu ya vita dhidi ya hicho kinachoitwa “ugaidi na msimamo mkali” kugeuka na kuwa kisingizio muafaka cha kupambana na kuondosha kila aina ya kiashiria chenye kuurudisha na kuuimarisha Uislamu miongo mwa watu Waislamu waliokoloniwa. Hata hivyo, katika kila kesi ya uhalifu, na kila kesi mpya ya kubandikiza, watu wanazidi kuelewa mpango wa Kremlin, na hisia za kuipinga Urusi zinazidi ndani ya maeneo ya Waislamu.

Mwenyezi Mungu Mtukufu asema:

[وَقُلْ جَاءَ الْحَقُّ وَزَهَقَ الْبَاطِلُ إِنَّ الْبَاطِلَ كَانَ زَهُوقًا]

“Na sema: Kweli imefika, na uwongo umetoweka. Hakika uwongo lazima utoweke!” [17:81].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Shaikhetdin Abdullah

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu