- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan: Huku Mwezi wa Ramadhan, Mwezi wa Ushindi, Unapokaribia, Umma na Majeshi yake lazima Yakabiliane na Mfumo wa Kilimwengu wa Kidhalimu wa Marekani!
Kati ya tarehe 7 na 11 Februari 2025, wanajeshi kadhaa wa majini wa Kiislamu watashiriki katika zoezi la (Aman 25) jijini Karachi, Pakistan, ambayo lengo lake ni "kuamiliana kwa pamoja katika kushughulikia vitisho vya baharini." Je! ni tishio gani kubwa la baharini kwa usalama wa Waislamu kuliko Jeshi la Wanamaji la Marekani? Jeshi la Wanamaji la Marekani linashambulia Waislamu na kulisaidia umbile la Kiyahudi katika mauaji ya halaiki ya watu wa Gaza. Pamoja na hayo, Jeshi la Wanamaji la Marekani limetenganishwa na ulimwengu wa Kiislamu na bahari, kwa hivyo linategemea watawala wa Waislamu, kwani watawala vibaraka wa Waislamu wanawapa Jeshi la Wanamaji la Marekani kambi za kijeshi na njia za baharini, ambayo pasi kwayo, Amerika haingeweza kushambulia Waislamu. Ramadhan ni mwezi ambao ndani yake Umma wa Kiislamu ulishinda maadui wengi wenye nguvu. Hebu Waislamu na waregeshe hukmu kwa Kitabu cha Mwenyezi Mungu ﷻ katika mwezi wa Ramadhan, na warudishe ushindi dhidi ya maadui, kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu ﷻ.
Imetayarishwa na: Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan
Jumatatu, 11 Sha'aban 1446 H sawia na 10 Februari 2025 M
Kwa Maelezo zaidi, Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan
Tovuti Rasmi: Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan
Facebook: Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan
Twitter: Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan