Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Jibu la Swali

Bin Salman na Uhalalishaji Mahusiano na Mayahudi
(Imetafsiriwa)

Swali:

Mnamo tarehe 21/9/2023, BBC News Arabic ilitangaza kwenye wavuti wake: (Mfalme Mtarajiwa wa Saudia alitangaza katika mahojiano na Mtandao wa Habari wa Fox wa Marekani, dondoo ambazo zilipeperushwa mnamo Jumatano, kwamba Ufalme huo "unafanya maendeleo" kuelekea uhalalishaji mahusiano na Israel. Alisema: "Kila siku tunakaribia zaidi na zaidi uhalalishaji mahusiano na Israel." Aliongezea, "Kuna uungwaji mkono kutoka kwa utawala wa Rais Biden kufikia hatua hiyo..."). Ujumbe mmoja wa Kiyahudi ulishiriki hadharani nchini Saudi Arabia: (Mamlaka za Israel zilionyesha furaha yao kwa uwepo wa ujumbe wa serikali nchini Saudi Arabia kuhudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa, wa Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) jijini Riyadh, zikiuzingatia ni hatua ya kwanza ya njia ya kuhalalisha mahusiano kati ya nchi hizo mbili (France 24, 11/9/2023). Je! Saudi Arabia inakaribia kufuata makubaliano ya uhaini wa Kiarabu na kujenga mahusiano na umbile la Kiyahudi?

Jibu:

Ili kuliweka wazi jibu hilo, tutahakiki mambo yafuatayo:

Kwanza: Kwa mujibu wa habari zinazozunguka, pande za mchakato wa uhalalisha mahusiano ni umbile la Kiyahudi, Saudi Arabia, na Marekani, na kuna ukweli unaohusiana na pande hizi vitatu:

1- Umbile la Kiyahudi linazingatia kuwa uhalalishaji mahusiano wowote na nchi yoyote katika kanda ya Kiarabu na Kiislamu ni mafanikio makubwa ya kumakinisha uwepo wa umbile la Kiyahudi na kulifanya "la milele" kulingana na matakwa yao. Kwa hivyo, serikali zote za umbile la Kiyahudi zinakimbilia kupata mwanya wowote ambao kwao wanaweza kuingia katika nchi za Kiislamu, haswa zile za Kiarabu.

2- Kwa kuwa Saudi Arabia ni mojawapo ya serikali za kanda hiyo ambazo hazioni haja ya vita na Mayahudi ili kuikomboa Palestina yote, serikali ya Saudia imekuwa ikidumisha mawasiliano na umbile la Kiyahudi kwa muda mrefu, lakini kwa siri. Kwa hivyo, Saudi Arabia haijali kimsingi kuanzisha mahusiano na umbile la Kiyahudi. Kwa kweli, mfalme wake wa zamani Abdullah bin Abdulaziz al Saud ndiye aliyezindua mpango wa usaliti wa Kiarabu 'mnamo 2002, na Saudi Arabia inaendelea kutangaza kushikamana nao.

3- Kwa upande wa Marekani, tawala zote za Marekani zimekuwa zikifanya kazi kwa miongo kadhaa kwa ajili ya 'amani' kati ya Mayahudi na majirani zao wa Kiarabu ili kuleta utulivu wa umbile la Kiyahudi, kulioanisha ndani ya kanda hiyo, na kuondoa ugeni wake. Vyama viwili vya Marekani (Democrat na Republican) havipingani juu ya hili.

Pili: Licha ya mazingira haya ya pande tatu ambayo yana uwezo wa kuhalalisha mahusiano, licha ya hayo, kadhia hii imejaa shida kuu za kisiasa:

1- Kupitia upinzani wake hadharani kwa makubaliano ya nyuklia na Iran mnamo 2015 na kuchochea kwake katika Bunge la Congress la Marekani dhidi yake, Netanyahu alipinga sera ya Rais wa Marekani wakati huo Obama kuhusu suala la nyuklia la Iran, na hii ilisababisha uchafuzi wa mahusiano ya umbile la Kiyahudi na Chama cha Kidemokrasia cha Marekani. Wakati Rais Trump na utawala wake wa Republican walipoanza kutawala jijini Washington mwanzoni mwa 2017, mahusiano kati ya umbile la Kiyahudi na utawala wa Republican jijini Washington ulianza kufufuka, ambapo ililipa umbile hilo kutambuliwa kwa Jerusalem kama mji wake mkuu, na Ubalozi wa Marekani ulihamishiwa hadi Jerusalem na pia ulitambua uunganishaji wake wa Golan.

Pindi utawala mpya wa Kidemokrasia ukiongozwa na Biden uliporudi madarakani mwanzoni mwa mwaka 2021, mahusiano kati ya Tel Aviv na Washington yakawa baridi tena. Kwa kweli, utawala wa Biden ulikataa kumpokea Netanyahu katika Ikulu ya White House hadi hivi karibuni baada ya kupangilia tena mahusiano. Kati ya ahadi za uchaguzi za Netanyahu ilikuwa ni kuhalalisha mahusiano na Saudi Arabia. Ilifichuliwa hivi majuzi kuwa kulikuwa na mawasiliano halisi kati ya Netanyahu na Bin Salman [gazeti la Israel la Jerusalem Post lilisema, Jumatatu, 22/5/2023, kwamba Waziri Mkuu wa Israel Netanyahu alizungumza kwa simu na Mfalme Mtarajiwa wa Saudia mara mbili katika kipindi cha wiki kadhaa zilizopita... na Riyadh iliwasilisha orodha ya matwaka kwa Israel yanayohusiana na kadhia ya Palestina. (Arab Post, 23/5/2023)].

2- Serikali ya sasa ya Saudia, inayoongozwa na Bin Salman, inachukuliwa kuwa mtiifu zaidi kwa Marekani, baada ya utawala wa Trump kumuondoa kibaraka wa Marekani, Mohammed bin Nayef, kutoka kwa mamlaka nchini Saudi Arabia na kumkabidhi mamlaka kibaraka mwengine, Mohammed bin Salman (MBS). Hii ilikuwa katikati ya mwaka wa 2017, ambayo ni, miezi sita baada ya utawala wa Republican wa Trump kuchukua madaraka jijini Washington. Kwa hivyo, Serikali ya Bin Salman ni tiifu mno kwa Marekani, lakini inadaiwa mshikamano wake kimsingi na Republican na kundi la Trump... Kutokana na haya, serikali ya bin Salman imempa mgongo Biden kwa kushajiishwa kwa siri na kundi la Trump nchini Marekani, Na utawala wa Biden umefanya jambo hilo hilo. Biden alitangaza kwamba hatashikana mikono na bin Salman dhidi ya mazingira ya mauaji ya Khashoggi.

3- Utawala wa Biden uliingia mamlakani nchino  Marekani mnamo 2021 dhidi ya mazingira ya mgawanyiko mkubwa wa Marekani ambao ulitishia na unaendelea kuishi maisha ya kisiasa nchini Marekani kwa jumla. Vyama viwili vinavyogombana (Democrat na Republican) vimeshiriki katika uwanja mkubwa wa ndani na wa nje wa migogoro kati yao kwa njia inayofanana na mgawanyiko wa wafuasi na vibaraka kwenye mandhari ya kimataifa na kuwaajiri kwa manufaa ya chama kimoja dhidi ya Chama chengine katika mzozo wa ndani wa Marekani, kama vile ilivyosemwa kuhusu upunguzaji wa Saudi Arabia wa uzalishaji mafuta pamoja na Urusi ili kuipa pigo Democrat nchini Marekani wakati wa uchaguzi bunge la congress wa 2022, na kama vile taarifa kubwa iliyotolewa na umbile la Kiyahudi baada ya kurudi kwa Netanyahu madarakani dhidi ya kurudi kwa Marekani kwenye makubaliano ya nyuklia na Iran, ambayo ni mambo ambayo Chama cha Republican na kundi la Trump hufaidika nayo ili kurudi madarakani tena, kwa hivyo utawala wa Biden uligundua kuwa nyuzi za uhalalishaji mahusiano za Saudia na umbile la Kiyahudi zilikuwa nje ya udhibiti wake baada ya Netanyahu kurudi madarakani mwishoni mwa 2022.

Tatu: Marekani ilikagua upya mahusiano yake na Saudi Arabia na kuregesha joto kwake. Pia iliimarisha mawasiliano yake ndani ya umbile la Kiyahudi, lakini kutoka kwa msimamo wa nguvu, yote kwa lengo la kuzikamata nyuzi za uhalalisha mahusiano kati ya Saudi Arabia na umbile la Kiyahudi na kuzitoa kutoka kwa mikono ya Republican:

1- Baada ya serikali ya Mohammed bin Salman kukataa ombi la Utawala wa Biden mnamo 2022 kuahirisha kupunguzwa uzalishaji wa mafuta kwa mwezi mmoja, utawala wa Biden uligundua kina cha uhusiano kati ya kundi la Trump na Saudi Arabia, kwa hivyo ulianza mara moja kutoa ukosoaji wake wa Saudi Arabia. Wana republican nchini Marekani walikuwa wakimdhihaki Rais Biden, ambaye usisitizaji wake ulisababisha kutogusa mkono wa bin Salman, lakini akamsalimia kwa bonge la ngumi badala yake, na akakataa mkutano wa faragha naye, lakini badala yake alikutana naye ndani ya ujumbe wa Saudia ulioongozwa na Mfalme Salman, Walishikilia kwamba sera ya Biden ndiyo inayohusika na kuongezeka kwa bei ya mafuta.

2- Mshauri wa Usalama wa Kitaifa wa Marekani Jake Sullivan alizuru Saudi Arabia na kufanya mkutano wa dhati na Mfalme Mtarajiwa wa Saudia Mohammed bin Salman, akizindua awamu mpya ya danganya toto ya Marekani kwa Saudi Arabia baada ya mahusiano yaliobadilika; ambayo iliwakilishwa kwa kuwashukuru kwa kuwaokoa Wamarekani kutoka Sudan, kushauriana nayo kuhusu maendeleo nchini Yemen, na kuipatia dori kubwa zaidi katika siasa za Marekani na dori yake katika kuiunganisha India na ulimwengu. (France 24, 8/5/2023).

3- Ziara ya Blinken kwenda Saudi Arabia [Waziri wa Kigeni wa Marekani Blinken alisisitiza juu ya uhalalishaji mahusiano kati ya nchi hizo mbili, washirika wawili wa kimkakati. Wakati wa kongamano hilo, mawaziri hao wawili waligusia juu ya kurudi kwa Syria kwenye Ligi ya Kiarabu, Mgogoro wa Sudan, na suala la kuhalalisha mahusiano na Israel. (France 24, 9/6/2023)].

4- Kuondoa mvutano kati ya Iran-Saudi. Hili lilielezewa kwa kina katika jibu la swali: maridhiano kati ya Saudia Iran la tarehe 1/4/2023. Saudi Arabia anajua kuwa makubaliano haya yana thamani kubwa katika utulivu wa utawala wake, na Marekani ilikuwa ikitangaza kwamba inajua kile China inafanya na Saudi Arabia na Iran. Ilinyanyua pia hadhi ya Saudi Arabia kwa kushiriki pamoja nayo katika mazungumzo ya kusitisha vita jijini Jeddah kati ya jeshi la Sudan na Kikosa cha Msaada wa Haraka tangu 8/5/2023.

5- Katika Mkutano wa G20, uliofanyika nchini India mnamo 9/9/2023, Saudi Arabia iliibuka kama mstari wa kati kati ya Njia za Bahari ya Mashariki kutoka India na zile za Magharibi hadi Ulaya, kwani ni jambo kuu katika Ukanda wa Kiuchumi wa Biden , unaounganisha India na Ulaya kupitia Saudi Arabia na umbile la Kiyahudi. [Saudi Arabia ilikubaliana na India hapo awali kwamba itasukuma uwekezaji wenye thamani ya dolari bilioni 100 (Al Jazeera Net, 11/9/2023)]. Yote haya yanaonyesha kuongezeka kwa ushiriki wa Bin Salman katika sera za Utawala wa Biden, ingawa ni utawala wa Democrat, hata kama hata kata uhusiano na Republican!

6- Utawala wa Biden unafanya mazungumzo na serikali ya Bin Salman juu ya kuhalalisha mahusiano na umbile la Kiyahudi na inazungumza kuhusu hilo. Kupitia hilo inataka kufanya makubaliano yoyote ya amani kati yake na umbile la Kiyahudi mikononi mwake, ili iweze kunufaika nayo katika uchaguzi wa Marekani na Chama cha Republican na Kundi la Trump hawatafaidika nayo, yaani, utaweza kupitia kugeuza hasara inayowezekana kuwa hatua ya nguvu mikononi mwake, ili kuitumia mbele ya ushawishi wa Kiyahudi kuuweka mbali na Trump na Republican haswa katika uchaguzi ujao.

7- Utawala wa Biden unaifanya serikali ya Netanyahu kumezea mate makubaliano ya amani na Saudi Arabia: [Balozi wa Mareka nchini Israel, Thomas Nides, alikuwa amefichua kuwa Marekani inafanya kazi kuhalalisha mahusiano kati ya Israel na Saudi Arabia, na maafisa wawili wa Marekani waliiambia tovuti ya Kimarekani ya Axios kwamba ikulu ya White House inataka kushinikiza kufikia makubaliano kati ya Riyadh na Tel Aviv ndani ya miezi sita hadi saba, kabla ya Rais Joe Biden kushughulishwa na kampeni yake ya urais (Arabi Post, 23/5/2023)] . Vyombo vya habari vya Kiyahudi pia vilimnukuu Waziri wa Mambo ya Nje wa umbile la Kiyahudi akisema, "Israel iko karibu kuliko hapo awali kufikia makubaliano ya amani na Saudi Arabia." (BBC, 22/8/2023).

8- Hata hivyo, Netanyahu anajua kutoka kwa pembe ya pili kwamba faili ya kuhalalisha mahusiano na Saudi Arabia imeambatana sana na utawala wa Biden, na kwamba hatua katika mwelekeo huu inaweza kuchukuliwa tu na utawala wa Biden, kwa hivyo Netanyahu alituma ujumbe hadi Washington mnamo 17/8/2023, ukiongozwa na waziri wake anayeaminika zaidi, Waziri wa Masuala ya Mikakati katika umbile la Kiyahudi, Ron Dermer, na alijadili na maafisa wa Marekani moja kwa moja wanaohusiana na faili ya Saudia, ambayo ni: [Mshauri wa Usalama wa Kitaifa wa White House , Jake Sullivan, mshauri wa kwanza wa Rais wa Mashariki ya Kati, Brett McGurk, na mshauri mwandamizi wa nishati wa Rais, Amos Hochstein, ambao ni Wamarekani watatu wanaosimamia juhudi za kidiplomasia zinazolenga uhalalishaji mahusiano kati ya Israel na Ufalme wa Saudi Arabia. (BBC, 22/8/2023)]. Kwa hivyo, Netanyahu anamgeukia Biden kwa ajili ya uhalalishaji mahusiano na Saudi Arabia.

9- Kisha mwishowe, kulikuwa na taarifa ya Bin Salman iliyotajwa katika swali hilo mnamo Jumatano 20/9/2023: (Mfalme Mtarajiwa wa Saudia Mohammed bin Salman alitangaza katika mahojiano na Mtandao wa Habari wa Fox wa Marekani, dondoo ambazo zilipeperushwa mnamo Jumatano, kwamba Ufalme "unafanya maendeleo" kuelekea uhalalishaji mahusiano na Israel. Mfalme Mtarajiwa wa Saudia alisema: "Kila siku tunakaribia zaidi na zaidi uhalalishaji mahusiano na Israel." Mwanamfalme Mohammed bin Salman ameongeza, akisema, "Kuna msaada kutoka kwa utawala wa Rais Biden kufikia hatua hiyo. Kwetu sisi, kadhia ya Palestina ni muhimu sana. Tunahitaji kutatua sehemu hiyo na tunayo mazungumzo yanayoendelea hadi sasa… Tunahitaji kuona tunakokwenda. Tunatumai kwamba tutafikia mahali, ambapo patayapa afueni maisha ya Wapalestina, kuifanya Israel kama mchezaji katika Mashariki ya Kati." Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya nje wa Israel Eli Cohen alisema Alhamisi kwamba mfumo wa makubaliano yaliyotangazwa na Marekani kuanzisha mahusiano kati ya Israel na Saudi Arabia yanaweza kuhitimishwa kufikia mwanzoni mwa mwaka ujao).

Nne: Ni wazi kutokana na haya yote kwamba mtawala wa Saudi Arabia, Bin Salman, hana udhibiti mkubwa juu ya mambo yake. Yeye ni kikaragosi baina ya Republican waliomleta madarakani jijini Riyadh na wapinzani wao wa Democrat. Anajibu matakwa ya hawa na wale sio kwa maslahi ya Saudia, bali kwa usaliti na utiifu watawala wa Waarabu na Waislamu  usio na mipaka, katika kuwatumikia mabwana zao. Watawala katika nchi za Waislamu wamesahau kuwa Palestina ni ardhi iliyobarikiwa, pamoja na viunga vyake.

[سُبْحَانَ الَّذِي أَسْرَى بِعَبْدِهِ لَيْلاً مِنَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ إِلَى الْمَسْجِدِ الْأَقْصَى الَّذِي بَارَكْنَا حَوْلَهُ]

“SUBHANA, Ametakasika aliye mchukua mja wake usiku mmoja kutoka Msikiti Mtukufu mpaka Msikiti wa Mbali, ambao tumevibariki vilivyo uzunguka” [Al-Isra: 1]. Ni jukumu la majeshi ya Waislamu kuhamasika kuikomboa na kuitakasa kutokana na najisi ya Mayahudi, na sio kwa Palestina kuwasilishwa kwa Mayahudi kwenye sahani ya dhahabu ya uhalalishaji mahusiano, kujisalimisha, na utumwa!

Kwa vyovyote vile, Palestina itarudi, safi na yenye baraka, kama ilivyokuwa kwa panga za majeshi ya Waislamu wakweli chini ya uongozi wa Khilafah Rashida, na Mayahudi na washirika wao watashindwa na kukimbia, na hofu itajaza nyoyo zao hadi mmoja wao ajifiche nyuma ya jiwe ambalo linamfichua zaidi ya kumficha!! Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amezungumza ukweli: «لَتُقَاتِلُنَّ الْيَهُودَ فَلَتَقْتُلُنَّهُمْ حَتَّى يَقُولَ الْحَجَرُ يَا مُسْلِمُ هَذَا يَهُودِيٌّ فَتَعَالَ فَاقْتُلْهُ» “Mtapigana na Mayahudi na mtawauwa mpaka hata jiwe litasema: ewe Muislamu Yahudi huyu hapa (amejificha nyuma yangu); basi njoo umuuwe.” Na katika riwaya nyengine «هَذَا يَهُودِيٌّ وَرَائِي» “Yahudi huyu hapa nyuma yangu.” Kwa Silsila (isnad) ile ile, Muslim ameisimulia kutoka kwa Ibn Omar. Na pengine hili litatokea hivi punde, Mwenyezi Mungu akipenda,

[وَيَقُولُونَ مَتَى هُوَ قُلْ عَسَى أَنْ يَكُونَ قَرِيباً]

“na watasema: Lini hayo? Sema: A'saa yakawa karibu! [Al-Isra: 51].

Kisha walio waliofanya uhalifu kwa kuhalalisha mahusiano yao na Mayahudi hawatapokea chochote ila aibu na adhabu kali.

[سَيُصِيبُ الَّذِينَ أَجْرَمُوا صَغَارٌ عِنْدَ اللهِ وَعَذَابٌ شَدِيدٌ بِمَا كَانُوا يَمْكُرُونَ]

“Itawafikia hao walio kosa udhalili na adhabu kali kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa sababu ya vitimbi walivyo kuwa wakivifanya.” [Al-An’am: 124].

10 Rabi ul Awwal 1445 H

25/9/2023 M

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu