Alhamisi, 09 Rajab 1446 | 2025/01/09
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

  Vichwa vya Habari 26/09/2020

Vichwa vya Habari:

Waziri Mkuu wa Pakistan Aikosoa India katika UN Huku Akisahilisha Kuichukua kwake Kashmir

Utawala wa Trump Kufanya Kazi Kusawazisha Mahusiano na Sudan kabla ya Uchaguzi

Amerika Yaamuru Serikali ya Iraq Kudhibiti Wanamgambo

Maelezo:

Waziri Mkuu wa Pakistan Aikosoa India katika UN Huku Akisahilisha Kuichukua kwake Kashmir

Haingewezekana kiurahisi kwa India kuchukua hatua ya kuliambatanisha jimbo la Jammu na Kashmir bila idhini ya kimya ya Pakistan, nchi ya kutisha ya nyuklia ambayo inapakana moja kwa moja na India. Lakini mnamo Ijumaa, Waziri Mkuu wa Pakistan Imran Khan alikuwa akikosoa sera za India katika hotuba yake isiyo ya ana kwa ana kwa Umoja wa Mataifa. Kwa mujibu wa gazeti la The Washington Post:

Waziri Mkuu wa Pakistan Imran Khan mnamo Ijumaa aliishambulia serikali ya kitaifa ya Kibaniani na hatua zake za kuimarisha udhibiti wa Kashmir iliyo na Waislamu wengi, na kuiita India nchi inayofadhili chuki na mapendeleo dhidi ya Uislamu. Khan alisema katika mkutano wa kila mwaka wa Umoja wa Mataifa wa viongozi wa ulimwengu kwamba hofu ya Uislamu inaitawala India na kuwatishia Waislamu karibu milioni 200 wanaoishi huko.

"Wanaamini kuwa India ni ya Mabaniani pekee na wengine sio raia sawia," alisema katika hotuba iliyorekodiwa kwa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ambao unafanywa kwa njia isiyo ya ana kwa ana kutokana na janga la virusi vya korona ... Wakaazi wa eneo linalodhibitiwa vikali kijeshi na India la Kashmir wanasema vikosi vya usalama vimewakamata maelfu ya vijana, wamevamia nyumba za watu, wamewapiga na kuwatia shoti za umeme, na kutishia kuwachukua na kuwaoa jamaa zao wa kike. Maelfu ya waandamanaji katika mwaka uliopita walijeruhiwa na vidonge vya risasi, pamoja na mamia waliopofushwa katika jicho moja au macho yote mawili. Kwa miezi saba, hadi Machi, eneo hilo lilikuwa chini ya kukatika kwa mawasiliano, huku mitandao ya kijamii na utumizi wa mtandao ukipigwa marufuku. "Jamii ya kimataifa lazima ichunguze ukiukaji huu mkubwa na kuwashtaki maafisa wa kiraia wa kijeshi wa India na waliohusika katika ugaidi wa serikali na uhalifu mkubwa dhidi ya binadamu," Khan alisema.

Kwa kweli Pakistan na India zinashirikiana pamoja dhidi ya Waislamu wa Kashmir, ili kumaliza suala hili kwa kuiingiza Kashmir ndani ya India. Amerika inataka Pakistan kusahilisha mapambano ya India dhidi ya China, nguvu inayokua ambayo inatishia kuingilia udhibiti wa kimkakati wa Amerika wa Bahari ya Pasifiki. Gharama kwa Pakistan ni kuwatoa kafara mamilioni ya Waislamu huko Kashmir kwa dola ya Kibaniani, na gharama kwa India ni uhusiano wa amani na jirani yake mkubwa; wote wakitoa huduma kwa malengo ya kitaifa ya Amerika. Matangazo ya umma ya Imran Khan dhidi ya India hayakusudiwi tu kuficha ulegevu wake katika uhalifu wa India. Yanakusudiwa pia kuikaribisha diplomasia ya Amerika ndani ya mzozo huu, kuunda njia nyingine ya Amerika kuingilia kati.

Uovu wa watawala wetu wa Kiislamu hivi karibuni utafichuka waziwazi kabisa na Umma wa Kiislamu utainuka tena, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, kulipindua tabaka hili la watawala vibaraka na kurudisha Dola ya Kiislamu ya Khilafah Rashida kwa njia ya Mtume (saw).

Utawala wa Trump Kufanya Kazi Kusawazisha Mahusiano na Sudan kabla ya Uchaguzi

Huku Raisi wa Amerika Donald Trump akiwa nyuma ya uchaguzi, utawala wake unafanya kazi kwa bidii kuonyesha mandhari kadhaa za uhusiano wa kigeni kwa wakati muwafaka kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Novemba. Ingawa Sudan imekuwa chini ya udhibiti wa Amerika kwa miongo kadhaa, msimamo mkali wa kisiasa wa kibaraka wa Amerika na Rais wa zamani Omar al-Bashir ulimaanisha kuwa Amerika haingewezi kutangaza hadharani uhusiano wake naye. Lakini huku kupoteza kibaraka muhimu mwaka jana ilikuwa ni hasara kubwa kwa Amerika, ilileta faida ya kufungua njia kwa Amerika kurudisha uhusiano hadharani na Sudan. Kulingana na The Hill:

Utawala wa Trump unasisitiza juu ya kuiondoa Sudan kutoka katika orodha ya wafadhili wa kiserikali wa ugaidi katika hatua ambayo inaweza kuanzisha nchi hiyo ya Afrika Mashariki kufungua uhusiano na Israeli na kumpa rais ushindi mwingine wa sera ya kigeni kabla ya uchaguzi.

Lakini mwendo mkali ambao utawala huo unatarajia kupata mpango na nchi hiyo umezidisha shinikizo kwa Bunge la Congress, ambalo limekwama juu ya sheria ambayo itaifanya Sudan kulipa fidia kwa wahanga wa ugaidi kwa badali ya kinga kutokana kwa madai mengine ya kigaidi.

Na wahanga wa ugaidi - ambao ni pamoja na wale waliojeruhiwa na kuuawa katika mashambulio ya mabomu ya majengo pacha ya ubalozi nchini Kenya na Tanzania mnamo 1998, pamoja na wahanga wa 9/11 - pia wamegawanyika ikiwa sheria ya majimbo itaumiza au kudhuru kesi zao.

Hata hivyo utawala huo unasisitiza kwa bidii Sudan kuitambua Israel kama sehemu ya ahadi ya Trump ya kutoa "tano au sita" nchi zaidi za Waarabu au nchi zenye Waislamu wengi kuasisi uhusiano wa kidiplomasia na Jerusalem kufuatia makubaliano yaliyosainiwa na Imarati na Bahrain.

Makubaliano na Sudan yatakuwa ni mafanikio makubwa ya kidiplomasia kwa Trump kabla ya uchaguzi, ikizingatiwa historia ya Khartoum kama eneo maarufu la azimio la "hapana tatu" la Jumuiya ya Kiarabu mnamo 1967, ambayo ilitangaza hakuna amani, mazungumzo au kutambuliwa kwa Israel. Na Trump anatafuta kuuza mafanikio ya makubaliano hayo katika Mashariki ya Kati kabla ya uchaguzi, licha ya kukataliwa kimataifa kwa Mpango wake uliopendekezwa wa Amani ya Ustawi kama suluhisho la mzozo wa Israel na Palestina.

Waziri wa Kigeni Mike Pompeo amesema utawala huo unapanga kuondoa jina la ugaidi la Sudan katikati ya Oktoba, kumaliza hali ya kuhamwa kwa serikali hiyo na kuruhusu uwekezaji unaohitajika sana kwa serikali dhaifu ya mseto wa kiraia na kijeshi ya Khartoum, ambayo iliwekwa mwaka mmoja uliopita baada ya mapinduzi ya mashinani yaliupindua udikteta wa miaka 30 wa Omar Al Bashir.

Ni muhimu tuangalie zaidi ya msimamo wa kisiasa ili kutambua hali halisi ya mienendo ya kisiasa ya kimataifa. Baadhi ya watawala wetu wanafanya urafiki na Amerika waziwazi, na wengine wanaishambulia Amerika hadharani huku wakitekeleza maagizo ya Amerika faraghani, hata kwa madhara ya maslahi yao wenyewe. Umma wa Kiislamu hautapata tena udhibiti wa mambo yake mpaka awalazimishe watawala wake kujitolea kwa mfumo wa Kiislamu kwa kusimamisha tena Dola ya Kiislamu la Khilafah Rashida kwa njia ya Mtume (saw).

Amerika Yaamuru Serikali ya Iraq Kudhibiti Wanamgambo

Kusudi la Amerika kupunguza idadi ya vikosi nchi Iraq halikuwa kurudisha uhuru wa Iraq bali kuhamisha jukumu la usalama wa ndani kwa serikali ya Iraq, wakati Iraq inaendelea kutumika kama jiwe la msingi la himaya ya Amerika, kama ambavyo maagizo ya hivi karibuni ya Amerika kwa serikali ya Iraq yanavyoonyesha.

Kwa mujibu wa gazeti la 'The Monitor':

Huku mashambulizi dhidi ya Amerika na misheni na kambi nyingine za kigeni nchini Iraq yakiendelea, Amerika inaionya serikali ya Iraq kwamba itachukua hatua dhidi ya wanamgambo waliohusika na mashambulizi hayo ikiwa itashindwa kufanya hivyo yenyewe.

Chanzo kimoja kilichohudhuria mkutano ulioitishwa na Rais wa Iraq Barham Salih, uliohudhuriwa na viongozi wengi wa kisiasa na wa makundi ya Iraq, kililiambia gazeti la 'The Monitor' kwamba Salih aliwaambia washiriki kwamba alikuwa amepokea barua kutoka kwa Waziri wa Kigeni wa Amerika Mike Pompeo akiionya Iraq kwamba ikiwa mashambulizi dhidi ya Amerika hayatakoma, itafunga ubalozi wake jijini Baghdad na kuwalenga wanamgambo wote wanaohusika bila ubaguzi.

Waziri wa zamani wa Kigeni wa Iraq Hoshyar Zebari alithibitisha kile ambacho chanzo hiki kililiambia The Monitor, alipoandika kwenye Twitter Septemba 24, "Onyo kali la hivi majuzi la @SecPompeo kwa #afisi ya raisi ya Iraqi ndio tishio kali zaidi kwa ustawi wa Iraq. #Viongozi wa Iraq wanapaswa kusimama kukabiliana na changamoto zinazosababishwa na wanamgambo wenye silaha kulenga #mitambo ya kidiplomasia na kijeshi ya Amerika. Iraq ni lazima ikomeshe mauaji haya na itende kwa uwajibikaji.”

Kufuatia mkutano huo, mjadala mkali ulifanyika kati ya kundi la wanamgambo wanaounga mkono mashambulizi dhidi ya Amerika na ujumbe mwingine wa kigeni, kwa upande mmoja, na mkuu wa Vitengo vya Uhamasishaji Maarufu (PMU) Falih al-Fayadh na mkuu wa kundi la Fatah la PMU Hadi al-Amiri, kwa upande mwingine.

Fayadh na Amiri walichukua hatua kali dhidi ya wanamgambo hao, wakiwataka wasitishe mashambulizi yote, kwani Amerika tayari imeanza kuondoa vikosi vyake kutoka Iraq. Waliwaonya kuwa hatua za Amerika huenda zikajumuisha kuzipiga mabomu kambi za wanamgambo hao.

Kwa kuongezea, inaonekana kwamba Fayadh na Amiri wote wanaogopa kuingia kwenye orodha nyeusi ya Amerika, haswa kwa kuwa Waziri Mkuu Mustafa al-Kadhimi anapata nguvu nyumbani na kimataifa kwa kukandamiza wanamgambo wasio chini ya udhibiti wa serikali.

Utawala wa Amerika baada ya Vita vya Pili vya Dunia haujamaliza ubeberu bali umebadilisha tu umbo lake, kutoka kwa ujenzi dhahiri wa himaya wa dola za Ulaya hadi ujenzi wa chini kwa chini wa himaya ya dola yenye nguvu kubwa ya Amerika ambayo inataka kuutawala ulimwengu wote. Hakuna serikali yoyote ya ulimwengu iliyo na uwezo wa kuindoa Amerika kutoka kwa msimamo wake. Inaangukia kwa Ummah wa Kiislamu kuibuka, kusimamisha tena dola yake, kuyakomboa maeneo yake yaliyo nyakuliwa, kuunganisha ardhi zake na kuregesha tena mfumo kamili maisha ya Kiislamu. Nguvu ya hadhara ya Kiislamu bila shaka itaisukuma Dola ya Kiislamu hadi katika hadhi ya dola kuu inayoongoza duniani, shahidi wa haki juu ya wanadamu, na mlinzi wa heshima wa mambo yote ya binadamu.

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumatatu, 28 Septemba 2020 21:51

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu