Ijumaa, 25 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  21 Muharram 1446 Na: H 1446 / 07
M.  Jumamosi, 27 Julai 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kwa Shangwe na Nderemo ya Hali ya Juu, Bunge la Marekani Lilimkaribisha Muuaji wa Gaza!
(Imetafsiriwa)

[قَدْ بَدَتِ الْبَغْضَاءُ مِنْ أَفْوَاهِهِمْ وَمَا تُخْفِي صُدُورُهُمْ أَكْبَرُ]

“Imekwisha fichuka chuki yao katika midomo yao. Na yanayo ficha vifua vyao ni makubwa zaidi.” [Aal-i-Imran: 118]

Baada ya miezi kumi ya mauaji ya kila siku dhidi ya watu wa Gaza, ambayo yanatangazwa muda baada ya muda kwa sauti na picha za hali ya juu, kwa idadi, takwimu, ushuhuda na hukumu za mahakama... baada ya yote hayo, Bunge la Congress lilimpokea kiongozi wa Baraza la Vita huko Gaza, Waziri Mkuu wa umbile la Kiyahudi Netanyahu, kwa karamu ya nderemo na shangwe kana kwamba yeye ni mmoja wa mashujaa wa watu wao. Sauti yao ya ndani ikisema: Tunataka kukupa ujira, Netanyahu, kwa kuwaua Waislamu wa Gaza kwa niaba yetu. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[إِن تَمْسَسْكُمْ حَسَنَةٌ تَسُؤْهُمْ وَإِن تُصِبْكُمْ سَيِّئَةٌ يَفْرَحُواْ بِهَا]

“Ikikupateni kheri huwaudhi. Na ikikupateni shari wanafurahia.” [Aal-i-Imran: 120].

Vitendo vinaendelea kuthibitisha kwamba Magharibi kafiri ya kikoloni inautazama tu Umma wa Kiislamu kama watu walioshindwa, na kwamba nchi zake ni makoloni yake. Lau nchi za Magharibi zingeweza kuwafutilia mbali Waislamu katika uso wa ardhi, zingefanya hivyo. Katika mawazo ya Magharibi, Vita vya Msalaba havijamalizika, lakini vimepewa tu majina mapya. Haichukui muda mrefu kutoka katika enzi moja ya ukoloni kabla ya kuingia nyingine; kubadilisha sura na majina lakini sio vitendo; mashambulizi ya kijeshi, kiuchumi na kithaqafa, kuwanyima haki ya Waislamu kwa ubinadamu wao, hata kujilinda wao wenyewe, nchi zao na imani zao, na inatoa uungaji mkono wa wazi kwa watawala vibaraka wahalifu wanaofungua milango ya nchi kwa ajili ya kupora kwao na kwa ajili ya madhara ya ukoloni wake.

Hakika, kafiri Magharibi ilirithi chuki kwa Uislamu kutoka kwa mababu zake wa vita vya msalaba! Ingawa ilipitia njia ya nuru iliyoitoa katika giza la Zama za Kati, moyo wake ungali unaishi katika giza hilo, hasa wakati inapoamiliana na Uislamu na Waislamu. Hii ndiyo sababu inayowafanya bado wanaogopa kufungua akili zao kwa Uislamu, na mfano rahisi zaidi wa hili ni vita vyake dhidi ya staha ya Waislamu, ingawa inatambua kuwa ni ustaha!

Hii ndio Magharibi na hawa ndio wanasiasa wake wanaosimama wakimpigia makofi muuaji wa Gaza, mhalifu Netanyahu!

Enyi Waislamu... Enyi Umma bora ulioletwa kwa ajili ya wanadamu: Ni lazima tuijenge dunia yetu haraka, dunia kwa ajili ya Waislamu, ambamo uaminifu wao umehifadhiwa na Dini yao imeinuliwa, dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Jueni kwamba maisha yenu hayatakuwa na utulivu isipokuwa musimamishe dola inayotawala kwa Uislamu. Njia ya ustawi ni kuwapindua watawala wasaliti, kuregesha mamlaka, kusimamisha utawala wa Uislamu, na kufukuza ushawishi wa mkoloni kafiri Magharibi kutoka katika ardhi zetu.

Enyi Waislamu... Enyi Wamiliki wa Mimbari, Majukwaa na Vyombo vya Habari:

Tazameni walivyompigia makofi yule muuaji wa Gaza huku mikono yake ikiwa bado imelowa damu ya watu wa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina! Je, hilo halikuudhini kuufikiria upya ujumbe wenu katika kuufahamisha Umma wa Kiislamu kuhusu kadhia zake?! Umbile la Kiyahudi na Wakoloni makafiri wa Magharibi walio nyuma yake waliweza kuiangamiza Gaza huku kamera zenu zikirekodi matukio na kupeperusha hewani muda baada ya muda. Waliweza tu kufanya hivyo kwa sababu walihakikishiwa kwamba majeshi ya Waislamu yangepewa amri kali ya kutosonga. Majeshi haya ambayo askari wao ni watoto na ndugu zenu, ambayo yanalipwa na kufunzwa kwa pesa na mali zenu. Kwa hiyo msisimame kimya, bali semeni kuhusu wajibu wa watu wenye nguvu na ulinzi wa kuhamasisha majeshi na kuwapindua watawala hawa wahalifu wasaliti.

Enyi askari katika majeshi ya Waislamu: Mumefungiwa kambini kwa muda wa miezi kumi, mkiwatazama Mayahudi wakiiangamiza Gaza na kuwaua watu wake. Mtakutana na Mwenyezi Mungu kwa uso gani Siku ya Kiyama, hali watu wa ardhi iliyobarikiwa wameuawa mbele yenu na nyinyi mna silaha mikononi mwenu?! Yako wapi mapenzi ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake na Waumini? Je, mnamuabudu Mwenyezi Mungu na mnampenda Mtume wake, au mnawaabudu watawala wenu na mnawapenda dinari zao? Uungwana, ujasiri, na ari yenu iko wapi? Mnajiandaa kwa vita gani? Je, sio wakati wa nyinyi kutambua kwamba watawala hawa hawatakupeni uhuru wa kutembea isipokuwa kuvunja nyumba za watu wenu juu ya vichwa vyao? Kwa hivyo, mnangoja nini Uislamu unakuhitajini musonge sasa ili kuwaokoa watu wa Palestina kutokana na uhalifu wa umbile la Kiyahudi. Ikiwa watawala watasimama kwenye njia yenu, ni wajibu wenu kuwachukulia hatua kwa usaliti wao. Sasa ni wakati wa kusahihisha mwenendo wa hatua, kwa hiyo songeni ili kunusuru Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina, kwani Ummah mzima unakungojeni na uko tayari kutembea nanyi kwenye njia ya ukombozi kutokana na ukoloni na ushawishi wake. Kwa hiyo mtafanya nini?

Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[وَالَّذِينَ آوَواْ وَّنَصَرُواْ أُوْلَئِكَ هُمُ الْمُؤْمِنُونَ حَقّاً لَّهُم مَّغْفِرَةٌ وَرِزْقٌ كَرِيمٌ]

“Na walio amini wakahama na wakapigana Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na walio toa mahala pa kukaa na wakanusuru, hao ndio Waumini wa kweli. Watapata msamaha wa Mwenyezi Mungu na kuruzukiwa kwema.” [Al-Anfal: 74].

Mhandisi Salah Eddine Adadah
Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu