Ijumaa, 25 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vichwa Vya Habari 10/06/2020

Vichwa vya Habari:

Misri Yashutumu

Mkakati wa Arctic wa Trump

Hali Mbaya ya Kiuchumi Inakuja

Maelezo:

Misri Yashutumu

Mamlaka ya juu kabisa ya kidini nchini Misri imemshutumu Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, juu ya mpango wake wa kutaka kugeuza jumba la makumbusho la Hagia Sophia kuwa  msikiti.  Dar Al-Iftaa, jopo la juu zaidi la kisunni nchini Misri, limeuita mpango huo kuwa ni "propaganda" na muendelezo wa kile kinacho semwa kuwa ni "Kazi" ya  Istanbul. Mwanzoni mwa mwaka huu, jopo la kidini liliilenga Uturuki juu ya sekta yake maarufu ya televisheni, likidai kuweka silsila ya vipindi kama vile "Resurrection: Ertugrul" na "Valley of the Wolves", kwamba ni sehemu ya juhudi zinazo ongozwa na Erdogan ili kurudisha upya Dola ya Kiuthmani. Tangu kutokea kwa machafuko ya kiarabu, Misri imeanguka kutoka neema katika mambo ya kieneo. Tangu jenerali wa jeshi Sisi alipo pindua serikali mnamo 2013, ameangusha uchumi chini na uongozi huo wa Misri umekuwa ukitazama mataifa kama Saudi Arabia, Uturuki na Umoja wa Falme za Kiarabu kuwa maregeo katika mambo ya kidini. Hasira za hivi karibuni zinatokana na sababu hiyo.

Mkakati wa Arctic wa Trump

Rais wa Amerika, Donald Trump, amewaagiza wanausalama wake kuanza kuunda  “Meli za ulinzi zitakazokuwa zinaelea katika barafu”  ambazo zitaanza majukumu yake rasmi mwaka 2029, akitaja haja ya kulinda maslahi ya Amerika katika maeneo ya Arctic na Antarctic. Katika taarifa iliyo tolea kwa Wizara ya Kigeni, Pentagon, Biashara, Nishati, na Usalama wa Nyumbani, Trump alisema Amerika inahitaji “kuendeleza na kufanyia kazi mipango ya upatikanaji wa meli za kwenye barafu.” Trump amekuwa akiitazama Arctic, kufuatia wazo la kununua eneo la Greenland kutoka Denma mnamo mwezi Agosti 2019. Ingawa watu wa Denmark waliikataa ofa ya Amerika, Washington imeendelea na mpango wake wa kukipata kisiwa kikubwa zaidi katika dunia na mlango wa Arctic kwa muda mrefu. Mtangulizi wake Barack Obama  aliapa mnamo 2015 kumaliza “mpango huo” kwa kushirikiana na Urusi – kitu ambacho kwa wakati ule kingehitaji meli 34 za namna hiyo, mara 11 Amerika imejaribu – lakini hakuna lililowezakana. Tangu kipindi hicho, Urusi imeunda meli nyingi kubwa zenye uwezo wa kinyuklia zinazo weza kufanya kazi katika maeneo hayo yenye barafu nyingi, wakati huo huo China pia imechukua hatua ya kurusha chombo hicho mwaka 2019. Sehemu hiyo ya arctic ni ukanda mwingine ambao umekuwa ukipiganiwa, pamoja na kuyeyuka kwa barafu, njia mpya inafunguliwa itakayorahisisha biashara ya baharini kutoka mashariki ya mbali hadi magharibi. Kigezo cha maslahi ya kikanda ndicho kinachopelekea kila nchi kutaka umiliki wa eneo hilo.

Hali Mbaya ya Kiuchumi Inakuja

Dunia ilikuwa inaelekea katika mporomoko wa kiuchumi mwanzoni wa mwaka 2020 lakini janga la virusi vya Korona likazidisha mgogoro na kuufanya kuwa mbaya zaidi. Wiki hii, Ujerumani imeonyesha tarakimu zake za kiuchumi zinazo onyesha taswira ya kiza. Usafirishaji bidhaa nje wa Ujerumani mnamo Aprili ulianguka kwa asilimia 24 kwa zaidi ya mwezi na asilimia 31 kwa mwaka  – ikiwa ni mporomoko mkubwa zaidi kwa mwezi wa tangu kuanzishwa kwa takwimu za biashara mnamo 1950. Hili ni dhahiri huku usafirishaji bidhaa nje ukiwa ni nyeti mno kwa uchumi wa Ujerumani kwani unachangia kwa takriban asilimia 50 ya pato la ndani la nchi. China, Ufaransa na Amerika nao hivi punde watatoa takwimu zao za kiuchumi na inatarajiwa kwamba chumi zao zitakuwa mbaya zaidi kuliko Ujerumani.

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoIjumaa, 17 Julai 2020 11:02

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu