Jumapili, 27 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/29
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vichwa Vya Habari 22/07/2020

Vichwa Vya Habari:

Matajiri wa Dunia Watofautiana kuhusu Kurefushwa kwa Afueni ya Madeni kwa Nchi Masikini

Amerika Yaagiza Kufungwa kwa Ubalozi wa China jijini Houston

Chama cha Assad cha Baath Chashinda Viti Vingi katika Uchaguzi wa Ubunge

Maelezo:

Matajiri wa Dunia Watofautiana kuhusu Kupanuliwa kwa Afueni ya Madeni kwa Nchi Masikini

Mawaziri wa fedha na magavana wa Benki kuu wa G-20 wamesitisha uamuzi wa kurefusha mradi wa kuziondolea madeni nchi masikini 73 mbeleni ya mwaka 2020 hadi itakapoamuliwa vinginevyo katika mkutano wao mnamo Oktoba 2020. Kutokana na janga la virusi vya Korona, nchi 42 zimeomba kuakhirishwa katika malipo ya dola bilioni 5.3 yanayo daiwa na wanachama 22 wa Kilabu cha Paris, lakini hadi kufikia mwisho wa Juni ni dola bilioni 1.3 pekee zinazodaiwa na nchi 18 pekee ndizo zilizopitishwa.  G-20 inatarajia ripoti juu ya mahitaji ya kipesa ya nchi masikini zaidi kabla ya mkutano wake wa mawaziri wa Oktoba. Wakopeshaji wa sekta ya kibinafsi wamegoma kushiriki, na ushiriki kamili wa China bado haueleweki, hata ingawa ni mojawapo ya nchi za G-20. Shirika la Oxfam International na mashirika mengine yasiokuwa ya kiserikali yalisema wiki iliyopita kwamba mradi huo hautoshelezi, haswa ikiwa kutakuwa hakuna ushiriki wa sekta ya kibinafsi, kwani ingali inahitajika nchi za kutosha kulipa karibu dola bilioni 34 mwaka wa 2020.

Amerika Yaagiza Kufungwa kwa Ubalozi wa China jijini Houston

Kwa ghafla Amerika iliagiza kufungwa kwa ubalozi wa China jijini Houston ikitaja kuwepo “ujasusi haramu uliokithiri na operesheni za ushawishi,” na kuwapa Wachina masaa 72 kuondoka. Hili limekuja chini ya muda wa siku baada ya Wizara ya Haki kuituhumu China parwanja kwa kuwasaidia wadukuaji wa mtandaoni kujaribu kuiba utafiti wa COVID-19 kutoka kwa kampuni za Amerika. Imeripotiwa kwamba Wachina hao walichoma moto nyaraka nyingi kabla ya kuondoka hadi kupelekea Idara ya Zimamoto ya Houston kuitwa katika eneo la tukio. Uhusino kati ya China na Amerika umefikia katika hali mbaya na japokuwa dola zote huendesha operesheni za kijasusi nje ya balozi zao, kitendo hiki kilichofanywa na Amerika kitapelekea kuvurugika kabisa njia za kidiplomasia.

Chama cha Assad cha Baath Chashinda Viti Vingi katika Uchaguzi wa Ubunge

Chama cha Raisi wa Syria Bashar al-Assad na washirika wake kimeshinda viti vingi katika uchaguzi wa ubunge wa nchi iliyo chakazwa kwa vita, ulipingwa na kuitwa kama "Usanii" na wapinzani walio uhamishoni. ile orodha inayoitwa "Umoja wa Kitaifa" ilishinda viti 177 vya ubunge kati ya 250. Utokelezeaji wa wapiga kura ulikuwa ni asilimia 33, ikilinganishwa na asilimia 57 miaka minne iliyopita. Mamilioni ya watu wameikimbia nchi kufatia vita vya muda mrefu na hawakuwa na uwezo wa kupiga kura, ambazo zimefanyika huku uchumi ukiwa katika hali mbaya. "kwa ufupi sema, huu ni uchaguzi usio halali. Serikali iliwateua wagombeaji, hata wale wa kibinafsi, na kuwachagua," Yahya al-Aridi, mwanachama wa kamati ya upinzani katika mazungumzo ya Umoja wa Mataifa jijini Geneva, alinukuliwa akisema hayo kupita shirika la habari la dpa news. " Watu wengu wa Syria wanaamini uchaguzi huu ni mchakato tu unaofanywa na serikali hii ili kujiwasilisha kama utawala halali nchini Syria," Zaki Mehchy, mshauri mkuu katika jumba la  Chatham  na mwanzilishi mwenza wa kituo cha utafiti wa sera cha Syria, aliiambia  Al Jazeera kabla kura hazijapigwa. "Watu wanajua kwamba wengi katika wabunge wameteuliwa na chama cha Baath na wote wanahitaji kuthibitishiwa usalama kwa msingi wa utiifu na wala sio sifa za taaluma," alisema.

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 09 Agosti 2020 15:16

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu