Jumamosi, 14 Muharram 1446 | 2024/07/20
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 

Vichwa vya Habari 8/11/2022

Vichwa vya Habari:

  • Marekani Yasema Zelenskiy Anahatarisha Uchovu wa Washirika wa Ukraine endapo atakataa Mazungumzo ya Urusi
  • Imran Khan Azungumza Hadharani kwa Mara ya Kwanza Tangu Kunusurika Ufyatuliwaji Risasi
  • Waundaji Chip (Vipuri vya Kompyuta) wa China Wapunguza Kasi ya Mashini za Processor ili Kukwepa Vikwazo vya Marekani

Maelezo:

Marekani Yasema Zelenskiy Anahatarisha Uchovu wa Washirika wa Ukraine endapo atakataa Mazungumzo ya Urusi

Maafisa wa Marekani wameripotiwa kuionya serikali ya Ukraine kwa faragha kwamba inahitaji kuashiria uwazi wa kufanya mazungumzo na Urusi. Maafisa jijini Washington wameonya kwamba "uchovu wa Ukraine" miongoni mwa washirika unaweza kuwa mbaya zaidi ikiwa Kyiv itaendelea kufungwa kutokana na mazungumzo, Washington Post liliripoti. Maafisa wa Marekani waliliambia jarida hilo kwamba msimamo wa Ukraine kuhusu mazungumzo na Urusi unazidi kuzorota miongoni mwa washirika ambao wana wasiwasi kuhusu madhara ya kiuchumi ya vita vya muda mrefu. Rais wa Ukraine, Zelenskiy amesema Ukraine iko tayari kuingia katika mazungumzo na Urusi iwapo wanajeshi wake wataondoka katika maeneo yote ya Ukraine, ikiwemo Crimea na maeneo ya mashariki ya Donbas, yanayodhibitiwa na Urusi tangu mwaka 2014, na iwapo Warusi hao ambao waliofanya uhalifu nchini Ukraine watakabiliwa na kesi. Zelenskiy pia aliweka wazi kuwa hatafanya mazungumzo na uongozi wa sasa wa Urusi. Mwezi uliopita, alitia saini amri inayobainisha kuwa Ukraine itajadiliana tu na rais wa Urusi ambaye amemrithi Vladimir Putin. Marekani hadi sasa imeipa Ukraine msaada wa thamani ya $18.9bn na iko tayari kutoa zaidi, ikisema kuwa itaisaidia Ukraine kwa muda wote itakavyochukua. Hata hivyo, washirika katika sehemu za Ulaya, Afrika na Amerika Kusini, maafisa wa Marekani waliiambia Post, wana wasiwasi na matatizo ambayo vita vinaweka kwenye bei ya kawi na chakula pamoja na silsila za usambazaji. "Uchovu wa Ukraine ni jambo la kihakika kwa baadhi ya washirika wetu," afisa mmoja wa Marekani alisema. Maafisa wa Marekani wameiomba Kyiv ionyeshe uwazi wake wa kufanya mazungumzo ili kutoisukuma Ukraine kuelekea kwenye meza ya mazungumzo mara moja, bali kudumisha uungwaji mkono wa washirika wanaohusika, kwa mujibu wa Post. Kwa maafisa wa Ukraine, ombi la Marekani litamaanisha kughairi miezi kadhaa ya matamshi kuhusu haja ya kushindwa kijeshi dhidi ya Urusi ili kulinda usalama wa Ukraine kwa muda mrefu - ujumbe ambao unawagusa vikali wakaazi wa Ukraine ambao wanahofia kwamba Urusi itajaribu tena kuiteka nchi katika siku zijazo. [Chanzo: The Guardian]

Inaonekana kwamba Marekani imeamua kuwa Urusi imedhoofishwa sana na kwamba mazungumzo yatasaidia kuhifadhi uwiano mpya wa mamlaka katika bara la Ulaya pamoja na Eurasia.

Imran Khan Azungumza Hadharani kwa Mara ya Kwanza Tangu Kunusurika Ufyatuliwaji Risasi

Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan Imran Khan ametoa hotuba yake ya kwanza kwa umma tangu alipopigwa risasi wakati wa maandamano katika mji wa mashariki wa Wazirabad. Akiwa ameketi kwenye kiti cha magurudumu katika hospitali moja huko Lahore, Bw Khan alisema hangeweza kunusurika kupigwa risasi ikiwa wapigaji risasi hao wawili aliowaona "wangesawazisha" shambulizi lao. "Kwa sababu nilianguka, mmoja wa wapiga risasi alidhani nimekufa, na akaondoka," alisema. Mwezi uliopita, tume ya uchaguzi nchini Pakistan ilimnyima Bw Khan kushikilia wadhifa wa umma, katika kesi iliyoelezwa na mchezaji huyo nyota wa zamani wa kriketi kuwa ilichochewa kisiasa. Katika ungamo la video lililotolewa na polisi, mwanamume mmoja anayetuhumiwa kumpiga risasi alisema mchezaji huyo wa zamani wa kriketi "alikuwa akiwapotosha" watu, na kwamba "alitaka kumuua" kwa kufanya hivyo. Hali ambazo ungamo hilo lilitekelezwa hayako wazi. Shambulizi dhidi ya Bw Khan limeichachawiza nchi hiyo, ambapo mwanakriketi huyo aliyegeuka kuwa mwanasiasa aliiongoza hadi Aprili, alipobanduliwa madarakani kwa kura ya kutokuwa na imani ya bunge. Shule zilifungwa katika mji mkuu, Islamabad, baada ya chama chake - Pakistan Tehreek-e-Insaf (PTI) - kuitisha maandamano ya nchi nzima kufuatia salwa za Ijumaa. Rais Arif Alvi - mwanachama mwanzilishi wa PTI - aliliita "jaribio katili la mauaji". Wapinzani wa kisiasa wa Bw Khan pia wamekuwa wepesi kulaani shambulizi hilo, huku Waziri Mkuu Shehbaz Sharif akiamuru uchunguzi wa haraka ufanyike. Wakati huo huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken ametoa wito wa utulivu na kusema: "Vurugu hazina nafasi katika siasa, na tunatoa wito kwa pande zote kujiepusha na ghasia, unyanyasaji na vitisho." Pakistan - ambayo inakabiliwa na mzozo wa kiuchumi unaoendelea na mafuriko makubwa - ina rekodi ya vurugu za kisiasa, kwa kuuwawa Waziri Mkuu wa zamani Benazir Bhutto mwaka 2007. Wengi walichochea mauaji yake baada ya shambulizi la Bw Khan. [Chanzo: BBC News]

Kufeli kwa mauaji ya Khan kutaongeza kasi ya uchaguzi mkuu miongoni mwa watu wanaomuunga mkono Khan. Pia kuna uwezekano wa kutoa msukumo mpya kwa walio wengi walio kimya kumuunga mkono Khan. Hata hivyo, mengi yanategemea uongozi mkuu wa jeshi ikiwa uko tayari kumvumilia Khan au una nia ya kumuondoa Khan kwenye uwanja wa kisiasa. Uwepo wa vifaru kwenye barabara ni ishara wazi kwamba uongozi mkuu wa jeshi unakusudia kuchimba vita.

Waundaji Chip (Vipuri vya Kompyuta) wa China Wapunguza Kasi ya Mashini za Processor ili Kukwepa Vikwazo vya Marekani

Alibaba na start-up Biren Technology zinaboresha muundo wao wa hali ya juu zaidi wa chipu ili kupunguza kasi za mashini za processing na kuepuka vikwazo vilivyowekwa na Marekani vinavyolenga kukandamiza nguvu za kompyuta za China. Alibaba, Biren na kampuni zengine za uundaji za China zimetumia miaka na mamilioni ya dolari kuunda mipango ya mashini za processor za hali ya juu ili kukipa nguvu kizazi kijacho cha supa kompyuta, algoriti za kompyuta na vituo vya data. Hizi zinatengezwa nje ya nchi na mtengenezaji mkubwa zaidi wa kandarasi duniani Taiwan Semiconductor Manufacturing. Lakini vikwazo vilivyotangazwa na Washington mwezi uliopita ambavyo vinazuia uwezo wa usindikaji wa semiconductor yoyote inayosafirishwa kwenda China bila leseni vimetia kitumbua mchanga katika matarajio yao. Alibaba na Biren zilikuwa tayari zimefanya majaribio ya bei ghali ya chipu zao za hivi punde zaidi katika TSMC wakati Washington ilipozindua vidhibiti. Sheria hizo zimelazimisha kampuni hizo kusitisha uzalishaji zaidi na kufanya mabadiliko katika muundo wao, kulingana na watu sita walioarifiwa juu ya hali hiyo. Wanaashiria pigo jingine kwa Alibaba, kampuni ya teknolojia iliyoanzishwa na bilionea Jack Ma. Hisa zake zimepoteza asilimia 80 ya thamani yake tangu Beijing ilipoghairi toleo la awali la kampuni pacha ya Ant miaka miwili iliyopita. Chipu mpya ya kampuni hiyo ilikuwa iwa kitengo chake cha kwanza cha usindikaji wa picha na ilikuwa karibu kuzinduliwa, kulingana na watu watatu wa karibu na suala hilo. Udhibiti wa usafirishaji wa Marekani unaenea hadi kwa watengenezaji wa chipu wa nchi ya tatu kwa sababu karibu mitambo yote ya kutengeneza semiconductor hutumia vipengele au programu za kompyuta (software) za Marekani, kumaanisha kuwa sheria zinaweza kuwa vikwazo kwa mashini zote za processor za hali ya juu zinazoingia China. Washington hapo awali ilizuia maduhuli kama hayo kutoka kwa kampuni za Chip za California Nvidia na AMD. Wakati huo huo, viwanda vya Chip vya ndani vya China viko mbali kwa miongo kadhaa kutokana na utengezaji chipu za kisasa kama zile zilizoundwa na Alibaba na Biren. Wachambuzi walisema vikwazo vya Washington, ambavyo vizuizi vya mashini za processor za hali ya juu ni sehemu moja yake, vinalenga kupunguza kwa nguvu maendeleo ya sekta ya teknolojia ya China. "Kujaribu kuifungia nchi kiwango cha teknolojia ya vifaa ni jambo kubwa," Paul Triolo, mkuu wa sera ya teknolojia katika kampuni ya ushauri ya ASG alisema. "Hilo ndilo ambalo Marekani inajaribu kulifanya kupitia kudhibiti mauzo na kufunga ramani ya utendakazi ya utengenezaji ili kufikia viwango hivi vya juu vya vifaa." [Chanzo: Financial Times]

Marekani inageuza skrubu katika maendeleo ya kiteknolojia ya China, na hii ni pamoja na juhudi za Marekani za kutenganisha silsila za usamabazaji na kuizingira China kijeshi katika eneo la Pasifiki la Asia. Kando na matamshi makali, kuna uhamasishaji mdogo sana wenye ufanisi kutoka kwa serikali ya China kupinga vikali hatua hizo. Swali linabaki kuwa je, muamala wa Amerika kwa Urusi umepunguza matarajio ya China ya kuwa dola kuu.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu