Jumamosi, 21 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Uhakiki wa Habari: 17/04/2021

Biden Atangaza Kujiondoa kutoka Afghanistan Ifikapo Tarehe 9/11

Wiki hii Rais wa Amerika Joe Biden ametangaza kwamba hatarudisha nyuma uamuzi wa mtangulizi wake wa kuondoa majeshi kutoka nchini Afghanistan lakini atachelewesha hilo hadi kufikia tarehe 11 Septemba 2021, tarehe hiyo itakuwa ni sawa na kufikisha miaka 20 tangu kutokea mashambulizi ya 9/11 ambayo ndio sababu kuu ya kuivamia Afghanistan. Rasmi, Amerika inadai kuwa na vikosi 2,500  pekee nchini  Afghanistan  na sasa itaanza kuwaondoa ifikapo tarehe 1 Mei, badala ya zoezi hilo kuisha tarehe 1 Mei kama ilivyojitolea Rais Trump katika makubaliano ya amani kati ya utawala wake na Taliban ya Afghan. Kufatia tangazo hilo la Biden, Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg akiwa jijini Brussels alisema muungano huo pia unawaondoa wanajeshi wake 7,000 kutoka Afghanistan. “Ni wakati sasa wa kumaliza vita vya muda mrefu vya Amerika,” Biden alisema. Pamoja na hayo, kiuhalisia, Amerika haijiondoi kutoka Afghanistan bali inabadili mtindo wake wa kuikalia kutoka katika kujihusisha moja kwa moja kijeshi hadi kujihusisha kijeshi kusio kwa moja kwa moja kama inavyofanya nchini Syria.

Amerika iliingia Afghanistan pamoja na Iraq kwa ujasiri mkubwa kufuatia matukio ya 9/11. Muongo mmoja tu kabla, kambi ya kisovieti ilikuwa imeanguka na kuiacha Amerika kuwa ndio dola pekee kuu ulimwenguni. Amerika ilitafuta kufunga ubabe wake kwa kuvamia kinguvu ardhi za Waislamu, kujenga kambi imara za kijeshi hapa, kwa kuwa sifa ya eneo la kistratejia la ardhi za Waislamu humpa manufaa makubwa kwa yeyote anayeweza kuzimiliki. Amerika ilifanikiwa kuzivamia nchi zote hizi mbili lakini ikazidiwa katika kila mojawapo na vikosi vya jihad. Ujasiri wa Amerika umetikiswa pakubwa, na Amerika ikafanya uhakiki wa uwezo na mwelekeo wake hivyo na kupelekea kuja na mtindo mpya wa uvamizi, kama inavyoonekana kwenye uingiliaji wa Amerika nchini Syria. Hapa, Waamerika waliweza kuidhibiti nchi hii bila ya kupeleka idadi kubwa ya vikosi vya kijeshi vya ardhini bali kwa kutumia nguvu ya jeshi la anga, ujasusi, operesheni maalumu na kuvitumia vikosi vya Ardhini vya nchi nyingine, mfano Uturuki na Iran. Huo ndio mtindo ambao Amerika inataka kuutumia hivi sasa nchini Afghanistan.

Katika makala moja katika gazeti la New York Times yaliyopewa anwani “Jinsi Amerika inavyopanga kupigana kutokea mbali baada ya vikosi kuondoka Afghanistan” Biden alinukuliwa akisema, “Tutapangilia upya uwezo wetu wa kupambana na ugaidi na rasilimali maalumu katika kanda kwa ajili ya kuzuia kuibuka kwa tishio la ugaidi katika nchi yetu.” Makala hayo pia yalimnukuu mchambuzi wa mambo ya kiusalama wa muda mrefu akisema, “Tunajihusisha kwa uchangamfu katika kupambana na ugaidi wakati ambapo kila juhudi imefanywa kwa ajili ya kupunguza ‘vikosi’ - viatu ardhini - na kuvibadilisha kwa vikosi visivyoonekana ambavyo vitapata mafanikio zaidi.” Makala hayo yameeleza zaidi kwamba Uturuki itaendelea kubakisha vikosi vyake vya ardhini nchini Afghanistan, na kwamba Amerika itajitahidi kuasisi kambi za kutoa msaada katika nchi jirani za Tajikistan, Kazakhstan na  Uzbekistan. Zaidi ya hayo, Amerika itaendelea kuitegemea Pakistan kusaidia malengo ya Amerika nchini Afghanistan, kama ilivyokuwa katika muda wote mrefu wa uvamizi wake wa nchi hiyo. Biden alisema katika hotuba yake, “Na tutaziomba nchi nyingine – nchi nyingine katika kanda hiyo – kufanya zaidi kuisaidia Afghanistan, haswa Pakistan...”

Amerika imegundua somo gumu walilojifunza nchi za Ulaya karne iliyopita, kwamba sio rahisi kuzikalia moja kwa moja ardhi za Waislamu. Kama Amerika itaendelea kuwa na udhibiti wa ardhi zetu, basi hilo ni kutokana tu na ushirikiano wa vibaraka wake miongoni mwa watawala wa Waislamu, ambao wanasaidia maslahi ya Amerika, watawala kama Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki na Imran Khan wa Pakistan. Lakini kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, hivi karibuni Ummah wa Kiislamu utawapindua viongozi hawa na badala yake kutoa viapo vyao vya utiifu, kwa uongozi wa kimfumo wa kweli, wenye uwezo, ambao utasimamisha Dola ya Kiisalmu ya Khilafah Rashida kwa njia ya Mtume (saw) ambayo itakomboa maeneo yote yaliyokaliwa kimabavu, kuunganisha ardhi za Waislamu, kurudisha mfumo kamili wa maisha ya Kiislamu na kubeba ujumbe wa Uislamu kwa ulimwengu mzima.

Iran, Pakistani, Nigeria

Eneo la Nantaz lenye utajiri mkubwa wa Urania limekuwa likilengwa na kupelekea uharibifu wa maelfu ya mitambo katika miundombinu yake ya ardhini kufuatia milipuko mikubwa iliyopelekea kuharibika mfumo wa ndani wa nishati unaojitegemea ambao hutumika kusambazia umeme. Pamoja na hayo, muda huu, Amerika imesema kwamba haihusiki. “Amerika haikuhusika kwa namna yoyote,”msemaji wa ikulu ya White House, Jen Psaki, alisema Jumatatu. “Hatuna cha kuongezea juu ya uvumi kuhusu sababu au athari zake.” Vyombo vya habari vya ndani katika umbile haramu ya Kiyahudi vimenasibisha shambulizi hilo na kazi ya chombo chake cha ujasusi, Mossad. Iran inaendelea kukumbwa na mashambulizi ya kudhalilisha kutoka kwa umbile la Kiyahudi, sio tu kwa mradi wake wa kinyuklia bali pia meli zake, wakati ambapo majibu yake ya mashambulizi yamekuwa hakuna au dhaifu mno, hii ni kwa sababu tu ya tamaa ya Iran ya kutaka kudumisha uhusiano wake wazi na Amerika. Umbile haramu la Kiyahudi limekuwa ni mtoto mbaya anaepewa kiburi na mzazi wake Amerika hivyo kupitia tabia hiyo Amerika huendelea kujiimarisha kinguvu, licha ya kuwa umbile hilo la linasalia kuwa dhaifu. Hadharani Iran daima imekuwa ikiishambulia Amerika. Lakini faraghani, utawala wa Iran mara kwa mara umekuwa ukiegemea malengo ya kistratejia ya Amerika, ikifikiri kwamba hii ndio njia ya kujiimarisha yenyewe. Kinyume chake, kujaribu kushirikiana na dola kubwa hii ni njia iliyojaa hatari.

Njia sahihi ya dola yoyote kujiendeleza yenyewe ni kupitia kupambana na maslahi ya dola kuu. Lakini uongozi dhaifu wa Iran kamwe hautaruhusu kufanya hivyo; wanatuliza hasira zao kwa hotuba za Ummah pekee.

Serikali ya Pakistan, imekumbwa na kuenea kwa maandamano kupitia Tehreek-e-Labbaik, Pakistan imetangaza kupiga marufuku vuguvugu hilo. TLP ilikuwa inaitaka tu serikali kushikimana na makubaliano yake ya awali pamoja na TLP ya kuchukua hatua za kumfukuza balozi wa Ufaransa kutokana na uungaji mkono wa Ufaransa wa kuchapishwa upya kwa vibonzo vya kumkashifu Mtume (saw). Serikali ya Pakistan inapendelea kuchukua hatua madhubuti dhidi ya TLP badala ya dhidi ya serikali ya Ufaransa. Watawala wetu hawasubutu kuzipinga nchi za Kimagharibi hata wakati nchi hizo zinapowadhalilisha.

Katika kujaribu kuimarisha akiba ya pesa za kigeni, Benki Kuu ya Nigeria wiki hii ilitangaza vizuizi vya uingizaji wa ngano na sukari, ikisisitiza haja ya uongezaji wa uzalishaji wa ndani wa bidhaa hizi msingi. Nigeria ndio nchi yenye uchumi mkubwa Afrika na muuzaji mkubwa wa mafuta nje; lakini nguvu ya kiuchumi ya Nigeria inanyonywa na Mamagharibi badala ya kuwatumikia watu wa Nigeria, kama ilivyo hali katika nchi nyingi zilizosalia ulimwenguni.  Wiki hii shirika moja la Nigeria kwa utata lilidai kwamba ni vigumu kujua ni kiwango gani cha mafuta husafirishwa ng'ambo kwa kuwa makampuni yanachimba mafuta baharini yote yanamilikiwa na wageni. Katibu Mkuu wa shirika linalojishughulisha na uwazi wa viwandani la Nigeria alisema wiki hii, “Hatuna uwezo wa kwenda ndani baharini ili kujua tunazalisha mafuta kiasi

gani, kama ilivyo hivi sasa, ni vigumu kwa Mnaigeria yeyote kufahamu ni kiasi gani tunapata. Hili ni moja ya mambo ambayo NEITI inalishughulikia. Kwa sababu kama hujui kiasi gani unachozalisha je, utajuaje kiwango cha pato unachotakiwa kupata?” Alieleza zaidi, “Makampuni yanayokwenda ndani baharini na yaliyo na hamu ya kufanya utafiti mafuta baharini sio makampuni wenyeji wa Nigeria na hayawezi kulinda maslahi ya nchi hii vilevile, lakini tunatakiwa kuyapongeza makampuni hayo; kwani yanafanya vizuri hapa, na bila hayo makampuni, sekta ya mafuta haitakuwepo.” Lakini badala ya kujikita zaidi kujenga uwezo wa ndani, serikali ya Nigeria inakusudia kushajiisha zaidi uingiliaji wa nje. Kwa mujibu wa ripoti ya Reuters wiki hii, “Nigeria imelegeza zaidi masharti ya mswada wa mageuzi ya mafuta ili kuvutia uwekezaji unaohitajika mno kwa sekta yake ya mafuta, watu wanne wanaohusika kwa karibu na sheria hiyo walisema na barua kutoka makampuni ya mafuta, ilioonekana na Reuters, ilionesha.” Baada ya Vita vya Pili vya Dunia, Magharibi ilibadili ubeberu wake rasmi wa dola za kizalendo kuwa katika mtindo mpya wa kibeberu wa kilimwengu wenye kusaidia dola za Magharibi kupata njia ya kufikia rasilimali za nchi zote zisizo za Kimagharibi. Lakini kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, punde Ummah wa Kiislamu utasimamisha tena Dola ya Kiislamu ya Khilafah ambayo, kuanzia kuasisiwa kwake, itajiunga na safu za dola kuu katika ukubwa wake, idadi ya watu, rasilimali, eneo mkakati lake, na mfumo wake, yenye kuonyesha badali sahihi, ya kivitendo na adilifu ya mfumo wa kibeberu wa Kimagharibi, na kurudisha amani jumla, utulivu na ufanisi dunia nzima, kama ilivyokuwepo kabla ya kuibuka kwa ubeberu, Ubepari na ukafiri wa Magharibi.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu