Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  4 Ramadan 1442 Na: 1442 H / 031
M.  Ijumaa, 16 Aprili 2021

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mashababu wa Hizb ut-Tahrir Wanabeba Mwenge wa Taa, na Mamlaka nchini Urusi zinawadhulumu na Kuwatesa

Tabia Hii Inatukumbusha Nidhamu ya Ufashisti na Unazi!

(Imetafsiriwa)

Tangu mwanzo wa mwaka 2021 M, maelezo yote ya mateso ya kikatili yaliyofanyika ndani ya vyumba vya chini vya "Huduma ya Adhabu ya Shirikisho" (FSIN) nchini Urusi yamefichuka mbele ya rai jumla. Gazeta la Novaya lilichapishwa mnamo 23/02/2021 M rekodi za video za mateso; Ilijumuisha video ya wafungwa wawili katika gereza la Yaroslavl mnamo 2017, mmoja wao alikuwa Muislamu na mwingine Mkristo.

Katika moja ya video, mfungwa anaonyeshwa akilazimishwa kuwa uchi kabisa, kulala chini, na kupanua miguu yake, huku idadi kubwa ya maafisa wa polisi wanamtazama. Miongoni mwa wale waliokuwa karibu naye alikuwa polisi (mwanamke!) Akiwa amebeba kifaa kinachojulikana kama "kipanuzi cha tupu ya nyuma" mkononi mwake ili kukitumia kwake. Wakati mfungwa alipokataa kitendo hiki kibaya, walimtupa juu ya meza kwa nguvu na kwa pamoja wakamtandika kwa fimbo kinyama. Waandishi wa habari wanasema mfungwa huyu ana uwezekano mkubwa alikufa hospitalini kutokana na kuvuja damu ndani.

Video nyingine inaonyesha polisi wapatao 15 wakibadilishana zamu katika kumpiga kikatili mmoja wa wafungwa wa Kiislamu, baada ya muda wake wa kifungo kumalizika wakati anakaribia kutoka gerezani, na inaonyesha wazi jinsi kila mmoja wao alikuwa akitokwa na jasho huku akihema kutokana na nguvu ya juhudi waliyoifanya katika kumpiga mfungwa huyo masikini. Ilibainika kuwa sababu ya kuteswa kwa mfungwa huyo ni kuwa alionyesha kukasirishwa kwake na tabia ya wafanyikazi wa gereza baada ya kutupa vitu vyake vya kibinafsi chini, ambavyo vilijumuisha nakala ya Quran Tukufu. Kwa bahati nzuri, alibaki hai baada ya mateso haya, lakini alibaki hospitalini kwa wiki mbili baada ya kuachiliwa.

Pia kati ya maelezo ambayo yamejulikana juu ya mateso ya kikatili ya wafungwa katika "Huduma ya Shirikisho la Adhabu" nchini Urusi, wanawatesa wafungwa kwa kutumia wafungwa wengine wanaoshirikiana na wakuu wa magereza, ambao wanawaita "wanaharakati". Mradi wa (Gulagu.net) wa haki za binadamu ulichapisha ukweli ulioandikwa kuhusu mateso na ubakaji katika gereza la Irkutsk, ambapo "wanaharakati" walitoa ungamo kutoka kwa wafungwa wengine kwa ombi la wafanyikazi wa huduma za usalama.

Hatutaorodhesha hapa ukweli wote juu ya ukatili wa mateso ambayo wafungwa wanakabiliwa katika vyumba vya chini vya Huduma ya Shirikisho la Adhabu nchini Urusi, ambayo nilitaja (Gulagu.net). Tutataja tu kile ambacho mkuu wa chombo "Shirikisho la Huduma ya Adhabu" nchini Urusi Alexander Kalashnikov alichokisema katika mkutano wa Tume ya Shirikisho mnamo 25 Februari 2021M juu ya matokeo ya uchunguzi katika idara yake katika mkoa wa Irkutsk. Watu arobaini na moja waliohusishwa na mateso wametambuliwa kutoka kwa wafungwa. Watu 47 walitambuliwa kama wahanga wa vitendo vya wabakaji. Imethibitishwa pia rasmi kwamba watatu kati ya wale waliowabaka wafungwa wanaugua maradhi ya upungufu wa kinga mwilini "UKIMWI".

Hatujui historia ya kidini ya wafungwa ambao waliteswa katika vituo vya Huduma ya Adhabu ya Shirikisho ya Urusi huko Irkutsk, lakini ukweli huu juu ya unyama katika kuamiliana na wafungwa nchini Urusi umechapishwa tangu mwanzo wa mwaka huu tu, na hutoa sura ya juu ya hali ya kazi ya vituo vya utekelezaji adhabu kote nchini Urusi. Na ikiwa tunajua kwamba Waislamu nchini Urusi wanahukumiwa bila ya msingi wa kisheria na kuwekwa katika magereza ya faragha chini ya dhurufu ngumu, hii inatoa taswira ya hali wanazokabiliana nazo Waislamu waliokamatwa kwa mashtaka ya uongo kama vile ugaidi na misimamo mikali. Hii ni kwa kuongezea kupitia mateso kwa wafungwa wa Kiislamu kwa kuwalaza njaa, ambapo wanapewa nyama ya nguruwe pekee kula.

Kituo cha Kumbukumbu cha Kutetea Haki za Binadamu kimechapisha kwenye wavuti wake ripoti ambayo inajumuisha orodha ya wafungwa 297 wa kisiasa, na ripoti hiyo ilisema kuwa majina kwenye orodha hiyo ni majina ya Waislamu peke yao. Aliongeza kuwa wafungwa wengi walikuwa wanachama wa Chama cha Kiislamu cha Hizb ut Tahrir (wafungwa 191), pamoja na Waislamu wengine, kama vile wa Jumuiya ya Tabligh, wafuasi wa Saeed Norsi. Ripoti hiyo inathibitisha kuwa orodha hii haijakamilika. Majina yaliyotajwa ni majina tu ya wale ambao kesi zao ziko katika uchunguzi. Na kwamba idadi ya watu wanaoteswa waliofikiwa na Kituo cha Kumbukumbu kwa uchache ni mara tatu au nne zaidi, lakini majina yao hayakutajwa katika orodha hii ama kwa sababu habari zinazohitajika juu yao hazikufika, au bado haijakamilika. Kituo kinasema kuwa hizi ni nambari tu ambazo kituo hicho kiliweza kugundua.

Ripoti hiyo inathibitisha kwamba miaka kadhaa iliyopita, wale wanaodaiwa kujihusisha na Hizb ut Tahrir waliainishwa nchini Urusi kama shirika (la kigaidi) bila msingi wa kisheria wa uainishaji huu, na mashtaka yaliletwa dhidi yao kwa kisingizio kwamba walikuwa ni (shirika la kigaidi). Tuhma hii ilielekezwa dhidi yao chini ya kifungu cha Kanuni ya Jinai ya Urusi, ambayo ina adhabu ya hadi miaka 3 gerezani, kwa kisingizio cha kushiriki katika shughuli za mashirika yenye msimamo mkali.

Ripoti hiyo inaendelea kwamba pamoja na kuimarishwa kwa sheria, ikiongezewa na tabia inayofuatwa katika utekelezwaji wa sheria, mashtaka huletwa leo chini ya kifungu kipya cha sheria kinachoitwa "kuratibu shughuli za shirika la kigaidi na kushiriki katika shughuli za shirika hili" ambayo yanaelezea adhabu ambayo inaweza kufikia kifungo cha maisha. Vifungo vya jela vilivyowekwa na mahakama pia vimeongeza hadi miaka 24 gerezani.

Inajulikana kuwa sheria zinatofautiana kutoka nchi moja hadi nyingine na kati ya sheria moja na nyingine, lakini mashtaka ya uongo hayatofautiani kati ya sheria na kanuni na kati ya watu, kwa hivyo kuelezea kitu dhidi yakekunapingana na mawazo ya akili. Vivyo hivyo, mashtaka ya Hizb ut Tahrir kwamba inajihusisha na vitendo vya kigaidi ni kuupindua ukweli chini juu. Hizb ut Tahrir, inashuhudiwa na wa mbali na wa karibu, kwamba imetabanni njia ya ulinganizi iliyojengwa juu ya fikra, hoja na ushahidi, na haikujiruhusia yenyewe au wanachama wake kuachana na njia hii. Na kazi zake za kisiasa, kithaqafa na kifikra baina ya watu wa ulimwengu zinashuhudia hilo. Licha ya ukweli huu, mashababu wa Hizb ut Tahrir bado wanahukumiwa kwa kadhia zisizo na msingi na mashtaka ya uongo.

Pamoja na mkazo wa sheria, ukamataji mkubwa kwa mashababu wa Hizb ut Tahrir umefanyika huko Tatarstan, Bashkortostan, Moscow, Petersburg, Chelyabinsk, Tumen na miji mingine. Baada ya uvamizi wa Crimea, jambo hilo limewafikia Waislamu huko. Lakini, vyombo vya usalama sio tu vimezuia kazi ya mahakama na kutoa adhabu za gerezani dhidi ya Waislamu katika dhurufu zisizo za kibinadamu, bali walianza kuzua mashtaka hata katika maeneo ambayo hukumu ya gerezani inatekelezwa. Haya hapa kwenu baadhi ya matukio haya meusi:

Mirzaparot Mirzacharibov alihukumiwa mjini Petersburg kifungo cha miaka 5 kwa sababu ya uanachama wake kwa Hizb ut Tahrir. Alipofika gerezani mnamo 21 Machi 2019, kikundi cha "wanaharakati" kilimpiga kikatili. Alipoingia kwenye chumba cha idara ya "utekelezaji adhabu ya  Urusi" gerezani, mfanyakazi aliweka kisu shingoni mwake, na kisha, pamoja na mfanyakazi mwingine, wakaanza kuuliza maswali juu ya Hizb ut Tahrir. Mirzaparot alijibu maswali ya wafanyikazi hao wawili na kuwaambia juu ya kazi ya Hizb. Alisisitiza kuwa kazi yake ni ya kifikra na haitumii mbinu za kimada na kwamba kesi yake ni ya uongo, kwani amehukumiwa kwa (ugaidi) kulingana na Mada ya 205, Kifungu 2, Sehemu ya 1 ya Kanuni za Adhabu, na baada ya miaka mitano gerezani alihukumiwa upya, miaka mitatu gerezani, na kwamba lazima atumikie miaka miwili katika gereza la chumba, na mwaka katika gereza la juu.

Galolin Rinat, mkaazi wa mji wa Chelyabinsk. Galolin alifungwa miaka 5 katika gereza la juu kwa sababu ya uanachama wake katika Hizb ut Tahrir. Katika siku ya kuachiliwa kwake, mashtaka mapya yalipangwa dhidi yake, kwa hivyo alikamatwa na kuzuiwa kutoka gerezani, na akatumwa kwa ajili ya uchunguzi. Mnamo 17 Agosti 2018, alihukumiwa tena kifungo cha miaka 8 gerezani, kulingana na Mada ya 205, Kifungu cha 5, Sehemu ya 2, kilichoitwa "Kushiriki katika shughuli za shirika la kigaidi." Hii ni licha ya ukweli kwamba Hizb ut Tahrir sio shirika (la kigaidi) na haiwezi kuainishwa kama hivyo.

Rehman Haggayev Zikrullah alihukumiwa jijini Moscow kifungo cha miaka 7 kwa uanachama wake katika Hizb ut Tahrir. Baada ya kumaliza hukumu yake, alihukumiwa tena kwa kulingania fikra za Hizb ut Tahrir kati ya wafungwa, na mnamo 13 Disemba 2018, alihukumiwa kulingana na Mada ya 205, Kifungu cha 5, Sehemu ya 2 ya Kanuni ya Adhabu ya Shirikisho la Urusi, na alihukumiwa kifungo cha miaka 14 na nusu gerezani. Hiyo ni, alimtaja Mwenyezi Mungu baada ya kukaa gerezani miaka 7 kwa tuhma za kufanya kazi na Hizb ut Tahrir, na akafungwa tena kwa tuhma hiyo hiyo, lakini kwa lugha mpya, na kwa kifungo cha gerezani mara mbili.

Mnamo 27 Januari 2021 M, ilithibitishwa kuwa uamuzi kama huo ulitolewa dhidi ya mkaazi wa Kazan, Usmanov Zakir John. Na mnamo 2017, alihukumiwa kifungo cha miaka 6 kulingana na Mada ya 205, Kifungu cha 5, Sehemu ya 2, na mnamo Oktoba 2020, Mahakama ya Eneo la Mashariki ya Jeshi ilitoa adhabu nyingine ya kifungo cha miaka 9 katika gereza la juu kulingana na Mada ya 205, Kifungu cha 1, Sehemu ya 1, "Ulinganizi kwa Shirika la Kigaidi", Mada ya 205, Kifungu cha 2, Sehemu ya 1, "Kutetea hadharani ugaidi," ambayo inahitajika kukaa katika vyumba vya gereza kwa miaka 5 kutoka katika asili ya miaka 9.

Asgat Hafizov, na ambaye alihukumiwa mnamo Disemba 2017 miaka 17 na nusu gerezani. Waliongeza kwenye mada ambayo alikuhukumiwa kwayo, ambayo ni kuratibu shughuli za (kigaidi) (Mada 205, Kifungu cha 5, Sehemu ya 1 ya Kanuni za Adhabu) na misimamo mikali (Mada ya 282, Kifungu cha 2, Sehemu ya 1 ya Kanuni za Adhabu) , na waliongeza shtaka jengine la kushiriki katika shughuli za (kigaidi) (Kifungu cha 205, Kifungu cha 5 Sehemu ya 2 ya Kanuni za Adhabu) na pia kusajili wanachama kwa shirika (la kigaidi) (Kifungu cha 205 Kifungu cha 1 Sehemu ya 1).

Na hapa kadhia nyengine mpya inahukumiwa dhidi ya mshtakiwa kwa kifungo cha miaka 16 gerezani, mwanachama wa Hizb ut Tahrir Hamid Igamberdiev, ambaye amehamishwa kutoka gereza la Belgorod kwenda kifungoni kwa faragha jijini Moscow.

Kila moja ya hali hizi ni dhulma dhahiri, na wakati huo huo bado hazionyeshi vya kutosha uhakika wa unyama katika kuamiliana na wafungwa wa Kiislamu, haswa mashababu wa Hizb ut Tahrir.

Mtetezi mkuu wa haki za binadamu wa Urusi Lev Panamaryov anasema ni vigumu kuvumilia ukatili wa utawala huu. Katika kalima yake ambayo aliitoa kwenye muhadhara ulioandaliwa na Kituo cha Kimataifa cha Kumbukumbu, Lev Panamaryov alisema: "Waislamu kutoka Hizb ut Tahrir hawakushtakiwa kwa kutekeleza au kujiandaa kwa vitendo vya kigaidi, hawakushtakiwa kwa vitendo hivyo au katika uamuzi wowote wa mahakama, wamehukumiwa vifungo vya kushangaza hadi miaka 24, miaka 20, miaka 18, lazima tupige kelele kila kona juu ya suala hili ... Majaribio hufanywa mara kwa mara na watu hufungwa zaidi na zaidi, hadi kufikia mamia, na wengine wao wamefungwa kwa mara ya pili, na kwa maoni yangu, huu ndio ufashisti halisi. "

Mwenyezi Mungu (swt) asema,

وَمَا نَقَمُوا مِنْهُمْ إِلَّا أَنْ يُؤْمِنُوا بِاللَّهِ الْعَزِيزِ الْحَمِيدِ﴿.

" Nao hawakuona baya lolote kwao ila kuwa wakimuamini Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Msifiwa" [Al-Buruuj: 8]

Hizb ut-Tahrir sio chama (cha kigaidi), na shutuma kama hizo dhidi yake si chochote bali ni uongo wa kulaaniwa, ambao unaweza kukanushwa kwa urahisi kwa kuangalia tu historia ya chama na shughuli zake za muda mrefu tangu kuanzishwa kwake 1953.

Tunamshukuru Lev Panamaryov na Kituo cha Kumbukumbu cha Kutetea Haki za Binadamu kwa kushughulikia kwao suala la wafungwa wa kisiasa wa Kiislamu, na kwa shughuli yao ya kutetea wale wanaoteswa katika kesi za Hizb ut Tahrir. Tunashukuru pia mashirika mengine yote ya haki za binadamu, mawakili, watetezi wa haki za binadamu na wanaharakati kwa kutetea maslahi ya wafungwa wa kisiasa wa Kiislamu, na wale wote ambao hawakubakia kwenye msimamo wa kati na kati na kutoa msaada kwa wafungwa wasio na hatia wa Kiislamu. Tunamuomba Mwenyezi Mungu awajalie subira wafungwa wa Kiislamu na familia zao, hakika Mwenyezi Mungu yuko pamoja na wenye kusubiri.

Mh. Salah Eddine Adada
Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari

ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu