Jumamosi, 26 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  19 Rabi' I 1446 Na: H 1446 / 028
M.  Jumapili, 22 Septemba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kauli za Aibu za Waziri wa Mambo ya Nje wa Jordan
(Imetafsiriwa)

Kufuatia mkutano wa ile inayoitwa “Kamati ya Mawaziri wa Kiarabu na Kiislamu iliyopewa jukumu la kuchukua hatua za kimataifa kukomesha vita dhidi ya Gaza,” Waziri wa Mambo ya Nje wa Jordan Ayman Safadi alitoa kauli za aibu kwa waandishi wa habari ambazo haziendani na uzito wa tukio ambalo kwalo walikuwa wamekusanyika. Alizungumza kuhusu makubaliano ya amani kati ya Jordan na umbile la Kiyahudi, na kwamba sasa ilikuwa inakusanya vumbi. Alisema kuwa kupamba moto kwa umbile la Kiyahudi kunalisukuma eneo lote ndani ya shimo, na kwamba eneo hilo linapitia awamu yake mbaya zaidi kwa kuzingatia kupoteza matumaini ya kupatikana kwa amani. Aliongeza: “Hatuamini kwamba kufutilia mbali makubaliano ya amani kutaitumikia Jordan na Palestina, na tunayatumia makubaliano hayo kulinda maslahi ya Jordan na kuwatumikia watu wa Palestina.” Akijibu swali la mwandishi wa habari, alisema: “Machaguo yote yaliyopo mezani kukomesha uvamizi wa Gaza yanazingatiwa,” akibainisha kuwa uvamizi huo umekuwa changamoto hata kwa wafuasi wake, na kwamba vikwazo lazima viwekewe dhidi yake. Aliongeza: “Siku zote tunatoa tahadhari kuhusu kile kinachotokea katika Ukingo wa Magharibi.”

Kukabiliana na kauli hizi dhaifu zinazoelezea msimamo wa utawala wa Jordan na tawala zingine katika nchi za Waislamu, tunasema:

Kwanza: Tukio hili kubwa halihitaji “kamati ya wizara iliyopewa jukumu la kuchukua hatua za kimataifa kukomesha vita dhidi ya Gaza”, lakini linahitaji baraza la kijeshi ambalo linajumuisha askari wa majeshi ya Waislamu kuunda mpango wa kijeshi wa kuikomboa Palestina, kisha kuhamasisha majeshi hayo kulishambulia na kulimaliza umbile nyakuzi la Kiyahudi.

Pili: Tukio hili kubwa ambalo kwalo mumekusanyika linahitaji watu watukufu, sio wapumbavu wapuuzi wanaokariri maneno ya mabwana zao, Ruwaibidha (watawala duni watepetevu) wanaousambaratisha Ummah kwa kudumisha viti vyao vibovu, kufuja masuala ya Ummah, na kuyakabidhi kwa maadui zake.

Tatu: Waziri wa Mambo ya Nje wa Jordan anatetea makubaliano hayo ya aibu na uhaini na umbile la Kiyahudi, na anadai kuwa yanatumikia maslahi ya Jordan na watu wa Palestina, na kuzibeza akili za watu, kwa sababu watu wanajua kwa hakika kwamba kutumikia maslahi ya Jordan na watu wa Palestina kuko katika kuuondoa uvamizi huo na kuufutilia mbali uwepo wake, sio katika kuhitimisha makubaliano nao, kuulinda, na kuupatia uhai.

Nne: Umelikwepa chaguo sahihi linalopaswa kuchukuliwa, ambalo ni la kijeshi, kisha waziri anadai kuwa “chaguzi zote zilizowasilishwa ili kuzuia uvamizi wa Gaza ziko chini ya uchunguzi”, akiendelea kubeza akili za watu, kwa sababu chaguo la jeshi sio kati ya machaguo yaliyowasilishwa. Kisha anasema kwamba vikwazo lazima kuwekwa dhidi ya uvamizi, kwani hiki ndicho kikomo cha mamlaka yake, na kikubwa zaidi anachoweza kusema na kutangaza. Hainuki kwenye kiwango cha wanaume wenye upeo mkubwa, walio tayari kujitolea muhanga nafsi zao na mali zao ili kuzima uchokozi na kumkomboa mvamizi kutoka katika ardhi ya Waislamu.

Tano: Ni hatari gani hii unayodai kuwa siku zote unatahadharisha!? Je, haijakujia kufikiria suluhisho sahihi la kuondoa hatari hii badala ya kutahadharisha, ili uchukue msimamo wa wanaume na utambue kuwa uchokozi kwa nguvu unahitaji nguvu mithili yake ili kuukomesha, ili uondoe hatari hii badala ya kujishughulisha na kutahadharisha kwake?!

Sita: Waziri bado ana matumaini ya kupata amani, amani na wale wanaonyakua ardhi, wanaokiuka matukufu, wanaoua watu, kuwahamisha na kuwaweka njaa, kwa hivyo hadith ya Mtume (saw) ni kweli juu yao: «... إِذَا لَمْ تَسْتَحْيِ فَاصْنَعْ مَا شِئْتَ» “Ikiwa huoni haya yoyote, basi fanya chochote upendacho.” Adui anayekalia kwa mabavu anafanya kile anachofanya na waziri, wenzake na mabwana zao wanaimba juu ya amani naye. Hawa ni watu wa aina gani? Na wanapima kwa kipimo gani?!

Saba: Waziri huyu, wenzake na mabwana zao wanakariri maneno ya mabwana zao katika miji mikuu ya nchi za Magharibi, wakielezea hofu yao ya maji kuzidi unga katika eneo hilo, na kuteleza kwake kuelekea shimoni na hofu yao ya vita vya kieneo. Hebu waziri na ajue - ikiwa hajui - kwamba nchi za Magharibi zinahofia hatua ya Umma wa Kiislamu ya kuliondoa umbile la Kiyahudi. Kwa sababu hii, ilikuja na manuari zake, ndege na vikosi hadi eneo hilo, ikifikiri kwamba inaweza kuuzuia kusonga ikiwa unataka.

Nane: Watawala wajinga wa Waislamu na wafuasi wao wanaendelea kuimba nje ya kundi la Ummah. Ummah umetambua kwamba maafa yake yako kwao, na upeo wa matakwa yake umepanda mpaka umewapita. Hakuna kilichosalia isipokuwa kuwarukia, kuuondolea udhibiti wao juu ya shingo zake, na kuyakabidhi mambo yake kwa waaminifu na wenye fahamu miongoni mwa watoto wake ili kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Kisha majeshi yasonge ili kuliondoa umbile la Kiyahudi kutoka kuwepo.

Hatimaye, watawala wetu wa Ruwaibidha na washirika wao wamezoea udhalilifu na fedheha, na hawajajua ladha ya utu uume, fahari na utu. Wametosheka kuwa wafuasi wa makafiri wakoloni, na walinzi wa umbile la Kiyahudi, na wanashuhudia uhalifu wake dhidi ya watu wa Palestina na kwengineko, na hawaoni chembe ya heshima, wala hawahisi miguno ya usaliti. Wabora wao zaidi ni wale wanaokariri maneno ya mabwana zao wa nchi za Magharibi, wakiningi'a katika uongo wa jumuiya ya kimataifa, sheria za kimataifa na Umoja wa Mataifa, ambazo zilianzishwa kimsingi kwa ajili ya vita dhidi ya Uislamu na Waislamu. Wamekuwa ni wasaidizi wa Magharibi katika vita vyake dhidi ya Uislamu na Waislamu, na pengine bishara njem itakuja moja baada ya nyingine kwa utambuzi wa Ummah kwa watawala hawa, na hivi karibuni wataanza kunguruma nyusoni mwao, pamoja na Mayahudi na Magharibi nyuma yao, na siku hiyo iko karibu, Mwenyezi Mungu akipenda.

Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu