Jumatatu, 28 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/30
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vichwa Vya Habari 26/06/2020

Vichwa Vya Habari:

Uchumi wa Ulimwengu Utapata Pigo la Dolari Trilioni 12 Kutokana na Virusi Vya Korona, IMF imesema

Upanuzi wa Mipaka wa Kiyahudi: Mpango Mpya wa Mpaka Umewaacha Wapalestina katika Hali ya Kukata Tamaa

Ni Namna Ambavyo Pakistan na China Zinadhihiti Simulizi kuhusu Ukanda wa Kiuchumi kati ya China na Pakistan

Maelezo:

Uchumi wa Ulimwengu Utapata Pigo la Dolari Trilioni 12 Kutokana na Virusi Vya Korona, IMF imesema

Shirika la fedha duniani limesema kuwa janga la Korona Litaugharimu uchumi wa dunia dolari trilioni 12 baada ya kupunguza ukuaji wake kwa kiwango kikubwa. Uchumi ambao tayari ulikuwa katika hali mbaya kwa Uingereza na mataifa mengine yaliyo endelea mwaka 2020. IMF imesema kuwa itachukuwa takriban miaka miwili ili uzalishaji wa dunia kuregea sehemu ulipokuwa mwishoni mwaka 2019, na ikatahadharisha serikali kuwa makini juu ya kuondoa msaada wa kifedha kwa uchumi wa nchi zao ambao tayari ni dhaifu. Shirika hilo lenye makao yake Washington, limesema kuwa linatarajia uchumi wa Ulimwengu kuporomoka kwa asimia 4.9 mwaka huu ikilinganishwa na asilimia 3 katika kipindi cha kiangazi. IMF imesema, janga la Korona limeleta athari mbaya kwa shughuli za uchumi katika nusu ya mwaka 2020 kuliko ilivyo kuwa inatarajiwa na kuregea katika hali ya kawaida kutakuwa polepole kuliko ilivyo tarajiwa. Ukuaji wa uchumi duniani unatarajiwa kuongezeka kwa asilimia 5.4 mwaka 2021 ambacho ni kiwango cha chini kutoka asilimia 5.8 mwezi Aprili, lakini unatarajiwa kuporomoka ghafla mpaka 0 katika kipindi cha mzunguko wa pili wa janga la Korona mapema mwakani. "Janga la Korona limesababisha shughuli za uchumi kufungwa jambo ambalo lilisaidia kuudhibiti ugonjwa na kuokoa maisha lakini ikasababisha hali ngumu ya uchumi na watu kupoteza kazi, hii ndio hali mbaya ya kuporomoka kwa uchumi, ambayo imetokea toka pale dunia ilipokumbwa na hali mbaya zaidi miaka ya nyuma"alisema Gita Gopinath a mbaye ni mshauri wa IMF. Alisema, kupungua kwa uzalishaji mwaka 2020 kutakuwa na hali mbaya ikifikia kuporomoka, nusu ya asilimia 10 ya mwanzoni mwa miaka ya thalathini, na akasema viwango vya ubora wa maisha vitapungua kwa asilimia 95 mwaka huu kwa nchi zote. Mtazamo mpya wa uchumi wa dunia unaonyesha kuwa janga la Virusi Vya Korona limesababisha hali mbaya kwa soko la wafanyakazi duniani, huku ukiongeza kwamba kuongezeka kwa bei ya hisa ni zaidi ya bei ile ya wakati mataifa yalipokuwa katika hali mbaya kiuchumi baada ya vita.  Mataifa ya G7 na mataifa mengine yanayoendelea yamelazimika kupunguza au kuyarudisha nyuma malengo yao, kwa kile IMF imesema kuwa "janga ambalo halijawahi kutokea". Kupungua kwa uzalishaji wa kiulimwengu wa karibu asilimia 5 mwaka huu utakuwa mbaya zaidi kuliko kushukakwaa asilimia 0.1 kuliko rekodiwa mwaka wa 2009, baada ya mfumo wa benki kuharibika na kuporomoka kabisa katika msimu wa mchepuo. IMF ilishatabiri kuwa mwaka 2020 ni mwaka mbaya kwa ukuwaji wa uchumi diniani kutoka pale ulimwengu ulipopatwa na mtikikisiko wa uchumi miaka ya 1930. Uchumi wa Uingereza ulitarajiwa kupungua kwa asilimia 10.2, shirika hilo lilisema.  Mwezi wa nne kabla ya Uingereza kuwa katika hali mbaya iliyo sababishwa na katazo la kutotoka nje, IMF ilitabiri kuwa uchumi wa Uingereza utaporomoka kwa asilimia 6.5 mwaka huu.  Ufaransa na Italia zinatarajiwa kuandikisha punguo la asilimia 12.5 na 12.8 mtawalia. IMF ilisema kuwa utabiri huwo umefanywa juu ya dhana ambayo haina umakini sana na pia ulifanywa juu ya dhana ya kimsingi ya hali ya hatari iliyo sababishwa na janga la Korona: Umbali baina ya mtu mmoja na mwengine unaoendelea ndani ya nusu mwaka wa 2020,  uoga wa muda mrefu kuwa ni changamoto zinazotarajiwa zinazosababishwa na katazo la kutotoka nje na uzalishaji kupungua wakati biashara zilizo salimika na janga hili zikiongeza umakini katika suala la usalama na kuzidisha tabia za usafi. IMF ilisema pia inadhani kuwa hali za kiuchumi zilitulia tangia kipindi cha baridi na zimesalia hivyo katika kiwango hicho." Matokeo mbadala ya hali iliyo tangulia yanaweza kutokea na sio kwa sababu ya vile ambavyo janga linavyoendelea kubadilika " [Chanzo:The Guardian]

Wataalamu wa uchumi pamoja na wataalamu wa majanga wamekuwa wakitabiri athari za janga la Virusi Vya Korona kwa uchumi wa dunia na vifo vitokanavyo na janga hilo duniani.  Uongozi wa kirasilimali haumiliki tena suluhisho la matatizo ya uchumi na ya kiafya yanayotokana na  janga la Korona kote ulimwenguni. Ni Uislamu pekee ndio unaoweza wa kumuokoa mwaadamu kutokana na shimo ambalo ametumbukia ndani yake...

Upanuzi wa Mipaka wa Kiyahudi: Mpango Mpya wa Mpaka Umewaacha Wapalestina katika Hali ya Kukata Tamaa

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu yawezeka akafanya tukio la kuinyakua sehemu ya ardhi ya Palestina katika kipindi hiki.  Alisema kuwa hatua hiyo ni msukumo kwa Raisi wa Amerika na mpango wake wa Amani, utakaofungua "ukurasa uliotukuka katika historia ya Wazayuni" Wapalestina wanalipinga hili vikali na wana tishia kujiondoa katika makubaliano ya nyuma jambo ambalo linahatarisha serikali ambayo tayari ipo katika hali mbaya.  Kwao hatua hiyo inamaanisha kupoteza ardhi yao muhimu mno kwa taifa la baadaye na matumaini yaliofifia katika suala la kujikomboa.  Jamii ya kimataifa inalifatilia suala hili kwa makini mno, hii ni kwa sababu wanaona wazi kuwa ni suala linalo kwenda kinyume na sheria za kimataifa, huku ikionya kuhusu mzozo unaotokota katika kipindi hichi cha joto. Ni maandalizi yapi yanayoandaliwa ili kutekeleza moja kati ya sera muhimu mno ndani ya maeneo ya Mashariki ya Kati?  Waziri wa ulinzi Benny Gantz alisema siku ya Jumanne kwamba "dola ya Kiyahudi haitoendelea kuisubiria tena Palestina" ikiwa watakataa kufanya mazungumzo kuhusu unyakuzi wa sehemu ya Ukingo wa Magharibi kama sehemu ya kutekeleza mpango wa Raisi wa Amerika Donald Trump Mashariki ya Kati. "Hatutokubaliana na upumbavu wa Wapalestina" alisema Benny Gantz akizungumza kwa ufupi na waandishi habari katika makao makuu ya jeshi, Tel Aviv.  "Wapalestina wanakataa  kukaa katika meza ya mazungumzo na wanaendelea na "upumbavu wao." Gantz ambaye miaka ya nyuma aliyasimamia mazungumzo na Palestina, yaliopelekea suluhisho la kupatikana dola mbili, alisema serikali ya Kiyahudi, sio tu isimamie mazungumzo pekee bali pia iyaelekeze. Na kama Wapalestina wataamua kutofanya mazungumzo na dola ya Kiyahudi kuhusu upanuzi wa mipaka, "basi itatulazimu kusonga mbele bila ya wao" alisema.  Maafisa wakuu wa ulinzi wameonyesha wasiwasi wao upanuzi wa mipaka wa upande mmoja. Upanuzi wa mipaka wa Kiyahudi wa hadi asilimia 30 ni kipengele muhimu katika mpango wa amani wa utawala wa Trump uliowekwa hadharani mwezi Januari, ambao pia unalenga kuasisiwa dola ya Palestina.  Ramani za mwisho za ile ambayo asilimia 30 itahusisha, bado hawajaafikiwa baina ya Mayahudi na Amerika, lakini itakujumuisha makaazi yote ya Wayahudi eneo hilo pamoja na Bonde la Jordan. [Chanzo: BBC, Haaretz]

Wakati ulimwengu unashughulishwa na janga la Virusi Vya Korona, dola ya Kiyadi inajipanga kuiunganisha Palestina, kwa usaidizi wa Rais Trump.  Kukosekana kwa upinzani kutoka kwa watawala wa ulimwengu wa Kiislamu, kuna ashiria kuwa wanashiriki kikamilifu katika uhaini huu wa Karne!

Ni Namna Ambavyo Pakistan na China Zinadhihiti Simulizi kuhusu Ukanda wa Kiuchumi kati ya China na Pakistan

Ukanda wa kiuchumi kati ya  China na Pakistani )CPEC) uwekeza wa China wa miaka 15 wa dolari bilioni 62 nchini Pakistan pamoja na miradi mikubwa ya kimkakati  'Belt and Road', imechukua miongo-mitano ya hadi kuundwa kwa muungano huo wa kimkakati baina ya nchi mbili hizi katika mawanda ya kiuchumi mwaka 2015. CPEC  inaonekana kama kiungo muhimu sana cha kiuchumi katika uhusiano kati ya Pakistan na China. wakati huo huo maelezo ya mpango huo — vipengele vya uwekezaji huo na mikopo, upana wa miradi, na jumla ya gharama zote za  Pakistan — imebaki kuwa ni siri nzito, serikali ya China na Pakistan kwa pamoja zimekubaliana kuisimamia na kuendesha simulizi zote kuhusu CPEC, kuuondoa kwa ukali ukosoaji.  Zhao Lijian, makamu mkuu wa zamani wa misheni ya China (DCM) jijini,  Islamabadndiye aliyekuwa mhusika mkuu katika udhibiti wa habari wa China kuhusu CPEC,  inajibu mashambulizi ya kuipinga katika mitandao ya kijamii kutoka katika kituo kilichopo katika ubalozi wa China. Mafanikio yake katika eneo hilo yalipelekea kupandishwa cheo na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Kigeni, na kwa hivi sasa ndio nyota wa mchezo nchini China katika kile kinachojulikana kama “mabwa mwitu shujaa wa  kidiplimosia” katika janga la Virusi  vya Korona. Nchini Pakistan, serikali yaWaziri mkuu Imran Khan  ili fikiria kurejelewa upya kwa CPEC, kitu kilichonekena kinakaribiana na serikali iliyopita, wakati ilipoingia madarakani mwaka 2018. ilionekana kwa haraka ikijivuta nyuma kutoka kati makucha ya China na jeshi la Pakistan, pamoja na mkuu wa majeshi wafanyakazi walirasimisha kauli ya  kutaka kuitembelea Beijing: “BRI na CPEC inatarajiwa kufanikiwa bila kujali changamoto zote na jeshi la Pakistan linapaswa kuhakikisha usalama CPEC kwagharama yoyote.” Idara ya Taifa ya Amerika imezungumza katika miezi ya hivi karibuni katika kile wanachoiona kinachoisukuma China kukita mizizi nchini Pakistan. Idara hiyo inasema kwamba vipengele vya mpango huo unanufaisha makampuni ya China na wafanyakazi na hauna maslahi yoyote kwa Pakistan, utapelekea ongezeko la mzigo wa madeni. China na  Pakistan zote zimepuuzia upingaji huo nguvu ya Pakistan kurudi nyuma inaanza kuonekana kwa kuanza kwake kuimarisha uhusiano na Amerika tangu mchakato wa amani wa Afghani, na utegemezi kwa shirika la fedha la kimataifa. Mwisho, kuendelea kuficha kuhusu CPEC kunakofanywa na nchi zote China na Pakistan na ukosefu wa uwazi katika vipengele vya mkataba kunaepusha uwajibikaji. itainufaisha Pakistan kuruhusu  baadhi ya   uwazi kuhusu CPEC jambo ambalo likingesukuma pande zote kuelekea katika usawa wa kimkataba na hilo lingenufaisha Pakistan.

Kushindwa kwa Pakistan kuipa China msaada wa wazi kwenye mapaka wa Ladakh, kunaibua wasiwasi mpya juu ya kujifunga kwa Khan na CPEC. CPEC haiwezi kufanya kazi bila ya Pakistan na China kuungana na kuisaida Kashmir jambo ambalo litasadia pakubwa CPEC.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu