- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Vichwa Vya Habari 12/06/2020
Vichwa Vya Habari:
Dow Yashuka kwa Pointi 1,700 Huku Visa vya Virusi vya Korona Amerika Vikipanda, Huku Kukiwa na Mtazamo Duni wa Uchumi
Je, Amerika Inaweza Kukataa Kulipa Deni la Dolari Trilioni Moja kwa China kwa kuvitumia Virusi vya Korona kama Silaha ya Kibaolojia?
Bilionea Mkubwa zaidi wa Japan Tadashi Yanai Asema Sura ya Amerika Inavunjika.
Maelezo:
Dow Yashuka kwa Pointi 1,700 Huku Visa vya Virusi vya Korona Amerika Vikipanda, Huku Kukiwa na Mtazamo Duni wa Uchumi
Hisa za Amerika zilishuka chini, kufuatia kushuka kwa viwango vya biashara ya kila Alhamisi mchana, huku kukiwa na dalili za kuzuka upya kwa visa vya maradhi yanayo tokana na aina mpya ya virusi, na huku wawekezaji wakitafakari mtazamo duni wa uchumi wa Jumatano kutoka kwa Hazina ya Majimbo ya Amerika. Mienendo ya masoko ilikuja huku idadi ya Waamerika waliokuwa wakijisajili kwa mara ya kwanza kwa ajili ya manufaa ya wasio na kazi ikipungua tena katika wiki ya hivi karibuni. Idadi ya maambukizi ya virusi vya Korona Amerika ilipita alama ya milioni mbili na zaidi ya Waamerika 112,000 wamefariki, kwa mujibu wa Chuo Kikuu cha Johns Hopkins. Licha ya visa vichache kurekodiwa katika baadhi ya miji na majimbo, kiwango wastani cha siku saba cha visa vipya vya katika kipindi cha wiki mbili zilizo pita kingali kinaongezeka katika zaidi ya majimbo 20, ikipelekea wawekezaji kuwa na wasiwasi kuhusu wimbi la pili la janga hili la maambukizi wakati ambapo biashara zinaanza kurudia hali yake ya kawaida. Raisi Trump alitangaza ataregelea kufanya mikutano ya uchaguzi huku wa kwanza ukifanywa mjini Tulsa, Okla., mnamo Juni 19 lakini hatarajiwi kuwahitaji wahudhuriaji kutekeleza masafa ya kijamii. Wakati huo huo, Waziri wa Hazina wa Amerika Steven Mnuchin alisema Amerika haipaswi kuufunga uchumi tena hata kama kutakuweko na wimbi jengine la visa vya virusi vya korona. Idadi ya kiulimwengu ya visa vya virusi vya korona ilipanda hadi 7.39 milioni mnamo Alhamisi, kwa mujibu wa data. Kiwango cha vifo kilipanda hadi 417,022. Mapema, mnamo Jumatano taarifa ya sera iliyo jadidishwa na tabiri za Fed ziliashiria kwamba inatarajia upungufu wa asilimia 6.5 mwishoni mwa mwaka kwa msingi wa mwaka nenda mwaka rudi, huku kiwango cha ukosefu wa ajira kikimalizikia kwa asilimia 9.3, juu ya makadirio ya Fed ya kiwango cha utabiri cha muda mrefu cha asilimia 4.1. Mtazamo mkali wa benki kuu unahusika katika kuuzwa kwa soko la hisa kwa bei duni, alisema Kristina Hooper, mwanamkakati mkuu wa masoko wa kiulimwengu wa Invesco. "Soko la Hisa limekuwa karibu na vipofu," Hooper alisema katika moja ya mahojiano. "Moja kati ya kampuni tatu katika S&P 500 zinasambaza kwa mwongozo wa mapato. Hivyo wawekezaji wamekwamilia data, ambazo zimekuwa nzuri kuhusu kufunguliwa tena kwa majimbo kadha wa kadha, kuboreshwa kwa PMI na ripoti ya kazi wiki iliyopita. Kwa mkupuo mmoja Jay Powell aliirushia maji ya baridi simulizi hiyo. "Hooper anadhani mienendo ya soko ya wiki hii sio lazima iwe ndio mwanzo wa awamu endelevu ya chini. "Kawaida majibu ya awali kwa mkutano wa waandishi habari wa Fed sio athari inayofuata. Kunahitajika kuweko na baadhi ya tafakari kwa wawekezaji." Nchi Amerika katika data ya kiuchumi ya Alhamisi, Waamerika wengine 1.54 milioni wamesajili madai ya mwanzo ya kutokuwa na kazi, serikali ilisema. Hayo yanapiku matarajio ya watu 1.565 milioni wanaotafuta manufaa ya ukosefu wa ajira, kwa mujibu wa itifaki ya Econoday. Ingawa madai mapya ya ukosefu wa kazi yamekuwa yakishuka tangu Machi, zaidi ya maombi 2.2 milioni ya fidia ya ukosefu wa ajira yalifanywa katika wiki ya mwisho ya Mei kupitia mipango ya misaada ya dola na majimbo. Hiyo ni takriban zaidi ya kazi 2.5 milioni zilizo patikana tena na uchumi katika mwezi huo mzima. [Chanzo: Market Watch].
Uhalisia bandia wa mashini ya kuchapa ya Fed umegongana na uchumi halisi, na masoko yameshuka. Ongezeko kubwa katika Dow Jones limesukumwa na Fed na C-Suite kwa mashirika makubwa kurudia ununuzi wa hisa, ili yaweze kutoka yakiwa tajiri zaidi kuliko yalivyo kuwa nyuma.
Je, Amerika Inaweza Kukataa Kulipa Deni la Dolari Trilioni Moja kwa China kwa kuvitumia Virusi vya Korona kama Silaha ya Kibaolojia?
Mahusiano baina ya China na Amerika yapo wakati wote. Raisi wa Amerika Donald Tramp amekuwa akiiandama China muda wote na hata kufikia hatua ya kutishia kukata mahusiano na nchi hiyo. Lakini, hatua hatari zaidi ambayo Marekani inaweza kuchukua dhidi ya China, kama inavyopendekezwa na baadhi ya Wajuzi wa Sheria wa mrengo wa kulia na wataalamu wa kisiasa, ni kukataa kulipa deni la China la dolari trilioni moja kutoka katika hazina ya Amerika. Seneta Lindsey Graham, rafiki wa karibu wa Raisi wa Marekani Donald Trump alisema wakati akizungumza na Fox News “Wao (China) ndio wanapaswa kutulipa sisi, sio sisi tuwalipe wao” Wakati huo huo akimuunga mkono seneta mwenziwe Marsha Blackburn aliye sema kwamba Marekani yafaa kulifuta deni hilo la China. John Yoo ambaye ni profesa wa sheria katika Chuo Kikuu cha California, Berkley naye pia alisema katika makala moja kuwa Amerika yaweza kuifanya, "China ilipe kwa sababu ya virusi vya Korona" kupitia kujitolea kwake upya kwa wamiliki wa bondi. "Kwa bahati nzuri, Washington ingeweza pia kuzuia deni hilo kutoka hazina na kufanya kuwa ni fidia kwa walio athirika na janga la virusi vya Korona". Kuna baadhi ya wataalamu wanatofautiana na mawazo hayo kwa kusema - Sisi ni soko kubwa zaidi la deni ulimwenguni pindi linapokuja suala la uhuru wa madeni na dolari imepewa thamani na kuwa ndio pesa akiba ya Dunia. Tatizo katika dhana hii ni kwamba itapelekea ongezeko la viwango vya riba na kushuka thamani kwa dolari na hayo yataathiri masoko. Moja kati ya fursa kubwa ambayo Marekani inayo ni gharama ndogo ya kukopa na suala la msingi mno ni kwamba tunalipa deni letu na hilo limeshapitishwa na walipa kodi wa Amerika na uchumi." Alisema Mark Sandi, ambaye ni mwana uchumi mkuu katika shirika la Moody's Analytics. Kama Amerika itajitoa kimakusudi katika yale ilojifunga nayo, fursa hiyo itapotea. Itamaanishi kwamba wawekezaji wote watalipia gharama endapo serikali ya Amerika itazisi kuwafadhaisha kwa sababu yoyote ile… na kutolipwa bondi zako,” Zandi alisema. Na watahitaji riba kubwa zaidi kwa kuchukua hatari hiyo. Mapema, kama ilivyoripotiwa na EurAsia timed, kwamba kuna kesi iliyo fikishwa kwenye Mahakama ya Wilaya ya Texas nchini Amerika kutafuta fidia kwa uharibifu unaozidi dolari trillion 20 dhidi ya China kwa "kutengeneza na kuachilia kwa makusudi au kwa bahati mbaya" virusi vipya vya korona kama silaha ya kibaiolojia kwa kukiuka majukumu ya China ya kimataifa. Walalamishiwamedai kiwango kikubwa mno cha dolari trilioni 20 za Amerika, ambacho hata kinapita uzalishaji wa ndani wa China, wakidai virusi vya Korona ni silaha ya kibaolojia iliyo tayarishwa na Beijing. Wameilaumu China kuandaa na kusababisha vifo, kuwapa msaada wa kimada magaidi, njama ya kujeruhi na kuuwa raia wa Amerika, uzembe, vifo visivyo na hatia, mashambulizi na hujma. Wakati hu huo, mshauri mkuu wa mambo ya kiuchumi katika ikulu ya White House,Larry Kuldow, ilidhibitisha katika mahojiano ya hivi karibuni kuwa hatarajii China itauza deni la Marekani kwa sababu kufanya hivyo "kutaifilisisha serikali ya China". Lakini China ilitathmini uwekezaji wake kwa uchache kuwa ni imekuwa ikipunguza poleple sehemu ya umiliki wake ni dolari za Kimarekani bilioni 36 katika miezi 3 ya kwanza ya mwaka 2020. "Nafikiri kuwa wamesha anza kuwa na tahadhari katika manunuzi yao” alisema Zandi. “Ikiwa China italichukulia swala hill kwa umakini, basi watafanya manunuzi kwa tahadhari zaidi” - jambo ambao litafanya kiwango cha riba ya kukopa kupanda na Kufanya iwe ghali zaidi kwa Idara ya Hazina kulilipa madeni yake makubwa. [Chanzo: Eurasian Times]
Ukweli ni kwamba Marekani inafikiria juu ya kulitupilia mbali deni la China, ili kuiadhibu kwa kusababisha virusi vya Korona, inaonyesha dhahiri kuwa Marekani haijajiandaa kuingia katika mapambano ya kivita na China. Jambo la kutarajiwa ni China kuwa na ujasiri wa kuonyesha nguvu zake kiuchumi na kijeshi katika bahari ya Pasifiki.
Bilionea Mkubwa zaidi wa Japan Tadashi Yanai Asema Sura ya Amerika Inavunjika.
Mzozo wa kimahusiano wenye sura ya ubaguzi wa rangi umebadilisha mtazamo wa dunia kwa Amerika. Haya ni kwa mujibu wa tajiri mkubwa zaidi wa Japan. "Sura ya Amerika inazidi kuvunjika," alisema Tadashi Yanai, Afisa Mkuu Mtendaji wa kampuni ya Uniqlo mmiliki wa Fast Retailing, alikiambia kitengo cha biashara cha shirika la habari la CNN katika mahojiano maalumu. "Natumai kwamba hili litakuwa na athari nzuri ya muda mrefu, kama ilivyotokea katika vuguvugu la madai ya haki za kiraia". Alisema Yanai ambaye ana umri wa miaka 71 na billionea mkubwa zaidi Japan na pia mmoja kati ya watu matajiri duniani. Utajiri wake una kadiriwa kufikia dolari bilioni 31.3, haya ni kulingana na BOOMBERG. Katika wiki za hivi karibuni, shughuli za kampuni katika miji mikubwa nchini Amerika kama New York, Philadelphia, San Francisco na Los Angeles zimepata "pigo kubwa" baada ya kutokea maandamo nchi nzima juu ya kifo cha George Floyd.” alisema Tadashi Yanai. Inaonyesha ni jinsi gani Wamarekani wamekasirishwa mno na tukio hilo. Hali ya kisiasa sio nzuri. Haiendi vizuri," aliongeza. "Kunatakiwa kuwepo na hisia nzito ya kuchukua hatua wakati ambao kuna matatizo ya kijamii, sio sawa kuendelea kupuuza mambo kama ilivyo hivi sasa".[Chanzo: CNN]