Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Jibu la Swali

Ni Upi Uhalisia wa Mzozo wa Kimataifa na Ushawishi wake ndani ya Algeria?

(Imetafsiriwa)

Swali:

Katika nchi ambayo watu wake wameubeba Uislamu, nchi ya mashahidi milioni moja kwa kupigana jihad dhidi ya uvamizi wa Ufaransa uliokuwepo kwa miaka 132, ndani ya nchi maandamano yaliyoungwa mkono na wengi yalianza, yakivunja vizuizi vya hofu kwa madhalimu wa Algeria tangu 22/2/2019 mpaka wa leo, lakini hawalinganii Uislamu! Ni zipi sababu za hilo? Ni upi uhalisia wa mzozo wa kimataifa na ushawishi wake ndani ya Algeria? Je una dori katika yale yanayotokea? Na kutarajiwe nini hususan kuhusiana na uchaguzi?

Jibu:

Ili kupata jibu kwa maswali hayo, tunatathmini yafuatayo:

Kwanza: Sababu ya kutolingania Uislamu katika harakati:

1- Naam, Algeria ni nchi ya Uislamu sahihi na hilo lilithibitishwa pale ambapo dola ilipotoa nafasi ya uchaguzi huru na wa haki mwanzoni mwa miaka ya 1990. Natija yake ilikuwa ni kutokana na ulinganizi mkubwa wa kutaka kuhukumiwa na Sheria za Mwenyezi Mungu ambao ulibebwa na mamilioni katika barabara za Algeria. Ulaya ilikasirika na Ufaransa kutishia kuingilia kati kijeshi. Ulaya na Ufaransa iliwasukuma watawala wa Algeria mwanzoni mwa 1992 kupinga matokeo ya uchaguzi wa 1991, kisha jeshi likaingilia kati na kutangaza udhibiti wake juu ya nchi. Uungwaji mkono mkubwa kwa watawala ulitoka kwa miji ya kiza, "Paris," ambayo kiurongo inaitwa miji ya nuru. Ujasusi wa Ufaransa kwa ushirikiano na taasisi za usalama za eneo zilichochea cheche za mauaji ya kidhalimu ambayo yalianzisha zama za mauaji ya miaka 1990 ambayo yaliua mamia ya maelfu ya Waislamu ndani ya Algeria. Kisha pasina aibu au fedheha, utawala wa Algeria na nyuma yake Ufaransa na Uingereza ikayanasibisha mauaji hayo na Waislamu wanaolingania Shari'ah ya Kiislamu. Janga hilo lilienea na utawala ukanasibisha kila tone la damu na mauaji hayo na Waislamu wanaolingania Shari'ah ya Kiislamu. Kipindi hicho kilichukua takribani miaka kumi na kuitwa "Muongo Mweusi" na utawala ulianza kueneza hofu katika akili za watu kutolingania Uislamu na kwamba yeyote anayelingania Uislamu uwe ndio unaohukumu anataka kurudisha miongo mieusi! Vyombo vya habari vya Kifaransa vililingania mwito huo wa kuogofya na hofu ya Uislamu ikawateka wanasiasa wengi ndani ya Paris. Uoga wa Ufaransa na Uingereza na kutekwa na harakati za Algeria lau zingelingania Uislamu zimehama mara moja kwa utawala wa Algeria: "Pande husika zilizo karibu na kikundi kilicho na maamuzi ndani ya nchi kimepigia debe kwamba Waislamu wanaolingania Shari'ah ya Kiislamu 'watakwenda kinyume na masekula na kuwa na mpango wa dola ya Kiislamu ambayo itajengwa juu ya magofu ya masekula na labda hata miili yao ikihitajika" (The Independent 21/3/2019). Hivyo basi, utawala unawapa onyo watu mara moja kuhusu "sanamu la Uislamu wa siasa kali" ambao uko tayari kumwaga damu! Licha ya kwamba ni utawala ndio unaowafuatilia Waislamu na kumwaga damu. "Vikosi vya usalama vya Algeria vilimshambulia muasi maarufu na mmoja wa waanzilishi wa Islamic Salvation Front, Ali Belhadj na kumburuza katika barabara" (Arabic 21, 23/2/2019) katika siku ya pili ya kuanza kwa maandamano ya Algeria…!

2- Hili ni pamoja na vita vya Amerika dhidi ya Uislamu ambavyo vimechukua kichwa kipana cha "Ugaidi wa Kiislamu" ambapo mukhlisina katika ulimwengu wa Kiislamu na harakati, miungano na watu maarufu wamelengwa na kutengwa kwa ugaidi na kuzifanya alama za Kiislamu ni uhalifu kama vile mabango na wale wanaojifunga na dalili za Kiislamu kuwa ni wenye misimamo mikali na magaidi n.k. Yote haya yanaweka kivuli juu ya ulinganizi wa harakati maarufu ndani ya Algeria.

3- Moja ya sababu ya zilizopelekea kutochipuza kwa madai ya Kiislamu katika harakati za Algeria ni yale yaliyoganda katika akili za watu kuhusu baadhi ya harakati zilizo na sifa za Uislamu ambazo zinaitwa "poa". Wameziona baadhi ya wakati zinajiita harakati za upinzani na mara nyingine zikishiriki katika serikali na kufurahia vyeo vya uwaziri na ubunge. Kushiriki kwao huku kuliwaathiri watu wengi na hususan wale ambao walikuwa wanaziamini harakati hizi kuwa zinafanyakazi ya Uislamu na kisha kuziona zinafanya kazi na utawala. Pasina kutaja hukmu za Kishari'ah ambazo hawakujifunga nazo za kuharamishwa kwa sheria zilizotungwa na mwanadamu ndani ya mabunge na kuharamishwa kwa kushiriki katika tawala ambazo hazitokamani na Uislamu kwa sura yoyote ile. Hili limepelekea kwa kundi kubwa la Waalgeria kutotaja Uislamu ndani ya harakati hizo.

4- Mwisho kabisa, mzozo wa kimataifa ndani ya Algeria ili kutia ushawishi na majaribio ya kukata tamaa ya Wamagharibi hususan Ufaransa  ili kueneza thaqafa ya kisekula na kuangazia uongozi ambao ni wafuasi wao katika harakati ambazo kwa uhakika ni za kisekula na kufaulisha hilo kupitia ushawishi wao wa kisiasa ndani ya Algeria. Tukizingatia kwamba pande husika katika mzozo wa kimataifa ndani ya Algeria unakubaliana kwa ukamilifu kuhusu kuangamiza utambulisho wa Kiislamu ndani ya Algeria na kuangazia sifa za kisekula za dola.

Hizo ni baadhi ya sababu za kina ambazo zimepelekea kuchipuza kwa sifa za usekula katika harakati maarufu ndani ya Algeria; ambazo nyuma yake ni uhadaifu, upotoshaji na chuki za kisiasa za Wamagharibi na vibaraka wao. Na lau inadhaniwa watafaulu katika kuzuia kuchipuza kwa harakati ya Kiislamu, Uislamu umemakinika katika moyo wa Algeria kwa mashahidi milioni moja na kuchipuza kwake hakutocheleweshwa, na kwa Idhini ya Mwenyezi Mungu. Na kesho inakaribia,

{إِنَّ اللَّهَ بَالِغُ أَمْرِهِ قَدْ جَعَلَ اللَّهُ لِكُلِّ شَيْءٍ قَدْراً} “Hakika Mwenyezi Mungu anatimiza amri yake. Mwenyezi Mungu kajaalia kila kitu na kipimo chake.” [At-Talaq: 3].”

 Pili: Ama kuhusu mzozo wa kimataifa ndani ya Algeria:

1. Kwa Uingereza na Ufaransa:

a- Tangu mapinduzi ya Boumediene mnamo 1965, ushawishi wa Uingereza uko juu ndani ya Algeria huku Ufaransa nayo ikiwa na baadhi ya nguvu. Lakini baada ya kufutwa kazi kibaraka wa Kifaransa Khaled Nizar kutoka katika Wizara ya Ulinzi mnamo 1993, ushawishi wa Ufaransa ulidhoofika polepole ndani ya jeshi mpaka ukafikia hatua ya kutegemea "thaqafa ya kijeshi" badala ya utiifu wa kisiasa. Bouteflika anajulikana kwa utiifu wake kwa Uingereza katika kipindi cha utawala wake tangu 1999 na amekuwa akitibu kujitanua kwa Ufaransa polepole pasina kuleta gumzo.  Suala la kusitisha ushawishi wa Ufaransa kutoka katika muundo wa dola ulikaribia kuwa mashindano ya riadha; kwani hakukuonekana ishara za kutokwa na jasho kutoka pande husika katika suala la ushawishi ambalo lilichukuwa sura ya mashindano. Lakini Bouteflika alipomfuta mkurugenzi wa Huduma ya Kijasusi, Mohammad Median anayejulikana kama Jenerali Tawfeeq mnamo 13/9/2015 lilikuwa ni pigo chungu kwa ushawishi wa Ufaransa ndani ya Algeria ambayo ilikuwa imefurushwa katika jeshi na kuendelea kutegemea ujasusi kama sehemu pekee ya nusu ya usalama kama ushawishi wa Ufaransa ndani ya Algeria. Pigo hilo chungu liliwasha moto chini ya majivu ya utulivu wa mahusiano baina ya washawishi wawili wa Algeria.

b- Kumekuwepo na hali mbili zilizopelekea ushindani baina ya ushawishi wa Uingereza na Ufaransa ndani ya Algeria kutoka kuwa ni wa ushindani wa kiriadha na hivyo mzozo baina yao ulikaribia kuwa "wakusokotana mikono" licha ya kwamba haikupelekea "kuvunjika kwa mfupa". Hali mbili hizi ambazo zimeyafanya mashindano baina ya nchi mbili kuwa moto ni:

Ya kwanza: kura ya maoni ya Uingereza kutoka Ulaya mnamo 2016 imepanua mzozo baina ya Uingereza na Ufaransa na hili lilidhihirishwa na ukazanishaji wa Ufaransa, Umoja wa Ulaya (EU) katika mazungumzo yake na Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May ambayo yalidhihirishwa katika mipango ya Waziri Mkuu mpya, Johnson ya kuondoka EU pasina makubaliano na haya ni madhara makubwa kwa Ufaransa. Kutokubaliana huko pia kulichipuza kuhusiana na suala la Amerika kusababisha janga na Iran baada ya kujitoa kutoka katika mpango wa nuklia. Ilhali Ufaransa ilikuwa imechukua mtazamo tofauti na Amerika nayo Uingereza ilikuwa inauunga mkono na tofauti zao ziliendelea kupanuka. Tofauti hizi mpya baina ya Uingereza na Ufaransa zinadhihirishwa na misimamo yao katika maeneo mengine kama Algeria.

Ya pili: kuanza kwa maandamano ndani ya Algeria mnamo 22/2/2019. Ufaransa iliona kwamba kukosekana kwa umakinifu ndani ya Algeria na kusukwasukwa kwa nguzo za ushawishi wa Uingereza ndani ya Algeria kuwa ni fursa ya kuurudisha ushawishi wake mkubwa ndani ya Algeria; kwa hiyo kuchipuza kwa harakati maarufu kumeufichua moto uliofichika wa Ufaransa tangu 2015!

c- Natija yake ni hali ya mashindano baina yao ambayo yamevuka na kuwa katika ngazi ya "kusokotana mikono". Huduma za usalama zimefichua mipango sawia ya mapinduzi ya kijeshi ili kumuondosha Qaid Saleh [Gaid Salah] kutokuwa mkuu wa majeshi kwa hiyo vikosi vya usalama viliwashika wanaume wenye nguvu na hatari wa Ufaransa kama Mohamed Median (Jenerali Tawfiq) na Bashir Tartak wakurugenzi wa zamani wa huduma za ujasusi ambao walishikwa mnamo 5/5/2019. Kisha kushikwa kwa kiongozi wa Chama cha Labour Louisa Hanoune, mnamo Mei 5, 2019 na kuongezea na Said Bouteflika ambaye anaonekana kuwa wanaume wa Ufaransa ndani ya Algeria wamemvuta upande wao hususan baada ya kujiuzulu kwa kakake, Rais Bouteflika na walishtakiwa; "mahakama ya Kijeshi ya Algeria ndani ya Blida iliwahukumu washtakiwa wanne kwa shutuma za kupanga njama dhidi ya jeshi na mamlaka ya serikali kwa kifungo cha miaka 15 gerezani. Hukumu hizo zilizotolewa mbele ya Said Bouteflika, Louisa Hanoune kiongozi wa Chama cha Labour na Luteni Jenerali mstaafu Mohamed Medine. Mahakama ya kijeshi ndani ya Blida pia ilimuhukumu pasina kuwepo mahakamani Waziri wa Ulinzi wa zamani Khaled Nizar kifungo cha miaka 20 gerezani” (Sky News Arabic 25/9/2019). Ufaransa imepinga dhidi ya uongozi wa kijeshi ndani ya Algeria kwa sababu ya kushikwa huko. Kwa mujibu wa Gazeti la Uingereza la Independent mnamo 18/5/2019, wakati aliposhikwa Louisa Hanoune, Wafaransa 1000 wakijumuisha Waziri Mkuu wa zamani Jean-Marc Ayrault walitia saini mpango wa kumtaka awachiliwe. Gazeti liliongeza "naibu wa chama cha republican katika bunge la Ufaransa, Jean LaSalle alihofia athari ya matukio juu ya maslahi ya nchi yake" na kusema "Kunyanyuka kwa kizazi kipya cha maafisa na majenerali katika jeshi la Algeria lililo na muundo na mpangilio wa kitaifa unatishia maslahi ya Ufaransa ndani ya Algeria hususan katika mitizamo ya kithaqafa, kiuchumi na kisiasa." Hii ni ishara ya kuudhika kwa Ufaransa inayomaanisha kuwa mzozo huu unachuku mkondo wa joto licha ya hivyo Uingereza bado iko juu ndani ya utawala na ikiungwa mkono na mkuu wa majeshi.

2 – Majaribio ya Amerika kujipenyeza ndani ya uga wa Algeria:

Vyombo vya habari vya Amerika vimejaribu kuwapigia debe baadhi ya watu waliochipuza katika harakati maarufu kama vile Karim Tabbou, katibu wa zamani wa Socialist Forces Front. Chaneli ya Alhurra, American TV ilimzungumzia mnamo 12/9/2019 kama ("sura maarufu katika harakati zenye umaarufu" na kuzipigia debe video za Karim Tabbou "akiongoza maandamano ndani ya mji wa Algeria kama sehemu ya harakati zenye umaarufu" na kupigia debe "upinzani wa kweli dhidi ya uongozi, sio kama vyama vyengine"). Hili labda linaashiria kuwepo kwa mawasiliano ya Amerika na wanaharakati kama hao na wengine ndani ya harakati maarufu ndani ya Algeria. Huduma za usalama za Algeria zimemshika mwanaharakai huyu na wengine na kuwashitaki kwa "kudhoofisha hamasa ya jeshi." Kwa kuchukulia uwepo wa mawasiliano ya Amerika na ishara za harakati maarufu ndani ya Algeria, na hili linatarajiwa kwa hiyo watu aina hiyo bado hawajafikia uwezo wa kushawishi maisha ya kisiasa ndani ya Algeria kwa malengo ya Amerika na kwamba haijaweza kujipenyeza katika ushawishi wa kijeshi na taasisi za kiserikali kwa sasa.

Katika yote haya, uga wa Algeria unakaribia kuwa hauna mzozo wa Ulaya na Amerika, bali ni mzozo baina ya Uingereza na Ufaransa ukikaribia jaribio la Uingereza na nidhamu yake ya kijeshi kuikata mbawa Ufaransa ndani ya uga huo. Majaribio ya Amerika hayakufaulu katika kujipenyeza katika dori ya Ulaya ndani ya Algeria licha ya kwamba kundi linalotawala ndani ya Algeria linahofia kuendelea kwa mzozo huo – harakati maarufu – inaweza kuiwezesha Amerika kufaulu ambako imekuwa inakutafuta kwa miaka, lakini kwa Ufaransa inaweza kutumia muda huo mrefu wa harakati ili kumakinisha wafuasi wake na kuwapa nafasi wao.

Tatu, ama kuhusu yanayotarajiwa kutokamana na uchaguzi, yanaweza kufahamika kama ifuatavyo:

1- Uingereza na wale walioko madarakani na uongozi wa jeshi wameweza kuwatenga wanaume wa Ufaransa pakubwa kutoka katika muundo wa serikali, kwa hiyo nidhamu hii inaharakisha uchaguzi ili isiweze kubadilisha hali zilizopo hususan harakati zinazoendelea, Qaid Saleh alisema: "kabla ya sasa tulikuwa tunazungumza kuhusu umuhimu wa kuharakisha uchaguzi wa urais. Leo, tunauhakika kwamba uchaguzi huu utafanyika ndani ya muda uliotengewa." (Independent 14/9/2019) pamoja na ombi lake la kuwepo kwa msimamo wa wazi kama (kutangaza kwamba muda uliopo sasa unahitaji msimamo wa wazi "Hakuna nafasi ya kushika bakora kuanzia katikati… Ima uwe na Algeria au maadui wake" (The Independent 14/9/2019). Hii ni ishara kwamba mrengo wa nidhamu ya utawala unaoegemea Uingereza unaharakisha uchaguzi ili kulisuluhisha leo kwa sababu mambo yanaonekana kuwaegemea wao. Ufaransa na vikosi vinavyoiunga mkono wanapinga kutekelezwa kwa uchaguzi huo au wanapendekeza kuuhairisha mpaka pale hali itakapokuwa upande wao lakini hawatoi kauli mbele ya umma kuhusu hilo bali wanasema kidiplomasia kwamba uamuzi upo katika watu wa Algeria kuhusiana na masuala ya nchi yao!

2- Nidhamu ya serikali inajaribu kuwasukuma wagombea kutoka katika wafuasi wake ili kugombania uchaguzi wa urais baada ya kubadilisha rangi zao "mawaziri wa zamani Ali Benflis na Abdelmajid Tebboun walitangaza mnamo Alhamisi ugombeaji wao katika uchaguzi wa urais wa 12 Disemba” (Reuters 28/9/2019). Hawa na mfano wao ni sura za kutegemewa na nidhamu ya serikali na baadhi yao wanacheza dori ya upinzani. Ali Benflis, kiongozi wa chama cha National Liberation Front kinajiwasilisha kama chama cha kisiasa na kulingania mabadiliko. Kiongozi wake, Benflis alikuwa kiongozi wa serikali wa Bouteflika baina ya 2000 na 2003, ikimaanisha kuwa nidhamu hii inataka kuurudisha utawala ukiwa na sura mpya kidogo ikipendekeza kwamba watu wa Algeria wakubali uhadaifu na harakati (Hirak) ziishe!

3- Lakini, liko wazi kuwa harakati maarufu kwa upana wake zinazopinga uchaguzi chini ya utawala uliopo zina nguvu zaidi kuliko zile zinazounga mkono utawala au vile vinavyojiita vyama vya kisiasa ambavyo vinaunga mkono uchaguzi na hili linaifanya nchi kuelekea katika hali mbili zifuatazo:

- Ima utawala uliopo utalazimishwa kuhairisha uchaguzi katika dakika za mwisho kama ilivyokuwa tarehe ya uchaguzi ya 18/4/2019 na ulihairishwa.

- Au kutakuwa na uchaguzi ambao haukukamilika, hivyo basi harakati maarufu zitaendelea lau kama ambaye uchaguzi haukufanyika hata kama baadhi ya vikosi vitasusia harakati maarufu lakini hali zitakuwa nzuri kwa kuwepo kwa vurugu ili Mamlaka yaweze kusitisha harakati hizo baada ya kusema kwamba rais halali ashachaguliwa na kwamba maamuzi yake lazima yahishimiwe! Hivyo basi, mambo yanaendelea kuwa ya mshikemshike baina ya toa na uchukuwe!!

4- Hivyo basi, harakati zilizopo hazitoleta mabadiliko ya kweli au ufufuaji ulio na ufanisi kwa sababu harakati hizi licha ya kuchipuza kimaumbile lakini uingiliaji kati wa Uingereza na Ufaransa ndani yake na makundi na wafuasi wanafanya harakati hizo kukosa ukamilifu hususan baada ya kuweka wazi mpangilio wa uongozi wa jeshi pamoja na utawala bali ni sehemu yake inayoipa maagizo na kuikataza. Hili linamaanisha kwamba mabadiliko yanaweza kupatikana tu ndani ya Algeria kwa kubadilisha utiifu wa jeshi kuwa ni Uislamu wa watu hawa sahihi. Hili linawezekana na kufaulu baada ya kuwaondosha majenerali wa juu, vibaraka wa Uingereza na Magharibi na kuwawezesha kundi la maafisa mukhilisina kuchukua udhibiti wa mambo ndani ya jeshi na kisha kunusuru mabadiliko ya kweli ambayo Ummah unayataka kwa msingi wa Uislamu. Hili halimaanishi kuwa jeshi lishikilie serikali bali wawe watu wanaoinusuru kwa Ukweli ili uongozi wa kweli ambao Ummah unausubiri uweze kuleta mageuzi ya kina kwa kurudisha maisha ya Kiislamu na kusimamisha Khilafah Rashidah ya kweli ambayo itaufufua Ummah na kuifufua mimea na ziwa na turudi kupitia hiyo kama Mwenyezi Mungu alivyotutaka tuwe.

{كُنْتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنْكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ}...“Nyinyi mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu.” [Al-i-Imran: 110]


{وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * نَصْرِ اللَّهِ يَنْصُرُ مَنْ يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ} “Na siku hiyo waumini watafurahi. Humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye Kurehemu.” [Ar-Rum: 4-5].

4 Safar 1441 AH
Alhamisi, 03/10/2019 M

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoAlhamisi, 02 Aprili 2020 20:47

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu