Jumamosi, 11 Rajab 1446 | 2025/01/11
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vichwa Vya Habari 02/12/2020

Vichwa vya habari:

Mwanasayansi wa Nyuklia wa Iran Auwawa

Imran Khan Asema Hatalitambua Umbile la Kizayuni

Saudia Imekubali Ndege za Umbile la Kiyahudi Zitumie Anga Yake

Maelezo:

Mwanasayansi wa Nyuklia wa Iran Auwawa

Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran limethibitisha kuuliwa kwa mwanasayansi wa nyuklia Mohsen Fakhrizadeh katika shambulizi la gari lililofanyika tarehe 27 Novemba 2020. Fakhrizadeh anachukuliwa kama ni miongoni mwa waasisi wa programu za nyuklia za Iran na kuuongoza mradi wa Iran wa AMAD, ambao ulizalisha bomu la nyuklia. Umbile la kizayuni kwa muda mrefu limekuwa likiwalenga wanasayansi na maafisa wa Iran katika vita fiche ili kudhoofisha matarajio ya Iran. Na Rais wa Amerika katika wiki zake za mwisho pamoja na Rais mteule, Joe Biden wameonekana kupendelea mkataba mpya wa nyuklia wakati ambapo umbile la Kizayuni linatarajiwa kuona fursa chache kwa hatua hizo za upande mmoja. Majibu kutoka kwa viongozi wa kidini wa Iran yamekuwa maneno matupu na vitisho vyenye hatua chache za kivitendo. Umbile la Kizayuni na Iran zinamenyana nchini Syria, Lebanon, Iraq na Palestina na licha ya urafiki wa karibu utawala huo wa kidini ulionao na Amerika hili halijafanya chochote cha maana kuipa iran usaidizi wa kutosha kukabiliana na mashambulizi kama hayo.

Imran Khan Asema Hatalitambua Umbile la Kizayuni

Chama tawala cha Pakistan kimesema hakitalitambua umbile la Kizayuni, hii ni kufuatia shinikizo kutoka Amerika na mataifa yake ya ghuba yanayotaka kusawazisha mahusiano pamoja na nchi hiyo. Nchi kadhaa hivi karibuni zimesawazisha mahusiano yao na umbile la Kizayuni kuanzia Umoja wa Falme za Kiarabu, Bahrain, Sudan na uvumi unaendelea kuzunguka kuwa Saudi Arabia na Pakistan nazo zinakadiria kusawazisha mahusiano. Huku Imran Khan akiandika katika Twitter kuangazia shinikizo alilokuwa chini yake katika kulitambua umbile la Kizayuni, uongozi wa kijeshi wa taifa hilo kwa muda mrefu umekuwa ukipima rai jumla katika hili. Kutua kwa ndege ya kitaifa mnamo mwaka 2019 kutoka Israel katika mji mkuu wa taifa kumezua tafrani na viongozi wa kijeshi wameonekana kunyamazia tukio hilo.  Uongozi wa kijeshi pasi na shaka yoyote utalitambua umbile hili kwani Amerika inaushinikiza, lakini kwa hili utajikuta pabayani na rai jumla nchini humo.

Saudia Imekubali Ndege za Umbile la Kizayuni Kutumia Anga Yake

Baada ya wiki ambapo kiongozi wa umbile la Kizayuni Benjamin Netanyahu alikwenda Saudi Arabia na baada ya ufalme huo kukataa kwamba ilifanya naye mkutano, wiki hii utawala wa Saudia umeruhusu ndege za umbile la Kiyahudi kupaa juu ya anga ya Saudia kuelekea Ghuba. Makubaliano hayo yaliwekwa wazi na mshauri mkuu wa Ikulu ya Amerika Jared Kushner na mabalozi wa Mashariki ya Kati Brian Hook na Avi Berkowitz, ambao walitembelea kanda hiyo kwa jili ya mazungumzo. Utawala wa Saudia umeonekana kujenga msingi imara wa hatimaye kusawazisha mahusiano na umbile la Kizayuni. Kwa hakika uhusiano kati ya ufalme wa Saudia na umbile la Kizayuni umekuwepo kwa muda mrefu, hivi sasa wameamua tu kuuweka dhahiri.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu