Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Jibu la Swali
Harakati za Kiraia Nchini Iraq, Lebanon na Iran
(Imetafsiriwa)

Swali:

Twajua kuwa harakati maarufu nchini Iraq, Lebanon na Iran zilianza kwa ghafla kama ilivyo dhihirika mnamo 5/11/2019; je, zingali hivyo? Je, kuna dori zozote za Ulaya katika nchi hizi tatu ambako Marekani ina ushawishi? Je, hali katika nchi hizi tatu itabaki kama ilivyo, au Marekani iko katika mchakato wa kuwabadilisha vibaraka hawa au baadhi yao kupitia mabadiliko ya kawaida au kupitia jeshi kama ilivyo fanya nchini Misri na Sudan? Mwenyezi Mungu akulipe kheri.

Jibu:

Ili kuliweka wazi jibu la maswali hayo ya juu, kwa kiasi fulani tutatathmini yafuatayo:

Kwanza: Sababu na misukumo ya malalamiko hayo:

Ndio, malalamiko hayo yalianza kwa ghafla katika nchi hizo tatu, na misukumo yake kwa mukhtasari ni kama ifuatavyo:

1- Maandamano nchini Iraq: Malalamiko yalizuka nchini Iraq mapema Oktoba 2019 kwa muundo wa maandamano na kufunga njia, yaliyo imarika na kuwa ufungaji wa madaraja jijini Baghdad na barabara kuu nyinginezo kulalamika dhidi ya kudorora kwa hali ya kiuchumi ya nchi hiyo, kuenea kwa ufisadi wa kiidara na kifedha katika taasisi za serikali na dhidi ya kukithiri kwa ukosefu wa ajira. Na maandamano hayo yalianza kwa ghafla baada ya kudhikika na kuadimika kwa nyenzo za riziki kwa watu. Serikali hiyo imeshindwa kutatua kadhia ya umeme katika umri wake wote wa miaka16, wala kutoa nafasi za kazi kwa vijana na wahitimu wa vyuo, wala kushibisha njaa ya watu licha ya kuwepo rasilimali kubwa za mafuta. Maandamano haya yakalipuka kwa kuuwawa karibu watu 350, ikiwemo kujeruhiwa na kukamatwa kwa maelfu. Afisi za vyama vinavyo unga mkono serikali ya Iran zilichomwa, na kisha kuwashwa moto eneo lililomo ubalozi wa Iran mjini Karbala mnamo 4/11/2019, wakiwarushia mawe, wakitaka watolewa mjini, na kuteketeza ubalozi wa Iran mjini Najaf mnamo 27/11/2019. Kilichoifanya serikali ya Iraq kutingishika na kushtuka zaidi ni kuwa maandamano haya yamezagaa miji ya Baghdad, Nasiriyah, Karbala, Najaf na miji mingineyo ya kusini; yale maeneo ambayo yalichukuliwa na serikali hiyo kuwa yenye ushawishi mkubwa. Athari yake ilikuwa mbaya sana hadi Abdul Mahdi akashindwa kuendelea kushikilia utawala, hivyo basi akajiuzulu mnamo 30/11/2019 na bunge kuidhinisha kujiuzulu huko mnamo 1/12/2019. 

2- Maandamano ya Lebanon: Hali ya kiuchumi nchini Lebanon imefikia ukingo wa kuporomoka kabisa au inakaribia hilo! "Deni la umma la Lebanon mwanzoni mwa 2019 lilikuwa ni dolari bilioni 85.32" (Al-Arabi Al-Jadeed, 15/3/2019), na hili ni deni kubwa ambapo riba juu yake inakula takriban nusu ya mapato ya Lebanon. "Kiwango cha deni la nchi hiyo ikilinganishwa na uzalishaji jumla wa nchi ni asilimia 1.52, na riba juu ya deni hutumia takriban nusu ya mapato ya dola hiyo" (BBC 28/10/2019), na uhalifu huu mkubwa umeacha "kiwango kikubwa cha ukosefu wa ajira nchini Lebanon ukikadiriwa kuwa asilimia 37 kwa wale walio chini ya miaka 35 …" (BBC 26/10/2019). Usoni mwa maangamivu haya ya kiuchumi yaliyoletwa kwa watu na tabaka la kisiasa, cheche ya Ushuru wa WhatsApp mnamo 17/10/2019 iliwaka mabarabarani nchini Lebanon, na kuzichoma afisi hizo za manaibu hususan eneo la kusini mwa Lebanon na kuzighadhabisha Beirut, Nabatieh na Tyre, hivyo basi maandamano makubwa yakajitokeza. Na kisha kwa haraka yakaigeukia serikali kutaka ijiuzulu, na hata mabadiliko jumla ya viongozi wa kisiasa nchini Lebanon. Na kwa mawazo ya usalama ambayo dola na wafuasi wake nchini Lebanon wanayazalisha, wafuasi wa chama cha Iran walijaribu kuwatishia waandamanaji mnamo 24 na 25/10/2019 kwa kuvivamia viwanja, na kisha kurudiliwa na wafuasi wa chama cha Iran na Harakati ya Amal jijini Beirut! 

3- Maandamano ya Iran: Serikali ya Iran haina ubora wowote kuliko dola muhimu kwake – Iraq, Lebanon na Syria kabla yao – kwa kuwa inakosa mtazamo wa kiuchungaji wa kusimamia nchi hiyo ambayo imepelekea Askari wa Mapinduzi kudhibiti sekta kubwa za uchumi wa Iran na kuyatelekeza maeneo yasiyo ya Kifursi pembeni ikisababisha msururu wa miji ya mateso pambizoni mwa dola hii na hali ya kiuchumi kukaribia kulipuka katikati na pembeni hali kadhalika na ilikuwa ni aibu kwa serikali hii kujigamba kwa mradi wa nuklia na makombora kwamba maandamano hayo maarufu yamelipuka kutokana na uhaba wa gasoline! Upungufu huu umetokana na ukosefu wa viwanda vya kusafisha mafuta, na viwanda vyepesi kwa nchi zinazojali vyema watu wake. Kisha, licha ya ongezeko la matumizi ya gasoline nchini Iran kwa takriban asilimia 40 tangu 2017 na kufeli kuendesha kiwanda cha usafishaji mafuta katika mkoa wa Hormuzjan, gasoline nyingi inaingizwa kwa magendo kutoka ng'ambo kwa sababu ya tofauti ya bei ya magenge ambapo sio vigumu kwa dola hiyo kugundua, ambalo ni dhihirisho jingine la kufeli kwa dola hiyo kusimamia rasilimali muhimu zaidi "mafuta"! Dola hiyo kisha ikapandisha bei ya gasoline kwa asilimia 300, na maandamano yakazuka mnamo 15/11/2019 jijini Tehran na miji kadhaa ya Iran. Maandamano hayo yaliongezeka, ambapo mabenki yaliteketezwa moto, majumba ya Wairani, afisi za usalama na serikali zilishambuliwa, na serikali kukata mtandao wa internet ili kuzuia mawasiliano miongoni mwa waandamanaji. Serikali ikaamua kufanya ghasia za kiwango cha juu zaidi katika kukabiliana na harakati hii ya maandamano na kuikandamiza kwa chuma na moto. "Majeshi ya usalama ya Iran yalipokuwa yakiendelea na msako wao wa waandamanaji, upinzani wa Iran, mnamo 23 Novemba idadi ya vifo vya maandamano hayo ilizidi watu 300, ili nakili majina 99 kati yao, na watu zaidi ya 4,000 walijeruhiwa, na zaidi ya watu 10,000 waliwekwa kizuizini, na ilionyesha kuwa Askari wa Maandamano hayo walizitoa maiti kutoka mahospitalini hadi eneo lisilo julikana" (Arabic Independent 24/11/2019). 

Pili: Je, maandamano hayo yangali huru bila ya kuingiliwa kati na Ulaya?

Ulaya imejaribu kuyapatiliza maandamano hayo kwa manufaa yake, lakini bado haijaweza kuwa madhubiti au kuwa na ushawishi katika kuupenya ushawishi wa Marekani katika nchi hizi tatu. Ufafanuzi huu ni kama ifuatavyo:

1- Majaribio ya Ulaya nchini Iraq: Kama tulivyo taja mwanzoni, maandamano nchini Iraq, hususan maeneo ya kusini, yalikuwa yanapamba moto, yaliyo makinika katika maeneo ya Kishia, na hauwezi kuondolewa uwezekano kuwa Ulaya hususan Uingereza, imejaribu kuyatumia maandamano haya, na ingawa hakujakuwa na dalili za kuaminika za Uingereza kuyaingilia maandamano hayo, Iran ilikuwa na tahadhari kuhusu jambo hili na hata ilikuwa imepagawa nayo kiasi ya kuwa khatibu wa Ijumaa wa Tehran Muhammad Ali Mouhadi Karma, alisema wakati wa khutba, akiwataja waandamanaji wa Iraq kama "Mashia wa Kiingereza", akiongeza "Baadhi ya makundi potevu tunayoyaita kama Mashia wa Kiingereza yamepenya ndani ya safu za watu wa Iraq …" (Iran International 11/11/2019). Taarifa yake ilikuwa kwamba maafisa wa Iran wanahofia kuwa Uingereza huenda ikapatiliza fursa ya harakati hizi za watu, mbali na Iran kujaribu kuwatishia waandamanaji kwa kuwatuhumu kuwa vibaraka wa Uingereza, hususan kwa kuwa msimamo wa Uingereza ulikaribia kuwa parwanja katika kuunga mkono maandamano hayo "Ubalozi wa Uingereza ulisema katika ukurasa wake rasmi wa mtandao wa Twitter kuwa "Maandamano ya amani ni haki ya watu wa Iraq." Alioongeza: "Ghasia dhidi ya waandamanaji hazikubaliki" … "Dua zetu ni kwa waliojeruhiwa na familia za wale waliopoteza maisha yao katika maandamano hayo." (Russian agency Sputnik 5/11/2019), ambao ni msimamo ule ule ulioonyeshwa na Waziri wa Kigeni wa Uingereza Andrew Morrison kama ilivyo nukuliwa na tovuti ya habari ya Al Ain mnamo 10/27/2019. 

2- Majaribio ya Ulaya nchini Lebanon: Inajulikana kuwa wafuasi wa Marekani na Ulaya wanazunguka na kuzurura nchini Lebanon, na pia inajulikana kuwa wafuasi wa Marekani, ima moja kwa moja mithili ya Aoun na Berri au wasio moja kwa moja mithili ya Hezbollah kupitia Iran, ni upande ulio imara na wenye nguvu … Ama wafuasi wa Ulaya "Uingereza na Ufaransa" ni upande ulio dhaifu, kama vile Geagea na Jumblatt … Ama Hariri, ndiye aliye hatarini zaidi kwa sababu anatia mguu mmoja Ulaya na mguu mwengine kwa Saudi Arabia kibaraka wa Marekani, na wafuasi hawa hawawezi kutoa uamuzi, bali tu kufanya mambo yanayo ukanganya upande wa pili. Kwa mfano, mawaziri wa majeshi manne ya Lebanon mnamo 19/10/2019 walijiuzulu kutoka katika serikali ambayo waandamanaji wanataka kuiangusha, na Waziri Mkuu Saad Hariri akatangaza mnamo 18/10/2019 makataa ya masaa 72 kukabiliana na mgogoro huo, kisha akawasilisha kujiuzulu kwake mnamo 29/10/2019 dhidi ya matakwa ya kiongozi wa dola hiyo na matakwa ya chama kikuu cha usalama cha Iran nchini Lebanon. Kisha Ufaransa ikatuma mjumbe wake hadi Lebanon mkurugenzi wa Kitengo cha Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini katika Wizara ya Kigeni ya Ufaransa, Christophe Farno, "ambaye kwake – Raisi Aoun – alifikisha risala kutoka kwa Raisi wa Ufaransa Emmanuel Macron, na serikali ya Ufaransa ukithibitisha hamu ya Ufaransa katika hali nchini Lebanon na kutaka kwake kuisaidia Lebanon katika dhurufu za sasa" (Al-Arabia 11/11/2019). Ziara ya mjumbe huyo haikukubaliwa na wafuasi wa Marekani, kama Taasisi ya Kitaifa ya Habari Rasmi ilivyo mnukuu Waziri wa Kigeni Basil kuwa alimwambia mjumbe huyo wa Ufaransa: "Upande wowote wa nje usiwepo katika laini ya mgogoro wa Lebanon na kupatiliza kuutumia" … Uingereza pia ilituma mjumbe wake, Richard Moore, aliye kutana na Aoun na kusema: "Ufalme wa Uingereza daima umekuwa mshirika na msaidizi muhimu kwa Lebanon kwa muda mrefu, kwa mfano, mwaka jana uliwekeza $200 milioni ili kusaidia usalama, ustawi, ufanisi, na ubwana wa Lebanon." Aliendelea, "Ni muhimu kuendelea kuheshimu haki ya maandamano ya amani, na ukandamizaji wowote wa harakati hiyo ya maandamano kupitia ghasia au vitisho vya yeyote yule kamwe haikubaliki." (Arabic Independent 25/11/2019). 

3- Majaribio ya Ulaya nchini Iran: Serikali ya Iran, kama kawaida, ilidai kuwa inajibu njama na matishio ya nje. "Leo, kinara wa Askari wa Mapinduzi ya Kiislamu y a Iran ametishia kuiangamiza Marekani, Israel, Uingereza, na Saudi Arabia, endapo zitavuka "mistari mekundu" katika kuamiliana na nchi yake. Salami alisema, katika hotuba iliyotolewa kwa waandamanaji wanaoiunga mkono serikali jijini Tehran na kupeperushwa na runinga ya Iran: "Naiambia Marekani, Israel, familia ya Saud na Uingereza mushawahi kushuhudia nguvu yetu katika uwanja wa vita na hamukuweza kukabiliana nayo; ulimwengu sasa umeyaona baadhi ya makofi yetu." Aliendelea: "Tunawaambieni: Musivuke laini zetu, lakini mukivuka mistari mekundu, tutawaangamiza" (RT 25/11/2019). Serikali hiyo inataka kuonyesha dhana kuwa nguvu za nje ziko nyuma ya maandamano hayo na sio kutoka kwa watu wenyewe walioonja uchungu. Zingatia kuwa viashiria vyote vyaonyesha kuwa maandamano hayo ya watu yanatoka ndani ya nyoyo na damu zao wenyewe! Lakini inaonekana kana kwamba sauti ya uingiliajikati kutoka nje inaendelea kuwepo ndani ya serikali ya Iran kiasi ya kuwa khatibu wa Ijumaa wa Tehran, kama tulivyotaja mbeleni, anawatuhumu Mashia wanao andamana nchini Iraq kuwa ni Mashia wa Kiingereza! Maandamano hayo nchini Iran sio ya mwanzo, wala hayatakuwa ya mwisho na labda yako huru na hayana dalili zinazoonyesha mikono ya kimataifa. Maandamano hayo nchini Iran, kama vile Syria, ni ya watu kupigana dhidi ya watawala madhalimu ambao sera zao hazijajua ladha ya mafanikio katika kuchunga mambo ya Ummah.

Tatu: Ama kwa Marekani kubadilisha vibaraka wake katika nchi hizi tatu, jambo hili ni kama ifuatavyo:

1- Ushawishi halisi katika nchi hizi tatu ni ushawishi wa Marekani, huku Ulaya (Uingereza na Ufaransa) zikiwa hazijafaulu katika kugawanya ushawishi huu pamoja na Marekani.

2- Hadi Ummah utakapo nyanyuka kwa mapinduzi sahihi juu ya msingi wa Uislamu na kisha mabadiliko sahihi kutokea, hadi hilo litokee, watawala wa nchi hizi tatu wataendelea kuwa chini ya sera ya Kimarekani kuwabadilisha au kuwabakisha. 

3- Dola za kikoloni za kikafiri zinataka vibaraka hawa kutumikia maslahi yao. Ikiwa watu watapinga na kutakuwa na ghasia katika utawala wake, basi watampa muda maalumu; ikiwa hatawezi kuleta utulivu katika utawala, basi atakuwa ameshindwa kumtumikia bwana wake, hapo atambadilisha. Chombo cha hili ni urongo wa ile inayoitwa demokrasia kupitia kumleta kibaraka mpya asiyekuwa na sura nyeusi zaidi kuliko yule kibaraka aliyefurushwa; yaani, hii ni endapo mgogoro hautakuwa sugu, lakini endapo utakuwa sugu chombo kitakuwa ni "jeshi" kama ilivyofanya nchini Misri 2011 au Sudan 2019. 

Nne: Kutathmini mabadiliko tarajiwa katika nchi hizi tatu kwa mujibu wa uhalisia wa sasa, yafuatayo ndio yaliyo dhahiri:

1- Kuhusiana na Iran: Marekani inatangaza waziwazi kuwa haitaki kubadilisha serikali nchini Iran; yaani, kadri mauwaji yatakavyokuwa katika maadamano hayo, Marekani inaamini kuwa serikali hii ingali inatumikia maslahi yake! Katika wakati ambapo damu ya Waislamu nchini Iran ilimwagwa na serikali hiyo, maafisa wa Marekani walikuwa wakisisitiza juu ya kudumishwa utulivu "afisa mkuu wa ikulu ya White House alisema Jumapili kuwa nchi yake haitaki kubadilisha serikali nchini Iran…" (Al Arabiya Net Jumapili, 11/17/2019); hivyo basi, hakuna mabadiliko yanayo tarajiwa katika serikali ya Iran kutokana na maandamano hayo ya 11/2019 kama vile ambavyo hakukuwa na mabadiliko kutokana maandamano ya mwaka jana. 

2- Kuhusiana na Lebanon: Kama tulivyo taja, Lebanon ina wafuasi wa Marekani na wafuasi wa Ulaya, timu ya kwanza ndio yenye nguvu zaidi na hii ndio inayoendesha hali ya madhaifu kwa mujibu wa njia ya maridhiano, na pande hizo mbili zinatofautiana juu ya serikali ya kiufundi na kisiasa au serikali ya kitaalamu! Baada ya yote haya, inatarajiwa kuwa Marekani itabadilisha mizani ya serikali nchini Lebanon, ili ushawishi uwe kwa wafuasi wa Marekani na kuwahusisha wafuasi wa Ulaya lakini kwa kiasi fulani, kisha kuzihusisha barabara ili kuzituliza.

3- Kuhusiana na Iraq: Marekani inaitawala Iraq karibia moja kwa moja nyuma ya pazia. Ubalozi wake jijini Baghdad una wafanyikazi 16,000, wanao fuatilia kazi ya mawaziri wote wa Iraq, hususan sekta za mafuta na usalama, na ndio ubalozi mkubwa zaidi wa Marekani duniani. Ina kambi nyingi za kijeshi nchini Iraq, maarufu zaidi katika hizo ni kambi ya Ain al-Assad mjini Anbar. Katika wiki ya mwisho ya mwezi uliopita, Marekani ilizidisha ujumbe wake, hivyo ziara ya ghafla ya Makamu wa Raisi wa Marekani Pence mnamo 23/11/2019 katika kambi ya Ain al-Assad, na kabla ya wiki kumalizika ya ziara ya Makamu wa Raisi wa Marekani nchini Iraq, Marekani ilimtuma kamanda wa Muungano wa Wakuu wa Kijeshi wa Jeshi la Marekani Mark Milley hadi Baghdad mnamo 27/11/2019. Hii ni dalili ya kudumu kwa ufuatiliaji wa Marekani hususan kwa kuwa Iraq ni kesi tete kwa Marekani; iliivamia na kudai kuwa inaishika mkono katika maendeleo lakini ikaipeleka katika ghasia na maangamivu, na sasa iko katika msururu wa migogoro na inatarajiwa kuwa endapo hali hazitakuwa shwari karibuni Marekani italeta mabadiliko kupitia "jeshi" na kuzihusisha barabara pamoja nao katika kutawala kama ilivyo fanya nchini Misri au Sudan. Imeoneka kuwa vyombo vya Kupambana na Ugaidi nchini Iraq, ambalo ni jeshi kubwa lililo undwa na Wamarekani na kupewa zana bora zaidi za kijeshi; viko mbali sana na sera ya kuyazima maandamano hayo, na inaonekana kuwa waandamanaji katika Uwanja wa Tahrir wanalitazama jeshi hili kama mkombozi wao kutokana na wanasiasa wafisadi kwani wanabeba picha ya Jenerali Abdel-Wahab Al-Saadi, mmoja wa viongozi wa taasisi hiyo baada ya kufutwa kazi na Abdel-Mahdi kana kwamba jeshi hili linakubaliwa na waandamanaji hao kuwa na dori ya kupangilia suluhisho. Hii ni upande mmoja, huku upande mwengine, mikutano ya kijeshi iliyo fanywa na Marekani jijini Baghdad, na kupeleka wajumbe wake kwa ajili ya hilo ikiongezewa na kazi ya ubalozi wake mkubwa jijini Baghdad, yote haya ni matayarisho ambayo Marekani inayatayarisha pindi yatakapo hitajika. 

Hili halitaathiriwa na kujiuzulu kwa Abdel-Mahdi na kuteuliwa kwa raisi mpya, kwani hili halitatui tatizo hilo, bali ni la muda tu, ikiwa na maana kuwa kidonda kitabakia wazi hadi kipone!

Lakini, harakazi kubwa katika nchi hizi tatu zina nukta za kuungwa mkono na nukta za kupingwa. Ama nukta za kuungwa mkono kwake ni kuwa harakati hizi ziko huru, na kwa kiasi kikubwa zingali huru. Ama nukta zinazo pinga dhidi yake ni kuwa bado hazijachukua uongozi wenye ikhlasi kwa Mwenyezi Mungu Subhanahu, na ikhlasi kwa Mtume Wake, rehma na amani zimshukie na jamaa zake, ili kuangaza njia yake kwa utawala wa Uislamu, Khilafah Rashida ya kweli. Na endapo harakati hizi zitaendelea pasina uongozi wenye ikhlasi na hivyo kuendelea pasi na uongofu, basi juhudi na kujitolea kwake zitaambulia patupu, na harakati hiyo hatimaye itakuwa mithili ya yule aliye geuza mwelekeo wake baada ya kuwa na nguvu! Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kuongoza katika njia sahihi.

7 Rabii’ II 1441 H
Jumatano, 04/12/2019 M

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoAlhamisi, 02 Aprili 2020 20:45

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu