Jumapili, 26 Rajab 1446 | 2025/01/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  12 Jumada I 1446 Na: H 1446 / 047
M.  Alhamisi, 14 Novemba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mkutano wa kilele wa Riyadh: Ushahidi kwa Usaliti wa Viongozi wa Waislamu dhidi ya Gaza na Lebanon
(Imetafsiriwa)

Zaidi ya siku 400 baada ya vita vya mauaji ya halaiki vilivyoanzishwa na umbile nyakuzi, halifu la Kiyahudi dhidi ya watu wetu huko Gaza, vita ambavyo havijawahi kushuhudiwa tangu Vita vya Pili vya Dunia, na kufuatia mauaji na uharibifu uliofuata nchini Lebanon, viongozi wa Waislamu walikutana jijini Riyadh kwa kile walichokiita kuwa ni “mkutano wa ajabu.” Matokeo, hata hivyo, hayakuwa chochote ila mfululizo wa maamuzi dhaifu ambayo yanaweza tu kusifiwa kuwa ya khiyana.

Walitoa wito wa “aina zote za uungaji mkono wa kisiasa na kidiplomasia” na “ulinzi wa kimataifa” kwa watu wa Palestina, na kulitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupitisha azimio la lazima la usitishaji vita mjini Gaza na kuweka vikwazo vya silaha kwa umbile la Kiyahudi. Ilhali matakwa haya hayabaki zaidi ya wino kwenye karatasi. Kwa nini? Kwa sababu hawakupendekeza mpango au utaratibu wa kutekeleza hata maombi haya madogo. Matakwa yao yalikuwa sawa na, au hata yenye athari kidogo kuliko yale ya maandamano ya umma. Angalau katika maandamano, sauti zinasikika pakubwa mabarabarani na viwanjani, na hata kuwasumbua watoa maamuzi katika miji mikuu ya kikoloni. Matakwa ya mkutano huo, hata hivyo, hayakuwa chochote zaidi ya sauti hafifu zilizofungiwa ndani ya kuta za vyumba visivyovujisha sauti.

Kwa hakika, baada ya kutoa matakwa haya matupu, ambayo yanadhihirisha usaliti wa Gaza na Lebanon wa watawala wa Waislamu, Waarabu na wasio Waarabu, washiriki wa mkutano huo walihamisha angazo lao kutoka kwa dori yao kuu kama waliopewa na mabwana zao wakoloni wa Magharibi, wakiongozwa na Marekani: kupanga upya miradi ya usaliti, utiishwaji, na utegemezi.

Kufuatia shutma zao za kihuni dhidi ya vitendo vya umbile la Kiyahudi huko Gaza na Lebanon, watawala hao watiifu walisisitiza umuhimu wa kupatikana kwa “amani” umbile hilo, na kuhalalisha kikamilifu wizi wake wa robo tatu ya Palestina. Walisisitiza tena dhamira yao ya suluhisho la dola mbili, ambalo linahusisha kuanzisha umbile la Wapalestina lisilo na nguvu za kijeshi, lililovuliwa ubwana kwenye kile kinachoitwa mipaka ya kabla ya Juni 4, 1967.

Umefika wakati sasa kwa Umma wa Kiislamu kuchukua hatua madhubuti dhidi ya watawala hawa, kuwapindua kutoka kwenye viti vyao vya enzi na kurudisha mamlaka yake iliyonyakuliwa. Hili linaweza kupatikana tu kwa kuwapa watu wenye ikhlasi ndani ya majeshi yake msaada unaohitajika ili kuisaidia Hizb ut Tahrir katika kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Khilafah kama hiyo italifutilia mbali umbile la Kiyahudi, itaikomboa Palestina yote kuanzia kwenye mto hadi baharini, na kuiregesha mahali pake panapostahiki. Bila ya hili, Umma na majeshi yake hawawezi kusalimika mbele ya Mwenyezi Mungu, Mtukufu na Mlazimishaji. Siku ya Kiyama wataulizwa juu ya kimya chao na kutelekeza kwao Uislamu na Waislamu.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا مَا لَكُمْ إِذَا قِيلَ لَكُمُ انْفِرُوا فِي سَبِيلِ اللهِ اثَّاقَلْتُمْ إِلَى الْأَرْضِ أَرَضِيتُمْ بِالْحَيَاةِ الدُّنْيَا مِنَ الْآخِرَةِ فَمَا مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا فِي الْآخِرَةِ إِلَّا قَلِيلٌ]

“Enyi mlio amini! Mna nini mnapo ambiwa: Nendeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu, mnajitia uzito katika ardhi? Je, mmeridhia maisha ya dunia kuliko ya Akhera? Lakini starehe za maisha ya dunia kulinganisha na ya Akhera ni chache.” [Surat At-Tawba:38]

Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu